Mabadiliko ya kweli Kamwe hayawezi kutokea ndani ya CCM.

Mabadiliko ya kweli Kamwe hayawezi kutokea ndani ya CCM.

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
Kuna kila dalili zinazonionyesha kwamba Mabadiliko ya kweli kamwe hayawezi kutokea ndani ya CCM, hata kama wangelishuka kutoka mbinguni akina Dr. Magufuli milioni moja wakasaidiana kuliongoza taifa hili chini ya mwavuli wa CCM, bado mabadiliko ya kweli hayatawezekana. Mabaliko ya kweli ya kifikra, kiuchumi na kisiasa kamwe hayawezi kutokea kabla hujaunda tume huru ya uchaguzi,upatikanaji wa katiba mpya pamoja na mihimili mitatu kutenda kazi kwa uhuru bila ya kuingiliwa na mhimili mwingine au mapendekezo ya mtu.

Tutapataje mabadiliko ikiwa mafisadi wote ambao wanamiliki 99% ya uchumi wa nchi kinyume cha sheria wapo ndani ya chama tawala? ikumbukwe kwamba wote hawa ndio waliofanikisha upatikanaji wa raisi.

Hii nchi ina wenyewe kama ambavyo CCM ilivyokuwa na wenyewe na hao wenyewe hasa ndiyo waliomuweka madarakani raisi Magufuli na wala siyo wananchi.

Wenye hati miliki na nchi hii hawafiki hata watu kumi ni watu kati ya 5 hadi 7 tu, lakini hawa ndiyo wanaomiliki na walioshikilia 99% ya utajiri wote na mamlaka ya kisiasa kwa 100% ya taifa hili; na watu hawa hasa ndiyo wenye mamlaka ya mwisho ya kuamua kwamba Rais wa Tanzania au Zanzibar awe nani au jimbo fulani nani awe mbunge au nani apewe Ujaji au Uprofessor au Ubalozi au Uwaziri na kadhalika. Huwezi kuubadili mfumo huu uliodumu kwa miaka 55 bila ya idhini ya vigogo hawa watano.

Ni vigumu kupata mabadiliko bila ya kuusambaratisha huo mtandao wa wakubwa mana wataweka watu wanaowapenda kuja kulinda maslahi yao na mali zao.
 
Ni vigumu genge la majizi, mafisadi, mala rushwa yakawa chachu ya mabadiliko kwa taifa, kusubili mabadiliko toka CCM ni sawa na kusubili au kutarajia mchicha toka ktk mmea haramu (CCM) aka bhange
 
Back
Top Bottom