We! Nini unatufundisha hapa Mzee Mwanakiji? Nikiangalia picha ya sura nakutathmini umri wako haundeni na umri wa mtu kujiandaa kutoa bali kupokea mahali. Au ndo kutekeleza usemi wa Ngombe hazeeki maini?! (Mimi Mjukuu wako Babu hivyo hii ni utani tu tusijenge chuki tafadhari)
Maana siasa za majukwaa tumeona zimetutoa na kutufikisha wapi. Na tafsiri ya uhusiano kati ya uchumi na siasa imeonekena kuendelea kuwa msamiati mgumu wenye maana isiyotekelezeka kwa Wadanganyika. Kwa kuwa tunakabiliwa na hatari ya kuvunja rekodi ya kuhamisha majukwa ya siasa za adhalani kuhamia janvi la mtandao kisha kujiita wanamabadiliko, wafurukutwa/wakereketwa, wapendamaendeleo, wanaharakati huku tukiongeza maji baharini, udongo juu ya kichuguu, sukari kwenye asali, chumvi kenye nyongo.
Hili limekuwa swali gumu sana kwangu kama mwanachama wa JK 2007. Hivi kwa upeo wa wana JF nani ameyasikia au kuyaona matatizo ya Danganyika tuliyojadili mwaka 2007 kwa mara ya kwanza? au nani kaleta mada mpya kabisa juu ya matatizo ya Danganyika Republic katika 2007? Labda hebu tukumbushane; katika majumuhisho tumejadili yafuatayo kwa urefu:
1. Ubadhilifu na Ufisadi
2. Upendeleo katika zabuni na ajila
3. Udini na ukabila
Mijadala ni muhimu tena sana lakini ni fanisi iwapo inaishia kwenye maazimo yanayotekelezeka. Vinginivyo hizo ni porojo sawa na za wamachinga wa Kigogo Sambusa ama wazee wa balaza la kahawa Yombo Vituka au wacheza pool popote Danganyika Republic. Hivi hawa watajwa hapo juu hawajui haya matatizo japo katika upeo tofauti? Na je tunajitofautisha nao vipi kimatendo?
Somo hilo hapo juu limekuwa ujumbe wangu mara kwa mara hapa JF. Sasa napendekeza mwaka huu 2008 uwe wa mabadiliko yenye kuonyesha tofauti ya waziwazi kati ya wapiga porojo na watendaji waungwana kwa kuhitimisha mijdala yetu kwa Maazimio na kuyatekeleza. Hebu tuweke mpango mkakati wa mwaka 2008.
Utume wangu katika mwaka huu 2008 ni kuanzisha Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji Vijana litakalotengeneza mabepari wa ndani baada ya miaka kumi. Kama wewe ni Mfanyabiashara mwenye umri chini ya miaka 32 tafadhari wasiliana nami haraka kupitia 0754 917205. Njooni tupange mikakati ya kumiliki uchumi wa nchi yetu yenye asali na maziwa. Kwa Danganyika Republic Siasa haiwezi kujenga uchumi bali kuuporomosha.