SoC04 Mabadiliko ambayo Serikali inatakiwa kuyafanya katika tasnia ya habari

SoC04 Mabadiliko ambayo Serikali inatakiwa kuyafanya katika tasnia ya habari

Tanzania Tuitakayo competition threads

Herman mdede

New Member
Joined
Jun 8, 2024
Posts
4
Reaction score
3
Waandishi wa habari wengi Tanzania tunashindwa kupata ile ABC ya kutumia elimu kwasababu tunakosa msaada wa serikali katika tasnia hii. Mimi naamini ili mwandishi wa habari awe kamili na mtu anayefanya kazi katika hali ya kiwango lazima awe na vitendea kazi vitakavyo mwezesha yeye aweze kufanya kazi hiyo. Sasa waandishi wa habari wengi wanaishia kuwa machwa kwa sababu wanakosa vifaa kama kamera, maiki pamoja na kompyuta zenye uwezo.

Hivyo niiombe serikali tuitakayo ya miaka 25 ijayo tunaomba iweke mfumo wa mkopo ambao ni maalumu kwaajili ya vifaa vya mwanafunzi wa chuo kikuu anayesomea tasnia ya habari ili tupate waandishi wa habari waliokamilika

Niiombe tena serikali kuboresha sehemu za za mafunzo kwa vitendo za tasnia ya habari. Hii itasaidia wanafunzi hao kujua kikamilifu namna ya kutumia vifaa hivyo

Na mwisho niiombe serikali kuwainua waandishi wa habari kwa kutengeneza fursa mbalimbali kama uanzishaji wa Radio na televition ambazo zitakuwa maalumu kwaajili ya matukio ya nchi na dunia kiujumla🙏🙏
 
Upvote 6
Back
Top Bottom