Mababu na Mabibi wa zamani na Story zao

KACHINJA

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
1,263
Reaction score
869
Walikuwa wanatudanganya sana na maneno yao ambayo walikuwa wakituaminisha ambayo akiyafikilia sasa unaona kabisa hayana maana.

Mfano
-ukimruka mwezio anakuwa mfupi

-ukiwa unakula chakula kikadondoka chini usiokote anakula babu yako aliyefariki au malaika

-wamama wajawazito wakila mayai watoto watazaliwa bila nywele

-usiku ukienda kwa jirani kuomba chumvi useme naomba dawa ya jikoni

-ukiona mvua inayesha na jua likiwaka basi ujue sima anazaa

-upende wa mvua unaambiwa nyoka anakunywa maji maharini

Weka na yako inayoikumbuka:-


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mala ukinyooshea kidole kaburi unatakiwa uking'ate kidole chako eti ni mwiko

Mala eti hutakiwi kumwita mtu usiku alieko mbali kwa kulitaja jina lake

Mala usifagie usiku

Mala hupaswi kuuliza mungu kaumbwa na nani

Mala hupaswi kutaja jina la nyoka usiku kama unapiga stori kuhusu nyoka unatakiwa utumie neno la ziada kama mkanda nk

Ukiwa porini hupaswi kulitaja jina la nyoka aitwae koboko

Mala ukiwa unakula hupaswi kuongea

Hizo ni old taboos ambazo hazina nafasi kwenye ulimwengu huu wa 2019

Sent using unknown device
 
Ukila uku unaimba
unaolea mbali,
Usikae chini
ya miti
usiku
kuna mizimu,
Mkichangia
tundu la
kukojolea chooni
mama zenu
wanavimba
maziwa,
 
Hehehe!!
wazee popote mlipo
kuleni ngada
ntalipa
 
Ukimruka mwenzio kama amelala au kukaa unaambiwa umruke tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…