SoC04 Mabadailiko chanya katika Sekta ya Elimu

SoC04 Mabadailiko chanya katika Sekta ya Elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Calista Mselewa

New Member
Joined
May 30, 2024
Posts
2
Reaction score
1
Kwa miaka kadhaa sasa kumekua na wimbi kubwa la vijana wasomi mtaani wasio na ajira, jambo hili limekua likiwavunja moyo wanafunzi waliopo mashulen kwa wakati husika na kupelekea wanafunzi wengine kukatisha masomo yao kabla ya muda sahihi wa kumaliza shule na kisingizio kimekua ni “ hawaoni umuhimu wa kusoma kama kaka na dada zao waliosoma wapo nao mtaani hawana ajira” jambo hili linajenga hofu kubwa sana kwa taifa letu la sasa na hapo badae maana inaweza kupelekea kuongezeka kwa wahalifu,wavuta bangi wengi, kazi za utotoni ikiwa ndio njia za wao kupata hela, hivo basi mabadiliko yanahitajika.

Nini kifanyike ndani ya Sekta ya Elimu ndan ya miaka 5-25 ijayo.
  • Serikali itengeneze mtaala ambao unampa nafasi mwanafunzi kusomea kitu cha ndoto zake kuanzia anapoanza shule na sio kusoma masomo mengi kwa wakati mmoja ambayo badae mengine atayaacha na pia itapendeza zaidi elimu wayopata wanafunzi iwe ya vitendo na sio maandishi tu, darasa limpe mwanafunzi nafasi ya kufanya kwa vitendo mambo aliyojifunza darasani na ni vema mambo haya yafanyike kuanzia elimu ya chini hadi juu.

  • Inahitajika kuwepo na somo la kumfundisha mwanafunzi elimu ya kujitegemea ili kumjengea fikra na uwezo wa kujiairi pindi akimaliza masomo yake na sio awe na dhana ya kutegemea kuajiriwa pekee, elimu hii inapendeza iwe kuanzia ngazi ya chini(mashuleni) hadi ngazi za juu za kimasomo(vyuoni).

  • Pindi mwanafunzi anapofika elimu ya chuo basi mkopo au hela anayopata kujikimu asilimia kadhaa apewe kwa matumizi yake binafsi na asilimia nyingine ni kwaajili ya kumuwezesha katika shughuli aliyoanzisha au kujiajiri ambayo inaonekana na kutambulika sababu tunaamini elimu wameipata toka chini na hii inasaidia kuongezeka kwa kipato binafsi kwa mwanafunzi na serikali jambo hili litaleta picha nzuri kwa taifa kua na vijana wanaojishughulisha.

  • Tunaamini kwamba ajira ni matokeo mojawapo kutoka kwenye elimu, kwamba mtu akiajiriwa ataenda kutumia elimu aliyopata shuleni kwa vitendo. Hivo basi pindi ajira zinapotangazwa zitolewe kwa usawa (namaanisha ajira zitoke kwa fani mbali mbali sio fani baadhi tu) na nafasi zaidi ya moja, sio serikali kutoa nafasi moja ambayo inagombaniwa na watanzania zaidi ya elfu moja ni jambo halipo sawa.

Nini faida ya mabadiliko haya kwa taifa letu.
  • Kupitia elimu kwa vitendo taifa litaweza kupata vijana mbalimbali wenye uwezo wa kufanya tafiti na kutatua matatizo ndani ya jamii zetu na nchi kwa ujumla.
  • Kufahamu nini ndoto ya mtoto ya mwanafunzi tangu akiwa mdogo na kupewa nafasi ya kusomea kile anachokipenda na kua na ndoto nacho inaleta faida kubwa kwa jamii yetu kwa sababu tutapata sio wasomi wazuri tu pia wataalamu wabobevu wenye uwezo wa kutengeneza vifaa mbalimbali kama kompyuta,magari na kadharika na sio kutegemea kutoka nchi jirani.
  • Endapo kijana akawa na uwezo wa kujiajiri au anapata nafasi ya kuajiriwa kwa wakati baada ya kumaliza masomo yake hii inamsaidia asipoteze maarifa alionayo kama akikaa mda mrefu mtaani bila ajira yoyote ile.

Ni kweli elimu ni ufunguo wa maisha lakini kusoma na kubaki na hayo maarifa bila kufanyia kazi mahali popote ni sawa na bure, hivo basi yatupatasa kujishughulisha.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom