Tetesi: Mabadiliko ya Sheria ya NGOs, baadhi ya Wabunge wameshindwa kujificha kimaadili na kukubali kupokea fedha

Tetesi: Mabadiliko ya Sheria ya NGOs, baadhi ya Wabunge wameshindwa kujificha kimaadili na kukubali kupokea fedha

blix22

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
213
Reaction score
645
Wakati Bunge likijiandaa na ukusanyaji wa maoni ya wadau katika mabadiliko ya Sheria ya NGOs (The Non-Governmental Organization Act), baadhi ya Wabunge wameshindwa kujificha kimaadili na kukubali kupokea fedha mchana huu maeneo ya Morena Hotel -Dodoma ili wapaze sauti zao.

Wabunge wengi inasemekana wana mahusiano na taasisi na asasi za kiraia kwa muda mrefu na kupata vijisenti na huenda wakaathiriwa na sheria hiyo ambayo lengo lake ni kuweka miundo mizuri na kuwarahisishia mchakato wa kuhudumia wananchi ambao walikuwa wanasumbuka kupata usajili au katika usimamizi.

#My Take: Suala la Mabadiliko ya Sheria halihitaji Lobbying. Wabunge wajenge utaratibu wa kutazama maslahi ya wananchi na nchi kwa ujumla bila kujali itikadi zao au kuongozwa na fedha.
 
Back
Top Bottom