SoC04 Mabadiliko ninayotamani kuona katika sekta ya elimu miaka 5-10 ijayo

SoC04 Mabadiliko ninayotamani kuona katika sekta ya elimu miaka 5-10 ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

true to oneself

New Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
1
Reaction score
2
Sekta ya Elimu nchini Tanzania ni miongoni mwa sekta muhimu ambapo watu wanapata maarifa na ujuzi unaowasaidia kuondoa ujinga, kuwa wasomi na watu wanaoleta mabadiliko Chanya nchini. Sekta hii inajumuisha shule za awali, shule za msingi, sekondari Pamoja na vyuo vikuu. Pia, elimu inajumuisha walimu, wanafunzi, serekali, sekta binafsi Pamoja na sera zote zinazohusika na utoaji au usimamazi wa elimu. Yafuatayo ni maelezo yanayoonesha Tanzania ninayoitamani miaka 5 hadi kumi ijayo.

Ni vyema kukawepo na utaratibu wa kila mwanafunzi wa shule ya msingi na sekondari (Ordinary Level) kusoma somo la kompyuta au Tehama. Hasa kwa shule za serekali, sababu shule hizo unakuta hazina hata komputa na somo halifundishwi. Na baadhi ya shule hufanya hili somo kuwa la kuchagua. Napendekeza liwe la lazima kusoma. Pale mwanafunzi atakapokua shule ya msingi na kidato cha kwanza hadi cha nne. Kwasababu teknolojia ya sasa inahitaji mtu awe na uelewa wa namna ya kutumia vifaa vya kielekroniki kama vile simu janja na kompyuta.

Mimi ni mhanga wa watu waliojua kutumia komputa nikiwa chuo kikuu. Ambapo ilinisumbua kidogo kwa mara ya kwanza sababu nilipaswa niwe nafanya kazi za nyumbani(assignment) huku najifunza kutumia kompyuta, ila kama ningekua nimejifunza tangu shule ya msingi au sekondari basi ningekua na uelewa zaidi. Sababu ninachosoma chuoni kina ulazima wa mimi kutumia kompyuta.

Hivyo basi, shule zote za kata au serekali Pamoja na za watu binafsi hasa kwa elimu ya msingi na sekondari kwa kidato cha kwanza hadi cha nne, utaratibu wa kusoma somo la komyuta au Tehama uwepo. Hata wanafunzi wakifahamu vitu vichache tu kama vile kutumia Microsoft word kwa ajili ya kuandikia, Power point kwa ajili ya kuwasilisha Mawazo au taarifa zao, na Microsoft Excel kwa ajili ya mahesabu. Ambapo, vyote hivi wataweza kuvifanya watakapokua wamejiajiri, wameajiriwa au watakaopokua wanasoma elimu ya chuo kikuu au cha kati.

Wanafunzi wasisome masomo yasiyo na lazima kulinganisha na kile wanachotamani kuwa baadae. Kama mtoto anatamani kuwa daktari ni vyema akasoma masomo yanayohusu udaktari tu na sio mengine kama historia ambayo hayatamsaidia sana kuwa daktari. Na hii itasaidia kupunguza miaka ya mtoto kuwa shuleni.

Kuwepo na somo juu ya nidhamu ya fedha kwa wanafunzi tangu wanapokua wadogo ili wakue wakijua kutumia fedha vizuri. Na hata pale watakapofanikiwa kupata mkopo vyuoni wawezee kutumia fedha walizozipata kwa nidhamu na watakapokuwa viongozi au wamiliki wa kampuni au mashirika mbalimbali wawezekuelewa.

Wanafunzi watakaochagua masomo ya sanaa wasibezwe au wasionekane kama hawana akili. Hivyo ninashauri hata wale watakaofaulu katika mtihani wa kidato cha sita kwa Daraja la kwanza kwa pointi 3-5 wapewe zawadi pia kama wanaosoma masomo ya Sayansi ambapo hupewa Ufadhili wa kusomeshwa bure. Mfano, Samia Scolarship.

Kwa Maisha ya sasa, Teknolojia inakua kwa kasi sana na mbadala wa aina mbalimbali kwa binadamu unatokea. Hasa tukiongelea mbadala wa akili kwa mfano kuna Akili Mnemba (Artificial Intelligence). Wanafunzi wengi hasa wa vyuoni, kwa sasa hawatumii akili zao kufikiri au kusoma vitabu mbalimbali au kusoma mtandaoni bali wanatumia Akili Mnemba kufanya kazi zao za nyumbani. Hivyo ni vyema kukawepo na namna mpya ya kugundua wizi huo huko vyuoni. Na pia wanafunzi wafundishwe namna na matumizi bora ya Akili Mnemba. Ili kuepusha kuwepo kwa kizazi cha watu wasiofikiri.

Miundombinu katika shule za vijijini bado haijakaa sawa. Hivyo ni vyema serekali ikatengeneza miundombinu hiyo. Kama kuongeza madawati, meza za walimu. Vitabu na walimu waongezwe. Mfano shule iliyopo mkoani Kilimanjaro Kata ya Oldi Moshi Mashariki inayoitwa shule ya Msingi Kidia.

Haina walimu wa kutosha, na wanafunzi wanabanana kwenye madawati. Licha ya hiyo kuwa shule ya msingi kuna chuo kikuu cha Dar es Salaam, Shule kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano Kwa Umma (SJMC) kuwa na madarasa madogo na machache ya kufundishia.

Hivyo kusababisha wanafunzi wengine kusimama nje au Kwenda Ndaki nyingine mfano CoICT (Ndaki ya Habari, na Teknolojia ya Mawasiliano) kusoma kwasababu tu kuna sehemu kubwa ya kusomea. Hivyo ni vyema wakajenga madarasa megine makubwa kuwatosha wanafunzi wengi na viti au meza za kukalia wakati wa kusoma ziongezwe.

Ni vyema mbinu na namna za kufundishia zikaboreshwa hasa katika shule za sekondari na msingi. Sababu bado waalimu wanatumia chaki kufundishia ambapo chaki zina madhara katika afya zao. Mfano katika mfumo wa kupumua hasa kwa wale wenye pumu, kuathiri macho na Ngozi hasa kwa vumbi linalotoka baada ya kufuta chaki. Na pia ni uchafuzi wa hali ya hewa sababu ya vumbi na mwalimu au wanafunzi wanaweza kuchafuka pia kwa vumbi hilo linalotengenezwa na chaki. Kuna vitu vingine kama Makapeni au Projekta ambavyo vinaweza kutumika kuwafundishia wanafunzi.

Serekali ya sasa inasisitiza katika elimu ya vitendo wakati shuleni wanafunzi hawasomi kwa vitendo jinsi ipasavyo, na hii ni kwasababu wa ukosefu wa vifaa vya kutosha au maeneo ya kufuundishia elimu ya vitendo. Elimu ya vitendo ni muhimu kwasababu inasababisha wanafunzi kuwa na ujuzi na uzoefu na kupelekea kuamua kutataka kujiajiri wao wenyewe. Hivyo bnasi, ni vyema vifaa vya kujifunzia elimu kwa vitendo vikawepo kwa shule ambazo havipo au vikaongezwa kwa shgule ambazo vipo pungufu.

Wanafunzi wafundishwe kuhusiana na afya ya akili kwasababu kadri siku zinavyoendelea ndivyo watu wanaugua afya ya akili hasa vijana. Mfano mwaka juzi 2022, mwezi Oktoba tarehe 10 katika Kongamano la kwanza la Afya ya Akili yaliyofanyika katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya nchini Tanzania alisema kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa takribani milioni 7 wa afya ya akili na miongoni mwao zaidi ya wagonjwa milioni 1.5 wanaishi na sonona.

Hivyo basi, ni vyema mabadiliko haya yakafanyika sababu ssekta ya elimu ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania mfano elimu ni chanzo cha kupingana na maadui walitajwa na Rais wa kiwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mfano adui maradhi anaweza kupingwa kwa kufuata namna bora za kujikinga na kuepuka maradhi ambapo elimu hii huwa inapatikana katika somo la Bayolojia, Adui ujinga anaweza kupingwa kwa taarifa na adui maskini anaweza kupigwa na elimu kwa kusoma, kufaulu kwa vitendo na kwa elimu ya darasani kisha kujiajiri au kuajiriwa.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom