SoC01 Mabadiliko Chanya Tanzania yanawezekana

SoC01 Mabadiliko Chanya Tanzania yanawezekana

Stories of Change - 2021 Competition

Rozney

New Member
Joined
Sep 11, 2021
Posts
3
Reaction score
3
Kumekuwa na mabadiliko makubwa katika huduma mbalimbali kabla na baada ya uhuru, kabla ya uhuru huduma zilikuwa zikitolewa zaidi kwenye maeneo ya shughuli za kiuchumi kama miji na mashamba makubwa, baada ya uhuru, huduma mbali mbali zimekuwa zikisambazwa kila eneo ili kuwafikia watu wengi zaidi, pia serikali ya Tanzania ilianza kuwa na ofisi za takwimu mara baada ya uhuru mwaka 1961.kabla ya uhuru ofisi hii ilikuwa Nairobi,Kenya ofisi ya takwimu ilipitia mabadiliko mengi hadi kufikia kuitwa ofisi ya Taifa ya takwimu (National Bureau of Stastics-NBS) Iliyozinduliwa rasmi tarehe 26 Mch 1999 kuwa wakala wa serikali ( Executive Agency).kwa mujibu wa sheria ya wakala wa serikali Na: 30 ya mwaka1997.Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ikiwa chini ya ya ofisi ya Rais,tume ya mipango iliundwa kutokana na iliyokuwa idara kuu ya takwimu (Central Bureau of Statistics) Ambayo ilikuwa inafanya kazi chini ya sheria ya takwimu Na.33 ya mwaka 1961 (Statistics Ordinance No 33 of 1961) sheria ambayo nayo ilifutwa kwa sheria ya Takwimu Na.1 ya mwaka 2002.Kama tulivyoona mabadiliko ya uchumi kabla na baada ya uhuru naomba serikali yangu tukufu iweze kubuni mbinu mbalimbali kuinua uchumi zaidi kwani maendeleo huletwa na ubunifu,mipango na utekelezaji.

Afya:
Ni ukamilifu wa binadamu kimwili, kiakili na kijamii na kutokuwepo na maradhi,Serikal inatambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi wote,afya bora ni raslimali muhimu kwa maendeleo.kwa kulitambua hilo,Serikali imekuwa ikishirikiana na taasisi za kidini kutoa huduma tiba zaidi kuliko Kinga, mwaka 1990 serikali ilijikita zaidi katika huduma za Kinga dhidi ya maradhi ya watoto wadogo na Mama wajawazito, kitu ambacho kinatiliwa mkazo ni utolewaji wa chanjo, kutolewa Elimu dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza pamoja na utolewaji wa huduma Bure za afya sambamba na ugawaji wa vyandarua. Sera rasmi ya Afya ilitayarishwa kwa kupitishwa mwaka 1990,msisitizo wa sera hii ulikuwa ni kuinua hali ya Afya kwa wananchi wote na kipaumbele kilitolewa kwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kuugua ambayo ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano,wanawake wajawazito, na wananchi wote.

Aidha sera hii ililenga kuweka mfumo wa huduma za Afya utakaokidhi mahitaji ya wananchi na kuongeza umri wa kuishi. Rais wa Kwanza wa Tanzania Mheshimiwa hayati Julius kambarage nyerere aliwahi kusema kuwa Kuna Maadui wakuu watatu wa kupambana nao ambao ni umasikini, ujinga na maradhi, Hivyo ili tuwe na mabadiliko Chanya, inabidi tujue jinsi ya kudhibiti Maaadui hawa watatu kwanza, katika suala la Afya Elimu inapaswa kutolewa ili watu waweze kujua vyanzo vya Magonjwa mengi ya mlipuko kama kipindupindu, maralia na hata gonjwa hili ambalo linaitesa dunia kwa sasa la Corona(COVID-19).Pamoja na jitihada ambazo nchi yetu imekuwa ikiweka katika suala la afya ila tatizo bado linakuwa ni vifaa vya kujifungua na madawa hasa sehemu za vijijini bado tunaomba serikali itazame suala hilo na kulifanyia kazi kwani Tanzania bora itajengwa na watu wenye Afya bora.

Maendeleo ya Jamii:
Kwa mujibu wa umoja wa Mataifa hutafsiriwa kama mchakato wa wanajamii kukusanyika pamoja kwa ajili ya kupata suluhisho la matatizo yanayowakabili, maendeleo ya jamii huwawezesha mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu wenye uhitaji wa kuwaletea mabadiliko kwenye jamii zao. Hivyo serikali inapopanga mipango ya maendeleo inapaswa imlenge mtu mmoja mmoja awezeshwe mtaji wa biashara au kufunguliwe viwanda ajira ziongezeke kwani Maendeleo huanza kwenye ngazi ya familia.

Utawala bora:
Ni mfumo wa utendaji unaozingatia uwazi, uadilifu na uwajibikaji, ili kuleta ufanisi katika sehemu za kazi, kiongozi anapaswa kusikiliza kero za watu wake na kutafuta njia ya kuzitatua kwa wakati, umoja na nia thabiti ya kufanya maendeleo kati ya wananchi na serikali yake vitafanya watu kuelewa nini cha kufanya na kina faida gani katika jamii.Uwajibikaji utahitajika katika kutimiza mikakati ambayo nchi imejipangia,viongozi wa nyanja mbalimbali kila mmoja na mahali alipopangiwa ajue wajibu wake na kuufanyia kazi bila kuvunja sheria za kazi yake,tunapozungumzia kiongozi Inamaanisha hata katika ngazi ya familia Kuna kiongozi ambaye anaweza kuhakikisha nyumba yake na watu wake wapo katika hali nzuri kiafya, Elimu,chakula na hata kuwa na makazi bora, Kama kila kiongozi wa ngazi ndogo ya familia ataiongoza vyema familia yake na kuwajibika kama baba au mama maendeleo ya nchi yatakuwa kwa kasi, Hivyo hivyo Kwa ngazi nyingine kama, kiongozi wa mtaa, kijiji, mkoa n.k,Utawala bora huanzia nyumbani katika ngazi ya familia.

Demokrasia:
Ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni sawa mbele ya sheria,na wanashirikishwa katika kufanya maamuzi ya kitaifa juu ya masuala ya umma,hivyo ni utaratibu ambao viongozi wa wananchi hupatikani kwa njia ya uchaguzi unaendeshwa kwa njia ya haki inayompa mwananchi uhuru wa kuchagua kiongozi anayemtaka. Nchi yenye democrasia na watu wake kuwa na uzalendo ni rahisi kuwa na maendeleo, kwa maana kila mtu atafanya kazi kwa bidii akitarajia mafanikio yake mwenyewe kwanza kabla ya mtu mwingine, nchi inapokuwa kiuchumi si faida kwa Rais wala makamo wake pekee bali ni sifa ya jamii Nzima na pia itafanya urahisi wa maisha kwa kila mtu mfano ikijengwa barabara nzuri ni sifa ya nchi kwa ujumla, kukiwa na maji Safi kila mtu atatumia yeye na kumwagilia bustani na hata kunywesha mifugo yake.,hivyo democrasia ni muhmu ,kwani hakuna maendeleo yoyote yatafanyika kama nchi Itakuwa na vita.Nchi bora huundwa na democrasia pamoja na uzalendo.

Kilimo:
Ni uzalishaji wa mazao kwenye mashamba,kilimo kina maana Pana inayojumuisha mifumo ya uzalishaji mimea, ufugaji wa wanyama na uvuvi wa samaki, ili tuwe na maendeleo thabiti inafaa tuwe na mazao ya kutosha yaliyolimwa kitaalam ambayo pia yatatuwezesha kupata masoko ya nje na kutuingizia pesa za kigeni, mfano mazao ya biashara kama pamba, katani na mengineyo.Ili kuboresha kilimo nchini, serikali inapaswa kuboresha sekta ya kilimo kwa kuagiza mbegu bora, dawa za kuulia wadudu, kuongeza wataalam pamoja na ununuzi wa trekta.kwa wakulima wadogo wanaweza jiunga vikundi na kukopeshwa vifaa vya kilimo ili kufanya kazi kwa umoja ,kukiwa na vitendea kazi vya kutosha tutakuwa na mazao mengi na bora ambayo tunaweza kuuza hata nje ya nchi yetu, serikali iingilie kati na kutilia msisitizo kilimo kwani ndio uti wa mgongo wa nchi yoyote ile,kukiwa na njaa nchini, hakuna jambo litafanyika hivyo kabla ya yote nchi inapaswa ijihakikishie kuna chakula cha kutosha,Nchi bora hujengwa na wananchi wenye chakula bora.

Biashara:
Ni mfumo wa kubadilishana bidhaa na pesa,kipindi cha nyuma watu walikuwa wakibadilishana bidhaa kwa bidhaa mfano mahindi kwa kuku,chumvi kwa mchele na vingine tofauti tofauti kwa makubalino na kipimo maalumu,kwa sasa kila bidhaa inabadilishwa kwa pesa,hata huduma mbalimbali zimepangiwa gharama ya malipo huku ikiunganishwa na Makato ya serikali(VAT),pamoja na makato ambayo yanakatwa kwa ajili ya kujenga nchi yetu ila serikali inapaswa kutafakari je makato hayo yanalingana na vipato vya wananchi wake,kuna makato ya vocha za simu na matumizi ya kutuma na kutoa pesa. Naomba serikali itazame kwa jicho la tatu kwani asilimia kubwa ya wanaotumia huduma hizo ni watu wenye hali ya chini ambao wanajikusanya kuwekeza vijisenti kwenye simu na kuwatumia wazazi vijijini ili wabadili mboga na kununua mitumba angalau wajisifu kuwa wana watoto waishio mjini,huu ni ukweli ulio wazi kuwa wanaoweka pesa kwenye simu asilimia kubwa ni wajasiliamali wadogo ambao bado hawajakuwa na uwezo mkubwa kufungua account za benki,zamani walizoea kuweka pesa kwenye vibubu lakini sasa wamepata urahisi wa kutembea na pesa kwenye simu zao.Leseni za biashara pia ziendane na thamani ya Bidhaa husika. Suala la wajasilamali wadogo kulipa elfu 20 kwa mwaka kama kodi ya biashara zao lilikuwa ni rafiki kwani wengi walitoa bila shida.Serikali itafute mbinu rafiki ya ukusanyaji mapato ambayo haitaleta madhara kwa jamii kwani watanzania sio wabishi kufanya jambo ambalo wameelewa faida yake.Pamoja na hayo,kulipa kodi ni wajibu wa kila mmoja kwani nchi bora hujengwa na ukusanyaji wa mapato kwenye Nyanja mbali mbali.

Sayansi na teknolojia:
Kwa mujibu wa tafiti za umoja wa Mataifa( UN), zinasema kuwa teknologia mpya Ina manufaa kama ikitumika ipasavyo,ripoti hiyo iliyofanywa na umoja wa Mataifa kupitia idara yake ya uchumi na masuala ya kijamii( DESA), ikiangazia masuala ya uchumi na kijamii ya dunia Nzima mwaka 2018 imegundua kuwa tayari teknologia za nishati salama na mifumo bora ya utunzaji nishati tayari, zinasaidia mazingira endelevu na kuzisaidia nchi kuziruka teknologia zilizopo kwa sasa pamoja na upatikanaji wa dawa. tunaishi katika wakati ambao kila siku vitu vinabadilika, sio kama zamani tulipokuwa tukiwasiliana kwa njia ya barua posta, sasa tuna simu za mkononi na kila siku zinabadilika na kuwa tofauti tofauti, Hivyo ili kuendana na wakati, inapaswa kuwa na wataalamu wa teknolojia ambao watatupa elimu ya jinsi ya kutumia vitu vipya, faida na hasara zake.Nchi ya kisasa itajengwa na utaalamu wa teknolojia.

Haki za binadamu:
Ni jambo ambalo linapaswa kuzingatia katika utoaji huduma yeyote, kila mtu anayo haki ya kupata Mahitaji muhimu kama, Chakula, Malazi na makazi, kila mtu ana haki ya kuishi. Kadri Maisha yanapobadilika na kufanya mwingiliano wa watu wenye tamaduni tofauti tofauti, vitu vingi vinaibuka kama mauaji ya kutisha ya binadamu kwa sababu za visasi, imani za kishirikina na hata udikteta wa baadhi ya viongozi katili au makundi ya waasi.Ili kupambana na jambo hili inapaswa kukemewa na adhabu kali iweze kutolewa pamoja na Elimu ya haki za binadamu.Nchi bora huundwa na watu wenye kupata haki zao za Msingi.Hivyo ili kuwe na mabadiliko chanya inapaswa kila sekta iweze kuwa imara na kuwe na mipango endelevu yenye kukabiliana na kila changamoto bila kutetereka.

MUNGU IBARIKI TANZANIA,
BARIKI NA KILA MMOJA AISHIYE NDANI YAKE AMEN.
 
Upvote 1
UNAWEZA KUFANYA HICHO UNACHOKITAMANI KIFANYIKE ILA FUMBIA MACHO HICHO UNACHOONA NI KIKWAZO KWAKO.
Watu wengi wamekuwa wakitamani kufanya vitu vikubwa na vizuri na pia huenda ni vipya lakini wanakata tamaa baada ya kutazama maumbile, umri, kabila, jinsia na hata hali ya kimaisha na mwisho huishia kutamka neno "MIMI SIWEZI LABDA NINGEKUWA HIVI AU NINGEKUWA VILE"
Waswahili walisema"uoga wako ndio umasikini wako"

Tambua kuwa vile ulivyo ndio style ya pekee na yenye kuvuta mtazamo mkubwa wa watu na kushangaa kuwa umewezaje. Mfano wewe ni mlemavu unatamani kuonyesha ulimwengu jinsi ambavyo unaweza kufanya kitu flani kama mtu mwingine mwenye viungo Sawa, mfano kula kwa kutumia mguu badala ya mkono, unaweza kuimba, unaweza kutunga vitabu, usiangalie watunzi wenzako vile Wana ukamilifu wa viungo, usitazame kuwa wenzako wengi wanafanya kazi unayoitamani kuwa ni jinsia tofauti na yako, usitazame kipaji ulichonacho eti kinafanywa na watu wenye umri tofauti na wako na ukaishia kusema "MIMI NIMEPITWA NA WAKATI NIACHIE VIJANA"
Kama ni jambo lisilo na limit ya Muda unatamani kufanya, Anza sasa,

Usijiulize utaanza vipi? anzia mahali ambapo unapaweza kufanya, usisubiri uwe na pesa nyingi, anza na kile ambacho unacho kwani Sio kila kitu kinahitaji Msingi wa pesa, kuna vingine unahitajika uthubutu wako tu mfano kama una kipaji cha kuimba rekodi clip fupi tuma mtandaoni, ni hatua mojawapo ya kuanza safari ya mziki huwezi jua clip ile italeta matokeo gani, kuna watu wengi wamepata udhamini kupitia clip zao ambazo walizirusha kama utani na sasa wamesajiliwa kwenye magroup makubwa mfano msanii Angela ambaye amesajiliwa Kondegang.

Kumekuwa na mifano Hai ya watu ambao walifukuza mawazo ya kushindwa vichwani mwao na kukaribisha Neno NAWEZA, jinsi walivyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kuliko hata hao waliojulikana kuwa ndio wenye sifa kwa mfano zamani hakukuwa na waimbaji watoto wadogo,wazazi wengi waliona kuwa Sanaa ni uhuni, Hivyo watoto waliishia kusoma masomo ambayo walilazimishiwa na wazazi, na watoto walisoma ili tu kuwaridhisha Ila vichwani waliwaza kucheza mpira, kuimba kuwa wanamitindo, n. K

Kitu hiki kimefanya familia nyingi kuwa na migogoro kati ya wazazi na watoto wakibaki kulaumiana, mzazi akijutia kupoteza pesa kumsomesha mwanaye awe daktari lakini badala yake akaishia kukimbia riadha, kuimba, n.k.

Nchi zilizoendelea wameweka kipaumbele vipaji vya watoto zaidi kuliko kusoma ili waajiriwe na ndio maana bado kiuchumi wanatuacha mbali sana, watoto wa kichina tangu wadogo wanafundishwa vitu ambavyo inaonekana wanapenda na kuviweza na bidhaa nyingi ambazo watoto wetu wanachezea zinatengenezwa na watoto wa kichina katika kujifunza kutengeneza ndege, magari n.k,watoto wetu wanaletewa kucheza na kikiharibika hawawezi hata kurudishiwa vile kilikuwa.Nchi yetu tumeonekana kama ni dampo la kutupa bidhaa ambazo kule zilipotoka hazina Thamani.

Hii natamani ifikie mahali tuseme No, nasi tuwe na watu wenye kutengeneza vitu na kuuza nchi zingine.

Nchi yetu ya Tanzania haijawekea mkazo kuendeleza vipaji vya watoto wanasisitiza kusoma tu na Elimu yetu inategemea kuajiliwa, maelfu ya wasomi wanamaliza vyuo na kukosa kazi, baadaye baada ya Maisha kuwachapa mtaani, ndipo wanakumbuka kutumia vipaji ambavyo wanavyo na inakuwa ni too late kwani ni vipaji visivyo na uzoefu, wanaishia kushika nafasi za mwisho mwisho kwani Kuna watu wenye uzoefu wa muda mrefu. Ushauri wangu ni kuwa, kuwe na mtaala wa kusoma masomo na vipaji pia, ili kuwe na plan A na B katika Maisha ya wasomi wa kesho.

Tukirudi kwenye point yetu, tunaona jinsi ambavyo wazazi wengi kwa Hivi Karibuni wameanza kuthamini vipaji vya watoto wao,
Sie wote ni mashahidi kuwa siku hizi Maisha yamebadilika sana Sio kama zamani ambapo hakukuwa na comedian watoto wadogo, hakukuwa na wasanii wa kike wenye watoto hata kama walikuwa nao, ila ilikuwa ni siri kubwa maana ingeonekana hana sifa za kuwa msanii hasa wa kuimba, ila nyie wenyewe ni mashuhuda wa kipindi cha Hivi Karibuni Kumekuwa na wimbi la wasanii wengi tena wenye majina makubwa kupata ujauzito na kuzaa watoto, mimba kwa wasanii wa sasa Sio siri tena ni jambo la kujivunia kuitwa Mama,japo Roseney nawapa ushauri kuzaa ndani ya ndoa, kwani pamoja na kusema kuwa kufanya Sanaa na Maisha ya kawaida inafaa yaendelee Ila inafaa tuangalie na kile ambacho tunafanya je tupo sahihi?

Natamani kuona kukiwa na mapinduzi makubwa ya fikra kuhusu kufanya jambo lolote wakati wowote bila kuwa na vikwazo, mfano mtu yoyote aliyeoa au kuolewa, aliyezaa au aliye na umri wowote kuonyesha kipaji chake bila shida, pamoja na watu wengi sasa Hivi kuwa na watoto huku wakiendelea na vipaji vyao bado suala la kuoa au kuolewa halijawekwa wazi, ni rahisi mtu kuonyesha jamii kuwa ana mtoto na si kuonyesha yule aliyezaa naye mtoto, au ni rahisi kuvalishana Pete ya uchumba kuliko kuvalishana Pete ya ndoa, Kwanini naongelea mambo haya, ni kwa sababu natamani tufikie mahali tuweze kufanya jambo lolote, wakati wowote bila kipingamizi chochote Yaani namaanisha mtu mwenye kipaji chochote aweze kukionyesha bila kujali, amezaa, ameoa au kuolewa, ana ulemavu, umri ni mdogo wala mkubwa.

Wasanii wengi Hivi Karibuni wamejifunza kwa Zari the boss lady ambaye ni X na mzazi mwenzake na msanii Diamond Platinum baada ya kutangazia Uma kuwa ana watoto wakubwa na bado ni mrembo, mwenye pesa na anayeheshimika mahali popote.

Mama Huyu licha ya umri wake na hata umri na idadi ya watoto watano alionao lakini ukimwangalia ni kama hana hata mtoto mmoja, bado ni mrembo na mchakarikaji, wasichana na wamama wengi wamejiamini kuwa licha ya kuzaa bado wanaweza timiza ndoto zao. Hivyo
Mfano huu unaonyesha dhahiri kuwa hicho Unachoona ni KIKWAZO wenzio wanajiamini na kufanya vitu vikubwa na jamii inawapa Heshima kwa sababu tu ya kujiamini. Kuna mifano mingi sana mtaani kwetu ambao hata wewe utakuwa na rafiki zako ambao wanajiamini lakini watu wengine wanawabeza kwa mionekano yao lakini hawajali na kila siku tunaona mafanikio yao.

Kuna wasanii na viongozi wakubwa duniani wenye ulemavu wa viungo, ulemavu wa ngozi,kuna wazee wenye pesa ambazo zimetokana na kufanya vitu mbalimbali na kupata mafanikio makubwa mpaka yakaishangaza dunia na jamii inayoizunguka.
Kitu kikubwa ninachokiongelea hapa ni Kujiamini, kuthubutu kufanya kile unachokiamini unakiweza bila kuangalia watu wanakuonaje, ili mradi kisivunje sheria za nchi na za dini.
Siongelei tu katika vipaji Ila kama Kuna wasomi wenye ndoto kubwa za urubani, udaktari bingwa na hata uongozi ngazi za juu bado inawezekana, jiamini thubutu usijione hufai kuendesha ndege kwa sababu ya ulemavu wala usione huwezi kuwa Rais kwa sababu ni mwanamke, fikra hizo futa kwani zimepitwa na wakati.

Watu wengi wanakwama katika uthubutu, mfano anaogopa kuanza biashara akiogopa kupata hasara, anaogopa kukopa akiogopa kufungwa pale akishindwa kulipa, anaogopa kuingia kwenye Mahusiano akiogopa kusalitiwa, Ondoa mawazo hasi kichwani yatakufanya ufe maskini, kila jambo linachangamoto lakini haimaanishi tuzikimbie
Nina imani baada tu ya kumaliza kusoma Maneno haya utajitathmini kufanya kile ambacho kimekuwa ni ndoto ya Maisha yako,bila kujali nani anasema nini, ukiamua kuanza safari usitazame mbwa wanaokubwekea utaghairi unapokwenda.

NAKUTAKIA SAFARI NJEMA KUELEKEA NDOTO ZAKO.
 
Back
Top Bottom