SoC04 Mabadiliko katika upatikanaji wa Spika wa Bunge na Mawaziri

SoC04 Mabadiliko katika upatikanaji wa Spika wa Bunge na Mawaziri

Tanzania Tuitakayo competition threads

Saidi malolo

Member
Joined
May 2, 2024
Posts
17
Reaction score
12
Spika wa Bunge asichaguliwe kutoka miongoni mwa Wabunge na pamoja na Mawaziri

Spika wa Bunge huyu ndie Kiongozi Mkuu wa Bunge, na mfumo uliopo sasa Spika wa Bunge na Naibu Spika wanatoka miongoni mwa Wabunge ndio anakuwa Spika. Tukumbuke kuwa Bunge ni sehemu muhimu kwasababu ndio sehemu ambapo maamuzi mengi yanafanyika hivyo basi ni vizuri kukawa na mfumo bora iwe hivi

Kuwepo na kipengele ambacho Spika wa Bunge achaguliwe watokee watu nje ya wabunge ambao watanadi sera zao ndio wagombee kama uchaguzi wengine unavyofanyika na sio lazima huyo mgombea awe na chama, hata mtu binafsi aruhusiwe kugombea. Kuhusu nani apige kura (hapo tunapanga kama nchi kati ya wananchi wote wapige kura au tunaweza kuamua wabunge ndio wapige kura kimoja wapo tutakiamua) baada ya kufanya kutafiti

Hii itamsaidia Spika kuwa huru kwa sababu hana kitu anachohofia kuliko hii ya sasa Mbunge kuwa Spika kuna baadhi ya maamuzi yanashindwa kufanyika kwa ufasaha na Spika anakuwa hana nguvu kwa viongozi wa Serikali

Kingine, Mawaziri nao vile vile wasiwe wabunge. Mawaziri wote wasiwe miongoni mwa wabunge, hii ili kupunguza upendeleo hawa wabunge wamechaguliwa kutoka majimboni kwao kwa ajiri ya kuwawakilisha wananchi unapompa uwaziri unakuwa umempunguzia ufanisi wa kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwa sababu wananchi wanakosa mtu wa kuwasemea shida zao

Hivyo katika mabadiliko Rais achukue watu wengine nje ya wabunge ndio wawe mawaziri ambao watakuwa hawana majimbo ndio awachukue kwa ajiri ya kuwa mawaziri na kumsaidia hizo kazi. Hii itasaidia kila jimbo kupata maendeleo sawa na kila jimbo litakuwa na mtu wa kuwasemea huko bungeni

Na kila mbunge atakuwa na wasaa mzuri wa kuihoji Serikali kuhusu vitu fulani na sio huyo ni mbunge na vile vile ni mtu wa serikali bungeni hii inapunguza ufanisi wa kazi.

Rais au Serikali inaweza kuandaa watu wake na kuwaalisha kisha wakaenda bungeni kufanya kazi za serikali. Hii itasaidia sana na hatimaye kupeleka kwenye nchi ya ahadi kwa hiyo Katiba ya nchi ifanyiwe mabadiliko ili tufikie nchi hiyo ya ahadi
 
Upvote 1
Hivyo katika mabadiliko Rais achukue watu wengine nje ya wabunge ndio wawe mawaziri ambao watakuwa hawana majimbo ndio awachukue kwa ajiri ya kuwa mawaziri na kumsaidia hizo kazi. Hii itasaidia kila jimbo kupata maendeleo sawa na kila jimbo litakuwa na mtu wa kuwasemea huko bungeni
Mwanzoni nilikuwaa sijakupata sasa nimeanza kuelewa. Ni kweli kuna mihimili ya Bunge, Utawala, na Mahakama. Tayari unapomchukua mbunge na kumpa cheo cha kiutawala unakuwa umeshagonganisha mihimili miwili 'somehow'🤔

itamsaidia Spika kuwa huru kwa sababu hana kitu anachohofia kuliko hii ya sasa Mbunge kuwa Spika kuna baadhi ya maamuzi yanashindwa kufanyika kwa ufasaha na Spika anakuwa hana nguvu kwa viongozi wa Serikali
Lakini kwa spika kuwa sehemu ya wabunge yenyewe haikatai maana ndo muhimili huohuo. Je? Hauoni kama unakuwa unataka meya asiwe miongoni mwa madiwani?
 
Back
Top Bottom