Sababu za mabadiliko haya yaliyotangazwa na Naibu waziri wa Elimu Bw. Mulugo! ni hizi zifuatazo: 1. Utata wa wanafunzi kukalishwa shule baada ya kumaliza mitaala ya masomo miezi mitatu kabla ya mtihani;2. Utata wa Ongezeko la gharama za uendeshaji shule kwa kuhudumia wanafunzi miezi mitatu bila kuwa na jambo jipya la kujifunza. Huu ni mzigo kwa Wenye shule, wazazi na serikali.
bas wizara iwe na msimamo na sera za kudumu siyo kila waziri na utaalamu wake
Badae utawekewa JK akiwa anabembea na mke wake, au akiwa na 50 cent au na Boys 2 men........... ni balaa. Inanikumbusha mfalme juha.Bw Paul hizi picha zimenifuhisha sana. Tehe tehe tehe teheee......!
Hii wizara kila anayeingia anakuja na utaratibu wake. Waliotoka walitaka elimu ya msingi iishie std 6 na wengine walitaka stv 8. Tutakuwa na msimamo mmoja lini?
kuna mantiki gani hapo?kwani mda huu unamadhara gani na maandalizi ya watahiniwa au inaathiri vipi maendeleo ya elimu hapa nchini? Msaada tafadhali mtoa maada.
Hapo kwa M Sita si kweli aliyefuta masomo uliyotaja ni Mungai na pia alikuwa na mpango wa kufuta History na Civics aweke somo litakaloitwa History with Civics Islamic na bible know yangefutwa na kuwa Dini Mseto,hvyo inathibitisha kauli yako kuwa hakuna Mtanzania mwenye msimamo endapo hata wewe mwenyewe umeshatuma kitu usichokijua,ila kauli ni too jenero kwa sababu kuna watu (waTZ) waliyaona hayo na waliyapinga na wamefanikiwa kwani walimu wa Bukipingi na biashara hasa shule binafsi walishapoteza ajira zao.:A S 465:MTANZANIA GANI MWENYE MSIMAMO?????? BAADA YA BABA WA TAIFA HAKNA MTU MWENYE MSIMAMO NDANI YA SERIKALI YETU. M NAKUMBA 2003/2004, WAZIRI WA ELIMU WAKATI HUO(JOSEPH MUNGAI) ALITAKA WATAKAO PATA DIVISION FOUR WASIPATE VYETI, IKAGUNDULIKA KUWA NA YEYE ALIPATAGA DIVISION FOUR, IKABIDI NA YEYE ARUDIE MTIHANI. AKAJA MWNGNE 2005- M.SITTA. AKATOA NA YEYE MTAZAMO WAKE. AKAFTA MASOMO YA BIASHARA ACHANGANYA BAADI YA MASOMO(eg,Chemistry + Physics, etc). Nani atakae KUWA NA MSIMAMO KTK NCHI HIIII????????? LABDA SERIKALI NZIMA IBADIRISHWE
kuna mantiki gani hapo?kwani mda huu unamadhara gani na maandalizi ya watahiniwa au inaathiri vipi maendeleo ya elimu hapa nchini? Msaada tafadhali mtoa maada.
Hatma ya wahitimu wa kidato cha sita itakuwa nini kuanzia 2014 katika kujiunga na elimu ya juu hapa nchini? Ilivyo sasa, Majibu yanatoka Mwisho wa April na mwanzoni mwa May. Udahili wa vyuo kupitia TCU unaanza April mpaka June. Applications TCU deadlines ni Early July. Notification of admission ni anytime August. Registration at Universities late Sept to early October. Swali linakuja kwamba ukibadilisha mihula ya Sekondari hawa wa kidato cha sita watajiunga lini na vyuo vikuu?
Hawa wenzetu wanapobadilisha mihula wanajua kuwa wanaathiri ratiba za vyuo vikuu? je, wakuu wa vyuo nao walihusishwa? TCU, HESLB???
Tusubiri Kasheshe 2014.
Bw Paul hizi picha zimenifurahisha sana. Tehe tehe tehe teheee......!
Kwani zamani ilikuwaje? Au wanafunzi hawakuwa wanajiunga na vyuo vya elimu ya juu? Manake enzi zetu mitihani ilikuwa inafanyika mwezi Novemba kwa Form 4 na mwezi May kwa Form 6. Hata hivyo ilibidi kusubiri mwaka mzima kujiunga na vyuo vikuu. Japo enzi hizo mwaka huo mzima tulikuwa tunaupotezea mitaani, safari hii vijana watautumia mwaka huo kupiga kwata JKT, period! Unataka nini tena?Hatma ya wahitimu wa kidato cha sita itakuwa nini kuanzia 2014 katika kujiunga na elimu ya juu hapa nchini? Ilivyo sasa, Majibu yanatoka Mwisho wa April na mwanzoni mwa May. Udahili wa vyuo kupitia TCU unaanza April mpaka June. Applications TCU deadlines ni Early July. Notification of admission ni anytime August. Registration at Universities late Sept to early October. Swali linakuja kwamba ukibadilisha mihula ya Sekondari hawa wa kidato cha sita watajiunga lini na vyuo vikuu?
Hawa wenzetu wanapobadilisha mihula wanajua kuwa wanaathiri ratiba za vyuo vikuu? je, wakuu wa vyuo nao walihusishwa? TCU, HESLB???
Tusubiri Kasheshe 2014.
Namkumbuka yule Waziri aliyekuja na hoja ya kufuta somo la Geography! Kweli TZ kichwa cha mwendawazimu
utaratibu huu unakuja serikali ikiwa na mpango wa wanfunzi wote kabla ya kwenda chuo wapitie JKT mwaka mmoja then wanajiunga vyuoni, maanake ukimaliza mei unaingia jkt mpaka mwakani june then ndo inafanya application chuo cheti cha kuhitimu jkt kikiwa ni kigezo muhimu kuingia chuo....GWARIDE HILO KAKA WANALO!
Madhara yake ni kwamba walimu wasahihishaji waendapo kusahihisha husababisha kutowafundisha wanafunzi waliobaki shuleni yaani(kidato cha I,II,III) Kwa kipindi cha Novemba na kidato cha V kwa kipindi cha machi,aprili na mei,kwa kufanya hivyo kwa mwakani kutawezesha walimu watakaochaguliwa kusahihisha mitihani hiyo kufanya kipindi cha likizo za Disemba kwa kidato cha nne na Juni kwa kidato cha sita,nimejaribu kukujibu tu mimi si mtoa mada ahsante kwa kuuliza.