promisegeofrey2012
New Member
- May 31, 2024
- 2
- 0
Suala la ajira hapa nchini, limekuwa moja ya agenda kuu na ngumu kutekelezeka tangu kupatikana kwa uhuru,hali iliyopelekea kila awamu ya utawala katika nchi yatu tangu awamu ya kwanza hadi awamu ya tano.
Katika awamu zote za utawala kumekuwa na mikakati pamoja agenda, sera na taratibu mbalimbali zinazoanzishwa kwa ajili ya kusimamia masuala ya ajira kwa wafanyakazi wa umma pamoja na sekta binafsi. Wafanyakazi katika sekta za umma na binafsi wamekuwa wakikumbana na matatizo mbalimbali ya kisera, kikanuni, kisheria na kiutawala katika maeneo mbalimbali, idara na sehemu wanakofanyia kazi.
Malalamiko juu ya mazingira magumu ya kazi, miundombinu, maslahi ya wafanya kazi, ushirikishwaji katika maamuzi ya kuamua maslahi ya wafanya kazi yamekuwa ni kawaida katika sekta za umma na binafsi. Kote huko hakuna mtu au taasisi iliyofanikiwa kuwatetea na kuwakomboa wafanyakazi licha ya taasisi hizo na watu hao kutoa kauli, matamko na machapisho mbalimbali kuhusiana na namna uboreshwaji wa masuala ya wafanyakazi yanavyopaswa kuwa.
Serikali inapaswa kuandaa sera na sheria rafiki kwa wafanyakazi zitakazoleta tija kwao, wale walio serikalini na hata mashirikia au sekta binafsi.
Serikali na taasisi binafsi zinatakiwa kuandaa mipango ya muda mfupi na mrefu inayotaja malengo ya taasisi na hata kuonyesha namna mipango hiyo itakavyotekelezaka bila kuathiri ustawi wa taasisi na wafanyakazi.
Mazingira ya kazi yanapaswa kuwa rafiki sio tu kwa mwajiri bali pia kwa mwajiriwa, ili kumwongezea hari na morali katika utendaji kazi wa kila siku.
Masilahi ya wafanyakazi pia ni sehemu muhimu inayopaswa kutazamwa na serikali ambapo sera zake hasa katika upangali wa viwango vya mishahara kuanzia kima cha chini mpaka cha juu unakuwa wa kuleta unafuu wa kipato kwa wafanyakazi wote wa serikali na binafsi.
Serikali inapaswa kujua kwamba mfanyakazi ana mzigo mkubwa ambapo serikali, yeye binafsi na ndugu jamaa na marafiki kwa pamoja wanamtegemea yeye katika kurahisisha ugumu wa maisha, hasa katika suala zima la kiuchumi.
Suala la ajira kwa upande wa serikali linapaswa kuwa kipaumbele hasa kwa vijana, na linapaswa kuwa kwenye mipango ya muda mrefu, na sio kulifanya suala hilo kuwa la kimkakati, sana sana pale masuala ya uchaguzi yanapokaribia.
Suala la ajira ni suala linalopaswa kuratibiwa kwa umakini, kwani ni suala linaloamua mustakabali wa taifa na maisha ya kila siku ya mtanzania.
Suala la ajira halipaswi kutumika kama zawadi kwa wananchi, bali suala la kisera,kisheria na kikanuni ili kudhibiti mianya ya upendeleo, undugu na rushwa katika masuala ya utendaji kazi hali itakayofanya wafanyakazi wanaishi bila mashaka na kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na uzalendo.
Masuala ya urasili mali watu yanapaswa kupewa watu wenye weledi, upendo, hekima, uzalendo na uadilifu ili kufanya masuala ya kazi na ajira kuleta tija kwa mwajiri pamoja na mwajiriwa.
Suala la ajira lisiwe la kisiasa bali la kisera jambo ambalo litarahisha utendaji kazi wa mfanyakazi, kumpa furaha kazini na kumfanya aipende kazi yake.
Serikali inapaswa kuangalia namna ambavyo inaweza kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kada zote, hasa katika suala la mishahara, marupurupu, pamoja na matakwa mengine ya wafanyakazi, ili waweze kustawi kimaisha wakiwa bado kazini na sio kusubiri mafao yao ndipo waweze kufanikiwa.
Serikali ihakikishe mazingira ya kazi, sera, sheria na taratibu za kuajiri pamoja na kanuni za kazi zinakuwa rafiki, na za kufikika kwa pande zote mbili yani mwajiri na mwajiriwa.
Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa mchakato wa kupata waajiriwa wapya unakuwa wa wazi na ushindani unapimwa kwa mizani sawa baina ya wanaoomba nafasi mbalimbali za kazi serikalini na kusimamia michakato hiyo pia kwa upande wa sekta binafsi.
Iundwe sheria inayolazimisha hata wale wafanyakazi wa kujitolea (INTERNS)kupata stahiki mbalimbali ikiwemo nauli na pesa kidogo za kujikimu kwa ajili ya kuwafanya wawe na hamu ya kuzidi kuitumikia serikali kwa ustawi wa sasa kesho na karne zijazo.
MIPANGO YA AJIRA KWA DIRA YA MAENDELEO YA MUDA MFUPI (MIAKA 5)
Kuwepo kwa sera mbadala ya ajira itakayowezesha kufikika kwa malengo ya muda mfupi kuanzia miaka mitano. Ili kufanikisha hilo hakuna budi kuajiriwa vijana kwa kupewa mikataba ya ajira ambayo ambapo waajiriwa watapimwa kwa malengo ya mwaka mmoja mmoja,ili kuwa kama sababu ya kupewa mkataba mwingine endapo utendaji wake ulileta tija.
MIPANGO YA AJIRA KWA DIRA YA MAENDELEO YA MIAKA 10 -20
Kuwepo kwa sera inayolenga maendeleo ya miaka kumi hadi ishirini, waajiriwe wafanyakazi wenye taaluma na weledi wenye umri rafiki na kiu ya maendeleo ambayo itawasukuma kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na uadilifu, bila kusahau kuwapa stahiki za mishahara na marupurupu kwa ajili ya kuwafanya wawe watedaji bora.
AJIRA ZA KUDUMU ZIZINGATIE WALE WALIOJITOLEA NA WALIOTOKA KATIKA MIKATABA YA AJIRA YA MUDA MFUPI NA MUDA MREFU.
Ili kupunguza gharama za mafunzo kwa watendaji wapya kila mara, pamoja na kupunguza gharama nyingi zinazotumika katika kuandaa mambo ya usaili ambayo hutumia gharama, na muda mwingi, waajiriwa wapya watoke ndani ya taasisi walizokuwa wakifanya kazi ya kujitolea, kwani tayari wanakuwa na uzoefu wa kazi. Hali hii italeta utendaji wenye tija kwa waajiri pamoja na waajiriwa.
Naitwa Geofrey Ephata Mollel, 0755173096,0655506609.promisegeofrey03@gmail.co

Upvote
2