SoC04 Mabadiliko makubwa katika uchukuzi, teknolojia ya habari na mawasiliano 2030-2055 katika kuchangia pato la taifa

SoC04 Mabadiliko makubwa katika uchukuzi, teknolojia ya habari na mawasiliano 2030-2055 katika kuchangia pato la taifa

Tanzania Tuitakayo competition threads

kaponder

New Member
Joined
Apr 29, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Uchukuzi na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ni muhimu Sana kwa usatawi wa nchi ya Tanzania kwa kuchangia Pato la Taifa. Uchukuzi hujumuisha bahari(bandari), usafirishaji wa anga, barabara na reli. TEHAMA hujumuisha matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano ikiwemo mitandao ya simu, mitandao ya kijamii, shughuli za serikali mtandao na matumizi ya vifaa vingine vya mawasiliano. Sekta hii ni nyeti Sana kwasababu imebeba shughuli nyingi za kiuchumi na kimkakati ambazo zinaweza kuwa chachu kubwa ya kukua kwa uchumi na Pato la Taifa la Tanzania.

Yafuatayo ni maboresho ambayo yakifanyika kati ya miaka ya 2030-2055 kutakuwa na mabadiliko makubwa Sana ya kiuchumi kupitia sekta hii:

Kuongezwa kwa reli za treni za umeme na treni za umeme zenye kasi zaidi; kutengenezwe reli za Standard Gauge Railway (SGR) kukutoka Morogoro kuelekea Zambia na Malawi. kununuliwe treni za umeme zinazokimbia kwa mwendo wa maili 250 kwa saa moja(250m/h). kuwepo kwa miundombinu hii wezeshi na iliyokuwepo itawezesha kukusanya mapato zaidi katika sekta ya uchukuzi hasa kuteka soko la usafirishaji katika nchi za Malawi na Zambia ambazo zinategemea bandari kuu ya Dar es salaam. Pia ongezeko la treni hizo itapelekea shughuli za usafirishaji kuongezeka na kuokoa muda na rasilimali na kuongeza pato la Taifa na fedha za kigeni katika nchi nyingine zitakazofikiwa na SGR ikiwemo Rwanda, Burundi na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maboresho makubwa katika sekta ya usafirishaji wa anga; hii ikiwa ni pamoja na kuweka mfumo bora wa utendaji wa shirika la usafirishaji wa anga ili kuongeza ufanisi na kuvutia wawekezaji na wateja WA kutumia ndege zetu. Kufanya ukarabati mkubwa wa viwanja vya ndege vya kisasa na vikubwa Ili kuruhusu ndege nyingi kutuma na kwa wakati mmoja. kuongeza idadi ya viwanja vya ndege vya kimataifa na pia kuongeza idadi ya ndege kubwa kama Airbus A380 na boeng 787 dreamliner za abiria na za mizigo zinazofanya safari za kimataifa kufikia nchi nyingi ili kupanua soko la matumizi ya ndege za Tanzania.

Maboresho ya huduma za serikali mtandao; kuwekwe mikakati kuanzia 2030 Kila huduma ya serikali iwe inapatikana mtandaoni hii ni kurahisisha mawasiliano pia kupoteza muda na fedha katika kutafuta huduma. Kufanyike semina na elimu kwa Jamii kuhusu matumizi sahihi ya mtandao na namna ya kupata huduma kwa njia ya mtandao kupata huduma kama maji, umeme, afya, elimu na shughuli nyingine za kiserikali. Pia kwa njia hii itasaidia kupunguza upotevu wa mapato ambayo yatakuwa yanakusanywa na mifumo ya serikali.

Kuwekeza katika elimu na vumbuzi mbalimbali za kitehama na uchukuzi. Uwekezaji mkubwa ufanyike katika taasisi za elimu kusaidia vumbuzi na bunifu mbalimbali zinazohusu TEHAMA. Hii ni muhimu kwasababu husababisha MAGEUZI makubwa ndani na nje ya nchi pia hii husaidia kufanya marekebisho na mabadiliko katika mifumo mbalimbali ya mawasiliano na kuongeza ufanisi katika utendaji.

Kuruhusu uwekezaji wa katika sekta ya TEHAMA na Uchukuzi; serikali ikaribishe wawekezaji zaidi kutoka ndani na nje ya nchi mfano makampuni kama Star link, Amazon, Google na Apple. Hii itasaidia kuongeza ajira, pato la Taifa pia itasaidia kupata teknolojia mpya za TEHAMA. Ziwekwe sheria zinazolinda maslai mapana ya nchi ikiwemo ulipaji Kodi, usalama wa nchi na ulinzi wa taarifa binafsi.

Kuboresha na kuongeza miundombinu ya barabara; barabara zote zinazounganisha mikoa, wilaya na mipaka zitengenezwe kwa kiwango Cha lami ili kuruhusu shughuli kubwa za usafirishaji na hii itasaidia kukua kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi kama biashara na viwanda. Pia shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii hufikiwa zaidi na miundombinu ya barabara ikiwemo viwanda, biashara, shule, huduma za afya na pia mipaka ya kimataifa.

Kuwekeza zaidi katika teknolojia ya akili mnemba na matumizi sahihi ya taarifa binafsi kwa manufaa ya kiuchumi; akili mnemba huweza kusaidia katika maeneo ya viwanda, elimu, afya, biashara, huduma za kifedha. Matumizi ya akili mnemba huongeza ufanisi, uzalishaji na pia huchangia ongezeko la pato la Taifa. Taarifa binafsi huweza kutumiwa na serikali vizuri katika kudhibiti uhalifu katika Jamii na pia kuweza kuangalia namna Bora ya serikali kuboresha, kutoa au kuongeza huduma mbalimbali kulingana na mahitaji.

Kuboresha miundombinu ya bandari na huduma za uchukuzi kupitia bahari ya hindi; usafirishaji kwa njia ya bahari ni muhimu kwasababu hupokea mizigo mingi kwa wakati mmoja. Kwa upande wa Tanzania hutegemewa na nchi nyingi za jirani katika kusafirisha na kupokea mizigo kupitia bandari yetu ya Dar es salaam na nchi hizo ni pamoja na Uganda, Rwanda, Burundi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC), Zambia na Malawi. Kuwepo kwa miundombinu bora na ya kisasa ya TEHAMA katika kurahisisha utoaji wa huduma. Pia bandari iwe karibu na miundombinu mingine ya treni ya kisasa ya umeme (SGR), barabara za kiwango bora na viwanja vya ndege.

Kwa mapendekezo hayo, Tanzania inaweza kukua kwa kasi Sana kiuchumi kwasababu miundombinu bora ya uchukuzi na TEHAMA. Hii ikiwa na maana kwamba Kila kitu kwa dunia ya sasa hutegemea miundombinu ya kisasa ili kuwezesha utoaji wa huduma kwa wakati na yenye tija kwa watu wengi. Yakifanyika mapendekezo hayo hapo juu kwa miaka ya 2030-2055 tutaweza kuhamasisha wawekezaji, wadau mbalimbali na nchi jirani watatumia bandari yetu, ndege zetu, barabara yetu, treni yetu na hii itachangia kukua kwa kiasi kikukwa kwa uchumi wetu na kuajiri vijana wengi katika kazi mbalimbali.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom