Mwesiga frolian
Member
- May 9, 2023
- 18
- 14
UTANGULIZI
Sheria ya ndoa Sura ya 29 ya mwaka 1971 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019 ni sheria kuu inayosimamia masuala ya ndoa nchini Tanzania. Sheria hii inakabiliwa na mapungufu mengi na changamoto nyingi miongoni mwa hizo changamoto ni pamoja na utata wa kimajukumu kati ya mme na mke katika ndoa, ugawaji wa mali za ndoa wakati wa talaka hasa katika ndoa za mitaala, ubaguzi kati ya mvulana na msichana katika umri au uwezo wa kuingia katika ndoa. Changamoto hizi zinaleta mkanganyiko wa kutafsiri na kusimamia masuala yanayohusu sheria ya ndoa nchini Tanzania.
Serikali inatakiwa kufanya maboresho na mageuzi makubwa katika sheria ya ndoa ili kuendana na mabadiliko na kasi ya maendeleo ya taifa kwa kuondoa mapungufu yaliyopo kama ambavyo nimeeleza katika jukwaa hili kupitia andiko hili kama ifuatavyo;
Maboresho ya sheria katika suala la uwajibikaji wa kimajukumu kati ya mme na mke ndani ya ndoa katika kuhudumia ndoa;
Kifungu cha 63 cha sheria ya ndoa kinaeleza kwamba mme ana wajibu wa kuhudumia familia kwa kumpatia mke wake mahitaji yote muhimu katika ndoa kama vile mavazi, chakula, na malazi, na mwanamke ana jukumu hilo tu ikiwa mme wake atashindwa kutunza familia kwa sababu ya ugonjwa wa akili na ulemavu.
Kifungu hiki kinastahili kufanyiwa maboresho kwani ni kifungu baguzi hasa kwa wanaume ukizingatia dunia ya sasa inaelekea kwenye usawa wa kijinsia, pia kifungu hiki kinahamasisha unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake, utegemezi wa kiuchumi kwa wanawake. Ili kuepukana na haya sheria inatakiwa kuweka wazi uwepo wa fursa sawa za majukumu kati ya mme na mke ndani ya ndoa.
Sheria inaruhusu ndoa za utotoni; Kifungu cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa vinachochea uwepo wa ndoa za utotoni nchini Tanzania kwa kuruhusu mtoto wa kike kuolewa kuolewa akiwa na umri wa miaka 15. Mahakama ya Rufani katika kesi ya Loveness Mudzuru na wengine dhidi ya Waziri wa sheria na wengine ya mwaka 2015 mahakama ilisema kwamba ndoa za utotoni zinasababisha wasichana kutotimiza ndoto zao hasa za kielimu, hivyo serikali haina budi kufanya marekebisho ya haraka ya sheria hiyo ili kuwanusuru watoto wa kike wasipoteze haki yao ikiwemo haki ya kuendelezwa ambayo kwa mjibu wa sera ya maendeleo ya mtoto Tanzania, maendeleo hayo yanahusu mtoto kubwa na kiwango kinachokidhi makuzi ya mwili, kiakili, kiroho .
(Chanzo: jamii forums)
Sheria ya ndoa inapingana na sheria nyingine katika kufafanua tafsiri ya mtoto;
Sheria ya ndoa inahitajika kufanyiwa maboresho ya haraka kwa kuondoa ukinzani uliopo dhidi ya sheria nyingine katika kufanya tafsiri ya mtoto hususani sheria ya mtoto ya mwaka 2009 ambayo inamwelezea mtoto kama mtu mwenye umri chini ya miaka 18. Katika mahakama ya rufani katika kesi ya Rebeca Gyumi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya mwaka 2016 mahakama ilitoa amri ya kwamba kifungu cha 13 na 17 cha sheria ya ndoa kinakinzana na katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 hivyo inatakiwa kufanyiwa marekebisho.
Maboresho katika suala la ugawaji wa mali za ndoa wakati wa talaka hasa katika ndoa za mitaala; Kifungu cha 9(3) na 10(1)(b) cha sheria ya ndoa kinatambua uwepo wa ndoa za mitaala nchini Tanzania. Sheria ya ndoa haijaweka wazi na kina mapungufu ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho au maboresho kwani hakijaweka wazi usawa linapokuja suala la ugawaji mali ya ndoa wakati wa talaka au urithi kwa kuzingatia kifungu cha 114 cha sheria ya ndoa. Suala hili linatakiwa kufanyiwa maboresho kwa kuweka wazi jinsi yaugawaji wa mali za ndoa katika ndoa za mitaala pale talaka inayotolewa .
( Chanzo: https://wildaftanzania. Or.tz.)
Sheria haitoi ulinzi kwa watoto walioko nje ya mfumo wa elimu;
Katika jamii zetu kuna utamaduni kwamba mtoto wa kike ambaye yupo nje ya mfumo wa elimu hulazimishwa kuozeshwa kwa kisingizio kwamba analindwa ili asiweze kupata mimba kipindi yupo nyumbani. Hivyo basi serikali inapaswa kupitisha mikakati ya kukabiliana na changamoto hizi kwa kuweza kutunga sheria inayowatambua watoto wa kike waliopo nje ya mfumo wa elimu.
Sheria ipo kimya kuhusu adhabu ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia;Kifungu cha 66 cha sheria ya ndoa kinakataza suala la unyanyasaji wa kijinsia kwa kutoa adhabu kwa mwenza wawapo kwenye ndoa ila hakijabainisha wazi au hakitoi adhabu kwa mtu atakayekiuka kifungu hiki kwa kufanya unyanyasaji wa kijinsia jambo ambalo linazidi kuchochea vitendo hivi kuzidi kushamiri kwa kasi katika jamii yetu. Hivyo katika kufanya maboresho ya sheria kifungu hiki hakina budi kupitia upya kwa ajili ya kuzuia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
(Chanzo: jamii forums.go.tz)
HITIMISHO
Jitihada mahususi zinatakiwa kufanyika kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, jamii, viongozi wa dini pamoja na serikali kwa ujumla kwa kutoa ushirikiano katika kupambana, kukemea na kutokomeza vitendo ambavyo vinachochea ukiukwaji wa sheria kama vile ndoto za utotoni, unyanyasaji.nk. Serikali haina budi kufanya jitihada ya haraka katika kufanya marekebisho na maboresho ya sheria ya ndoa kwa kupitia upya sehemu zenye mapungufu kwa kuchukua hatua za kuvifuta vifungu ili kuendana na kasi ya maendeleo nchini.
Frolian mwesiga Matungwa -lawyer. 0623435098

Upvote
7