Hakuna suala la kukwepa kodi katika hili kumbuka Celtel International imenunuliwa na Zain kwahiyo wameamua kutumia brand name yao kwenye operations zao zote afrika nzima.sasa wanakwepa kodi Uganda,Malawi,Congo na kila mahali walipokuwa na operations? Na ikumbukwe its very costly kubadilisha jina kwasababu inakubidi ufanya matangazo mengi kulifanya jina lijulikane kwa wateja wenu,kuweka billboards mpya,signboards,vipeperushi vipya na kadhalika nchi nzima.kufanya branding mpya kwenye magari na kila kona na mabango yote ya zamani kuyaondoa na kuweka mapya zoezi hili pengine lina gharama kubwa kuliko kodi wanayoikwepa kama kodi ndiyo lingekuwa tatizo. Mambo yaliyokuwa yanafanyika kwa sheraton-royal palm-movenpick ni tofauti na haya ya makampuni ya simu.Mobitel ilinunuliwa na kubadilishwa jina kwa hilo sasa n.k. Kwahiyo siyo kila mabadiliko ya majina yana lengo la kukwepa kodi lazima tufahamu chanzo cha mabadiliko hayo!