Uongozi katika nchi yetu umegubikwa na wingi wa watendaji wa serikali ambao wanapelekea wingi wa matumizi ya pesa za serikali ambazo zingefaa kutumika katika sekta mbalimbali.
Andiko hili litaenda kugusia namna mabadiliko ya kiutawala katika ngazi ya vitongoji, vijiji, tarafa, wilaya mpaka mkoa yanavyoweza kubadili taswira na utendaji ambao utakuwa rahisi na utaoleta manufaa kwa wananchi na nchi yetu kwa ujumla wake.
Katika ngazi ya mikoa mpaka chini serikali za mitaa tunaona kuna wingi wa viongozi wakuchaguliwa na wananchi pamoja na wale wa kuteuliwa na serikali. Wanakua wakifanya kazi kwa kutegemeana na kushirikiana lakini ni wakati sasa wa kubadili mfumo huu wa kiutawala, kwani katika wilaya moja unakuta kuna mkuu wa wilaya, katibu tarafa, wabunge wa jimbo au majimbo, madiwani, wenyeviti wa vijiji. Hawa watu wote wapo kwa ajili ya kutekeleza sera za serikali pamoja na kusikiliza wananchi.
Lakini tunaona namna viongozi wa kuteuliwa wamekua na nguvu sana kuliko wale wa kuchaguliwa na wananchi ambao ndio walipaswa kuwa wakuu kuliko wale wa serikali kwani serikali ipo pale kutekeleza matakwa ya raia wake. Tunashuhudia wenyekiti wa vijiji wakishiriki ofisi na watendaji wa kata, wabunge wakitumia ofisi zilizopo kwa wakuu wa wilaya n.k.
Mfumo huu unapunguza uwajibikaji wa viongozi wa kuchaguliwa na wananchi na majukumu yote kusalia kwa viongozi wa kuteuliwa jambo ambalo sio sahihi kwani kunakosekana uongozi wa kuwajibisha serikali pale ambapo miradi haitekelezeki katika eneo husika.
Tutazame nchi jirani na nyingine nyingi zilizoendelea uongozi wa kuteuliwa unakua ukisimamiwa moja kwa moja na viongozi wa kuchaguliwa na wenye mamlaka ni viongozi wa kuchaguliwa zaidi ya wakuteuliwa. Mfano halisi ni Kenya na mfumo mpya wa kaunti badala ya mikoa na wilaya, kila kaunti ina bunge na gavana wa kaunti aliechaguliwa na wananchi anateua baraza la mawaziri wa kaunti na wanafanya kazi chini ya uangalizi wake gavana.
Hivi sasa nguvu ya utawala walio nayo wakuu wa mikoa na wilaya ni kubwa sana inayofanya watu wajisahau katika nyadhifa hizo na kwakuwa hakuna muangalizi wa moja kwa moja wa kuwasimamia inapelekea tunaona kila leo Mh Raisi akibadili wakuu wa mikoa na wilaya kila mara. Ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya ni chanzo kikubwa cha kupotea kwa mapato ya serikali, rushwa, na mambo mengi ya kufanania hayo.
Ubadilishwaji wa mfumo huu wa kiutawala utasaidia sana katika uratibu na kuleta uwajibikaji kwa wabunge wanaochaguliwa na wananchi kwani imekua ni kama wananchi wanachagua watu wakwenda kuwawakilisha bungeni na watakaa bungeni miaka mitano kisha watarudi tena kuomba nafasi ya kurudi bungeni bila kusimamia miradi yeyote katika majimbo yao au kusimamia kwa uchache na kukosekana kwa uwajibikaji kwani yeye hausiki moja kwa moja katika kuwasimamia wakuu wa mikoa na wilaya ambao ndio wasimamizi wa serikali katika ngazi hizo.
Mamlaka waliokabidhiwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya watendaji wa kata n.k ni kubwa sana kulinganisha na mamlaka alionayo mbunge, diwani na mwenyekiti wa kijiji jambo hili linapelekea kukosekana kwa ufanisi wa utendaji na uwajibikaji katika ofisi hizi.
Matumizi ya fedha katika ofisi hizi za viongozi wa kuteuliwa ni kubwa na kufanya kuongeza mzigo wa matumizi ya kawaida katika bajeti yetu ya nchi kwani kuna uhitaji wa kulipwa kwa viongozi na watumishi mbali mbali wanaofanya kazi katika ofisi za viongozi hawa wa kuteuliwa, ilihali wenyeviti wa vijiji/vitongoji utendaji wao na motisha zao ni hafifu licha ya kwamba wao ndio watu wa kwanza kukutana na wananchi na ndio watu wa kwanza kabisa wanaoweza kutambua changamoto zilizomo katika ngazi ya chini kabisa ya kiuongozi.
Hali hii inaondoa uwajibikaji wa viongozi hawa wa kuchaguliwa kupelekea utendaji mbovu na matumizi mabaya ya fedha za umma, hivyo ni dhahiri kabisa mabadiliko ya mfumo wa kiutawala yanahitajika na mamlaka ya viongozi wa kuchaguliwa itambulike na kuheshimiwa kwani hawa ndio wawakilishi wa wananchi.
Mabadiliko haya yatarudisha nguvu ya umma na utayari wa wananchi kushiriki kikamilifu katika mambo yanayohusu nchi yao ikiwemo upigaji wa kura, utoaji wa kodi halali, kudhibiti rushwa n.k kwani watakuwa na mtu wa moja kwa moja wanaomchagua ambae wanaweza kumwajibisha pale wasipoona maendeleo kwani mbunge huyu atakua na mamlaka ya kuteua watu wakumsaidia majukumu na atakua akiwasimamia tofauti na sasa wabunge hujificha katika kivuli cha kusema ni serikali haijatenda na kufanya wasiwe wawajibikaji kwani wanatambua fikra kuna wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wa serikali.
Kwa kuhitimisha uwajibikaji kwa ngazi hizi za mikoa na wilaya pamoja na serikali za mitaa utapelekea katika mafanikio na maendeleo bora ya wananchi na ukusanyaji wa mapato utakua salama zaidi kwani wananchi watakuwa washiriki wa moja kwa moja kwa kupitia viongozi waliowachagua.

Upvote
1