Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Kama ambavyo tumewahi kujadili hapa JF kuhusu makelele yaliyokithiri katika miji yetu. Ipo haja katika mabadiliko ya sheria za mazingira ambayo yatajadiliwa bungeni kuhakikisha hivi vipaza sauti bubu katika masoko, fremu za maduka na vibiashara ndogondogo zinadhibitiwa.
Kwa sasa wauza sumu ya panya, wauza nguo, wauza nyama, wauza nguo kila mmoja unakuta ana spika yake inaita biashara, yaani ni vurugu mtindo mmoja hakuna utulivu kabisa. Hii inasababisha ukosefu wa utulivu kwa watu na misongo ya mawazo.
Pia katika vituo vya madaladala
unakuta Walokole na Maspika yao, ni kuunguruma mtindo mmoja. Naamini katika taratibu za mipango miji, shughuli za Ibada zimetengewa maeneo maalum japo kwa dharura za hapa na pale zinaweza kufanyika ktk viwanja kadha wa kadha.
Kuhusu adhana za Waislamu, kama ile ya Alfajiri iwe strictly ni kuhusu adhana, isizidi dakika 3. Na pia Kiwango cha sauti ambacho spika za msikitini kiwe kile ambacho hakina madhara kwa masikio ya watu.
Haya mamiziki ya matangazo yanayopitishwa barabarani katika magari ya matangazo huku kukiwa na wasanii wakiimba na kucheza ili kutangaza bidhaa fulani yadhibitiwe, haya yanakosesha sana watu utulivu.
Haya mabodaboda yanayofunga spika za miziki nayo yazuiwe, ni hatari kwa usalama barabarani.
Mabar yanayopiga miziki ktk makazi ya watu nayo itafutwe namna ya kudhibiti hiyo hali.
Pengine watu hawaelewi kuwa utulivu wa kiakili wa watu unasaidia ktk productivity. Ukivuruga utulivu wa watu hata nchi haiwezi kuendelea.
Haya makelele mijini yatafutiwe dawa!