SoC04 Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania kwa Kuongeza Uwajibikaji, Utawala wa Haki na Sheria, na Utekelezaji wa Shughuli za Serikali

Tanzania Tuitakayo competition threads

popoG

New Member
Joined
Mar 11, 2024
Posts
2
Reaction score
5
Kwanza kabisa ili kuifikia Tanzania tu itakayo Tanzania yenye mafanikio kiuchumi, kisiasa na kijamii tunatakiwa kuangalia namna ya mawazo, au vile tunavyopanga vinaweza kutimizwa. Tunapaswa kuzingatia

  • Mchakato rafiki wa kuwapata wasimamizi bora wa mipango na rasilimali za watanzania
  • Nguvu na mamlaka yanayopaswa kuwekwa kwa msimamizi na mtekelezaji wa mipango yote ya watanzania.
  • Namna ya kudhibiti nguvu na mamlaka wanayokua nayo viongozi wa serikali.
  • Mgawanyo dhabiti wa mihimili ya serikali katika kutekeleza majukumu ya kila mhimili.
  • Uwajibishwaji binafsi wa watendaji wa kuu wa kiserikali watakao tumia vibaya madalaka watakayo pewa.
Kwa muktadha huo napenda kusema kwamba

Ni muhimu kuwa na katiba inayo toa mwelekeo sahihi kuhusu maswala tajwa hapo juu

Kwanza kwa kuanza na swala la katiba inayotoa mchakato bora wa upatikanaji wa viongozi wa serikali na wawakilishi wa wananchi bungeni na katika serikali za mitaa. Michakato ya kuwapata viongozi hao inasimamiwa na tume ya uchaguzi ya tanzania, iliyopewa nguvu na ibala ya 74 ya katiba lakini mchakato wa uuudaji wa tume hiyo umekua kitendawili aambacho wanasiasa wengi wamekua wakikililia.

Kwa misingi hiyo ni vyema tukaangalia katika michakato lalamikiwa ya uundaji wa tume namna tume husika yafanya kazi,

Nitajizuia kusema baaadhi ya mambo ili kuaendana na kizuizi cha idadi ya maneno pasi na kupoteza mantiki ya kile nataka kukueleza

  • Upatikanaji wa tume
  • Utendaji wa tume
  • Uwajibikaji wa tume na wajumbe wake
  • Mchakato wa kupinga matokeo ya uchaguzi pindi tume inapotangaza
Swala lingine ni nguvu au mamlaka inayowekwa kwa viongozi wateule wa kiserikali

Hapa nitaangazia kwa uchache sana hoja hii na nikiunganisha na hoja ya tatu kuhusu uthibiti wa nguvu/ mamlaka waliyo nayo viongozi wakuu wa kiserikali.

Kwa kuanza na swala la mamlaka walionayo viongozi wa serikali wakuu haswa Rais, Waziri mkuu na watendaji wao wakuu katika kutekeleza majukumu ya kiserikali na uthibiti wa mamlaka hayo.

Katika swala hili mwongozo mkuu ni katiba katika ibala ya 34, 35, 36 na 37 zinazungumzia kuhusu Rais na mamlaka zake na ibala 34 ibala ndogo ya 4 imempa rais mamlaka ya kukaimisha mamlaka aliyopewa yeye kwa watu wengine wenye madaraka katika serikali pia raisi anayo mamlaka ya kufuta au kuanzisha au kufuta madaraka yeyote katika utumishi ndani ya jamuhuri ya muungano ya tanzania hiii imeoneshwa katika ibala ya 36 na katika kutenda kwake kazi Rais halazimishwi kutenda au kuacha kutenda jambo lolote lile na mtu yoyote bali kwa kuzingatia katiba.

Mbali yote hayo pia Rais kapewa mmlaka ya kuteua watendaji wa mahakama kwa ushirikiano na tume ya uteuzi wa majaji kama ilivyo oneshw akatika ibala ya 109

lakini pia Rais anaonekana kuingilia mchakato wa uchaguzi kwa kupewa mamlaka chin ya ibala ya 74, imempa pia mamlaka Rais kuunda tume ya uchaguzi.

Ibala zote hizi na zingine nyingi zinaonesha namna Rais anamajukumu mkubwa sana na yote yanahitaji utekelezaji wake. Jambo linaloweza kuiingiza nchi katika matatizo endapo nchi haitapata kiongozi mwadilifu kwasababu kwa namna mamlaka hayo yamekua makubwa sana inaweza kutengeneza mianya ya kua na viongozi madikteta wala rushwa na mafisadi.

Na ikizingatiwa kwamba Rais anakinga ya kuto kushtakiwa kwa makosa yoyote jinai au madai atakayo kua ameyafanya kipindi cha uongozi wake hii ni kama inavyo oneshwa na ibala ya 46 ya katiba.

Hivyo kwakuzingatia maslai mapana ya nchi ni vema baadhi ya majukumu aliyo pewa Rais yakakupunguzwa na kuwekewa Mchakato mwingine rafiki wa kusimamia majukumu hayo mfano swala la kuteua watendaji wa mahakama na uundwaji wa tume ya uchaguzi.

Na kuachwa kua muhidhinishaji tu na mchakato mzima wa nyanja hizo muhim mahakama na tume za uchaguzi kukawa na mchakato mwingine unaoweza kusaidia kupata watu mahili na wawajiikaji na Rais kama mtekelezaji wa mambo ya serilkali akabaki kama mhidhinishaji tu.


" Uteuzi wa Katibu wa Bunge na Katiba dhaifu! "
Kielelezo ambatanishwa hapo chaonesha uliopo katika swala la uteuzi wa viongozi wa kuu wa nchi

Sio hivyo tu kunatakiwa kuwepo na sheria maalum itakayo kua inawajibisha viongozi hawa wa kiserikali kwa makosa ambayo watagundulika walifanya kwa nia ovu pindi walipokuwepo kwenye nyzfa zao za uongozi mfano shwal kama la rushwa na matumizi mabaya ya madalaka.

Swala hili litachagiza kukua kwa utawala wa haki na sheria na ukuu wa katiba ya jamuhuri ya muungano utazingatiwa. Kwakuto kuwepom kwa uwajibishwaji wa pekee kwa viongozi hawa kunawapa mwanya wa kutenda vyovyote waonavyo vyema kulingana ni miono yao binafsi.

Swala lingine ni uwepo wa mgawanyo dhabiti wa mihilili ya serikali katika utendaji wa kazi zake kwakuzingatia ukuu wa kila muhimili na namna unatenda kazi pasi na kuadhili check and balance principle.


Serikali yetu ina mihimili mitatu ambayo ni mahakama iliyoanzishwa chini ya sura ya tano ya katiba, serikali kuu sura ya pili ya katiba na bunge sura ya tatu na kila muhimili upo kwa misingi ya kuangalia namna mhimili mwingine unavyofanya kazi. Hivyo basi ni vyema dhana ya mihimili hiii kutengana ikatunzwa na kutimizwa tofauti na inavyo lalamikiwa sasa.

"My government respects separation of powers: Magufuli ". Kiungo hiki kitakuonesha taswira ya kuwepo kwa utata kuhusu ugawanyo wa madaraka ya mihimili ya serikali

  1. Serikali kazi na majukumu ya serikali yanaweza kurejewa mwanzoni mwa wasilisho hili pamoja na kuangalia sura ya pili ya katiba ya Tanzania.
  2. Bunge, ni chombo ambacho kimsingi kimepewa madalaka na wananchi kuwawakilisha katika kuweza kusimamia serikali na utendaji wake ikiwa ni pamoja na kupitisha bajeti kuu ya serikali, kutunga sheria na kujadili maswala yote yaihusuyo Tanzania kwa niaba ya watanzania wote.
Endapo bunge likatimiza wajibu wake kama ilivyo katika katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ni hakika serikali yetu itawajibika ipasavyo.
3. Mahakama, hiki ni chomo kilicho na kazi ya kutoa haki kwa kutoa tafsiri ya sheria zilizotungwa na bunge, utendaji bora kazi wa mahakama ni nguzo katika kuifikia Tanzania ya tamanio.​
kwa sababu mahakama inanguvu ya kuzipa uhai sheria zote zinazotungwa na bunge kwa kutoa tafsiri dhahili na swala hilo lina akisi nini watekelezaji wa sheria husika (serikali) wanapaswa kufanya au kutekeleza.

Hivyo basi kwa kumalizia ni muhimu sana kabla ya kufanyika kwa jambo lolote lakini pasi na kua na msukumo wowote wa kisiasa. Tunapaswa kama nchi kutunga katiba mpya inayotoa mwongozo dhabiti wa utawala na utekelezwaji wa shughuli za kiutawala Tanzania kwa manufaa mapana ya Tanzania ya leo na vizazi vijavyo.

Mwisho pasi na umuhimu asante sana kuchukua mda wako wa thamani kusoma andiko hili. Pia karibu kuweza kuchangia lolote kulingana na kile nimewasilisha

Asante!!
 
Upvote 4
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…