SoC01 Mabadiliko ya Mifumo ili kuchochea maendeleo

SoC01 Mabadiliko ya Mifumo ili kuchochea maendeleo

Stories of Change - 2021 Competition

Manventure

Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
10
Reaction score
4
Maendeleo ya taifa yanachangiwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mifumo na sera zilizopo kwenye nyanja mbalimbali kama uchumi na biashara, afya, maendeleo ya jamii, utawala bora, demokrasia, kilimo, sayansi na teknolojia, haki za binadamu. Mabadiliko kadhaa yanaweza kufanywa kwenye hizi sekta au nyanja ili kuongeza ufanisi zaidi na kuliletea Taifa maendeleo. Baadhi ya mambo yanayoweza kufanyiwa maboresho na mabadiliko ni pamoja na yafuatayo.

Namna ya kupambana na kutokomeza malaria. Ugonjwa wa malaria umekuwa ni tishio sana na umeleta athari kubwa kiafya katika nchi nyingi zilizo ukanda wa tropiki. Lengo la kuandika ni namna ya kupambana na ugonjwa huu. Mwandishi mmoja wa gazeti mwaka 2016 aliandika "mapambano ya malaria zamani na sasa ni tofauti...". Zamani tulifunzwa mazalia ya mbu huwa katika majani marefu, maji yaliyotuama na mazingira machafu. Ili kupambana na malaria ni lazima kisafisha mazingira, kufukia mashimo na kuondoa maji yaliyotuama. Lakini sasa silaha ya upambanaji imehamia kutumia chandarua sana. Chandarua hakiui mbu bali kinazuia. Ni heri kutokomeza mazalia ndiyo kutumia chandarua kuliko kuacha mazalia halafu kutumia chandarua pekee. Elimu hii imesahaulika sana kwenye sekta ya afya. Hivyo elimu irudishwe tena.

Sera tofauti kwa wakuu wa nchi kila awamu. Taifa letu japokuwa ipo Katiba ya nchi inayotoa mwongozo lakini bado utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Kila Rais katika awamu yake huwa na sera yake muda wa utawala wake. Mfano, "Sera ya hayati J.K. Nyerere ilikuwa - Uhuru na Kazi", "Sera ya hayati B.W. Mkapa ilikuwa ni - Mageuzi ya viwanda na mifumo", "Sera ya J.M. Kikwete ilikuwa ni Kilimo", "Sera ya hayati J.P. Magufuli ilikuwa - Viwanda".³ Ijapokuwa sera hizo zimeleta maendeleo lakini kama kungekuwa na sera ambazo zimeainishwa kwa maendeleo ya taifa kila kiongozi afuate, Taifa lingefikia maendeleo kwa haraka na ufanisi zaidi kulinganishwa na kila uongozi kuunda sera yake binafsi.

Kodi na makato mengi kwa wafanyakazi au watumishi wa umma. Tozo na kodi tunakiri zina manufaa mazuri katika kuendeleza taifa lettuce lakini zinapokuwa nyingi hupunguza kiasi cha pesa anachopokea mtumishi wa umma au mfanyakazi. Mfano, tuangazie mshahara wa mwalimu. "Uhalisia wa mshahara wa mwalimu baada ya makato...
mfuko wa hifadhi ya jamii (35,800 sawa na 5%)
,
Bima ya afya (21,480 sawa na 3%),
CWT (14,320 sawa na 2%),
bodi ya mikopo (107,400 sawa na 15%),
income tax (86,580 sawa na 12%)."²

Kama mtumishi huyu angepunguziwa makato angeweza kujiinua kiuchumi zaidi na kuongeza pato la mtu binafsi ikilinganishwa na sasa. Mapendekezo yangu ni mamlaka husika ni kupunguza makato angalau kuweka ahueni kwa watumishi. Ambapo mwisho itakuza uwezo wa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Utendaji kazi wa mamlaka huru nchini. Mamlaka huru ni taasisi za kiserikali ambazo zinafanya kazi bila kuegemea upande wowote katika utekelezaji wake. Mfano ni Mahakama, Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), TAKUKURU, n.k. Mamlaka hizi zitakuwa na uhuru kamili na utendaji madhubuti endapo zitakuwa na utaratibu wake kamili na wa ndani zaidi. Mfano, nchini Tanzania hizi mamlaka huru wakuu wake huteuliwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano. Sifa hii inatoa uhuru kamili katika utekelezaji wa majukumu kwa sababu kiubinadamu ni vigumu kumgeuka alokuinua. Ili ufanisi uendelee hamna budi Katiba ya nchi itoe mamlaka ya uongozi wa taasisi huru kwa Mamlaka husika na sio mkuu wa nchi.

Uzalishaji na utengenezaji dawa za binadamu ndani ya nchi. Wizara ya afya imekuwa ikitumia fedha nyingi kuagiza madawa nje ya nchi. Tanzania imekuwa ikinunua dawa kutoka Asia, nchi za Ulaya na Amerika. Kuagiza madawa huongeza gharama kwa taifa na pia kwa wananchi. Mfano, "Serikali ya Tanzania yatumia sh. bilioni 334 kununua dawa, chanjo na vifaa tiba."¹ Gharama hizi zingepungua zaidi endapo kutakuwa na viwanda ndani ya nchi kwa sababu teknolojia ipo, rasilimali zipo, wawekezaji wapo pia. Pia kwa upande wa usalama wa madawa haya ni heri kuzalisha ndani kwa sababu sio dawa zote zitakuwa salama na halisi. Baadhi ya dawa zinapungua viwango kutokana na ushindani kwenye soko la dunia, uhuru wa bidhaa kutokana na utandawazi. Hivyo, ili kuimarisha sekta ya afya tuwe na viwanda vya utengenezaji wa dawa ndani ya nchi.

Mwisho, kiujumla mabadiliko kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo nidhamu na utekelezaji ndio nyenzo zinazoweza kufanikisha mambo yote. Kwa pamoja ili kuendeleza na kukuza Taifa letu la Tanzania kila mwananchi anapaswa kutekeleza kwa nafasi yake, mfano kwenye mapambano dhidi ya malaria. Na mengine mengi ili kutoka hatua moja ya maendeleo ya taifa hadi hatua nzuri zaidi.

Reference
³ www.mwananchi.com
² https://www.jamiiforums.com/threads/uhalisia-wa-mshahara......
¹www.malunde.com
 
Upvote 1
Back
Top Bottom