Theb
JF-Expert Member
- Jan 25, 2019
- 3,927
- 7,276
Habari zenu wakuu wa JF.
Kwenye andiko hili nitaelezea baadhi ya maboresho yanayohitajikika au yanayo paswa kutekelezwa ili kutuletea maendeleo na pia kuendana na ukuaji wa uchumi duniani.
MABORESHO ni nini..?
Maboresho, ni mabadiliko yanayofanyika katika kutekeleza jambo fulani ambalo lipo tayari lakini lina onesha mapungufu kiasi ya kuhitaji kubadilishwa kwa baadhi ya vitu au mambo.
Nitaonesha maboresho yanayohitajika kwenye idara mbali mbali kama inavyofuata:-
1. Maboresho katika mfumo wa elimu nchini
Elimu ndiyo nguzo kuu katika maendeleo ya taifa lolote ama jamii yoyote ile. Kwa kuangalia mfumo wa elimu itolewayo nchini, ni mfumo ambao hauwaandai vijana kujiajiri kwa asilimia kubwa kwa maana unawajenga kutegemea kuajiriwa hili ni kutokana ni mfumo wa elimu yetu.
Maboresho katika mfumo wa elimu.
(i) Michezo na burudani kuwa sehemu ya elimu itolewayo mashuleni kuanzia shule za msingi mpaka ngazi ya vyuo.
(ii) Masomo ya vitendo yenye kuendana na mazingira au hitaji la jamii yawe sehemu ya elimu itolewayo nchini. Mfano elimu ya stadi za kazi haipewi kipaumbele zaidi wakati inaweza kutuzalishia wasusi, wachoraji, wafinyanzi, waimbaji, wapishi, na wachongaji. Sanaa iwe sehemu ya masomo ya shuleni.
(iii) Elimu itolewe kwa kuendana na sayansi na teknolojia inavyokua nchini na kuendana na ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
(iv) Kufanyika kwa tafiti mbali mbali zitakazo tumika katika kufanya maboresho pendekezwa niliyotaja hapo juu (i),(ii) na (iii).
(v) Utolewaji wa elimu uzidi kuzingatia usawa wa kijinsia katika jamii zetu
2. Uongozi bora unaozingatia misingi ya demokrasia.
Uongozi ni nguzo nyingine muhimu katika kuchochea maendeleo ya jamii au taifa kwa ujumla.
Uongozi bora nini..?
Uongozi bora ni uongozi unaofuta sheria za nchi na kuongoza kwa mujibu wa katiba.
Maboresho yanayoweza kutekelezwa kwenye uongozi nchini kama ifuatavyo:-
(i) Uongozi unaosimamia demokrasia imara.
Hapa lazima tuwe na demokrasia imara hususani kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi na kila mhimili wa serikali uweze kujitegemea. Mfano Bunge liweze kutekeleza majukumu yake bila hofu ya kuingiliwa na mhimili wowote ule.
(ii) Katiba kufanyiwa maboresho penye mapungufu na penye uhitaki kutokana na matakwa au hitaji la wananchi na sio mahitaji ya viongozi.
(iii) Uongozi wenye kutambua haki za binadamu au raia wake na kuzingatia usawa wa kijinsia katika uongozi nchini.
(iv) Uongozi unao simamia sheria katika kuongoza.
(v) Uongozi usiokuwa na upendeleo wa kikabila, kidini, kikanda, kiitikadi na usio na ubinafsi.
(vi) Mgawanyo wa madaraka kwa viongozi na uadilifu, uwajibikaji, uaminifu na uzalendo kwa viongozi wote.
(vii) Uongozi unaoweza kuchukua sheria kwa mujibu wa katiba kwa viongozi wabadhirifu na wala rushwa kwa maslahi mapana ya taifa letu.
3. Maboresho katika utoaji wa huduma za kiafya nchini.
Ili taifa liwe na nguvu kazi lazima wananchi wawe na afya bora. Maboresho wizara ya afya.
(i) Kuandaa wataalamu wa afya mfano madaktari na wauguzi kwa wingi na wenye ujuzi unaoendana na sayansi na sayansi na teknolojia ya sasa duniani.
(ii) uboreshwaji wa hospitali na vituo vya afya vilivyopo pia ujenzi wa hospitali na vituo vya afya zaidi kila mkoa kila wilaya kila kata na mapaka ngazi ya vijiji hii itarahisisha utoaji wa huduma za dharura.
(iii) Utumiaji wa nyenzo za kisasa yaani katika kutoa huduma za kiafya tutumie nyenzo za kisasa kufundishia na kutolea huduma. Tuendane na mahitaji ya sayansi na teknolojia.
(iv) Bima za afya ziwe kwa watanzania wote na sio kuwa bagua wengine hasa masikini ambao kipato chao kidogo wanashindwa kupata bima za afya.
4. Maboresho katika masuala ya uchumi nchini.
Hapa nitaangazia wawekezaji, wajasiriamali, wafanyakazi wa uma na sekta binafsi, viwanda, biashara na miundo mbinu kwa ujumla. Na maboresho hayo ni kama ifuatavyo:-
(i) Sera za uwekezaji ziwe wazi na wezeshi kwa wawekezaji wote wa ndani na wa kigeni.
(ii) Miundo mbinu iwe bora kote nchini, hapa barabara, njia za reli, viwanja vya ndege, bandari na vyombo vya usafiri wa majini pia huduma za mawasiliano ziwe bora kurahisisha usafirishaji na mawasiliano katika kutekeleza au kufanya biashara kwa wananchi wote. Kuanzia mijini mpaka vijijini kote miundo mbinu iwe bora na fanisi.
(iii) Ukusanyaji wa kodi unaofuata sheria. Hapa mlipaji kodi na mchukua kodi wote lazima wafuate sheria kwa maslahi ya taifa letu.
(iv) Maslahi ya wafanyakazi yaweze kuboreshwa. Yatasaidia kukuza uchumi na kuleta uadilifu pia kupunguza mianya ya rushwa.
(v) Wawekezaji na wafanyabiashara nao wazalishe bidhaa bora na kutoa huduma zilizo bora na pia kusaidia jamii kupiga hatua katika maendeleo ya jamii.
(vi) Mashirika ya kibiashara na kiuchumi yatoe mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo nchini. Mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba pia.
5.Maboresho katika kilimo,
Kwenye kilimo nitatoa mapendekezo yakuangazia ili kuboresha kilimo nchini kama ifuatavyo:-
(i) Upatikanaji au kuwepo na wataalamu wa kilimo nchini kwa kila mkoa wilaya kata mpaka ngazi ya vijiji wawe zaidi ya mmoja kutokana na uhitaji uliopo hususani maeneo ya kilimo nchini.
(ii) Upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakulima wote nchini.
(iii) Miundombinu iwe bora na yenye kuwezesha usafiri na mawasiliano tokea shambani mpaka kufikisha mazao sokoni.
(iv) Kilimo cha kisasa kutiliwa mkazo na umwagiliaji uwezeshwe kwenye kilimo kuondokana na utegemezi wa mvua katika kilimo.
(v) Upatikanaji wa soko kwa mazao yanayo zalishwa shambani ili kumkomboa mkulima aondokane na umaskini.
(vi) Kilimo kiwe kwa biashara na sio kwa ajili ya chakula tu.
(v) Ufugaji uwe kwa ajili ya biashara na uwe wa kisasa unaoendana na mahitaji ya viwanda, mfano uzalishaji wa manyoya kupitia kondoo kwa ajili ya viwanda.
6. Maboresho katika sayansi na teknolojia nchini.
Ili kuendana na dunia kwa ujumla lazima taifa liweze kumundu ukuaji wa sayansi na teknolojia ambazo pia ni.nguzo muhimu katika maendeleo katika taifa lolote. Maboresho yawepo kama ifuatavyo:-
(i) Uhusiano bora na mataifa mengine katika tafiti za kisayansi na teknolojia iwe mataifa ya bara la Afrika au taifa lolote duniani.
(ii) Kuandaa wataalamu wengi nchini katika nyanja mbalimbali wenye ujuzi uliomithilika na kuendana na ukuaji wa sayansi na teknolojia. Na mashuleni mpaka vyuoni matumizi ya komputa yawezeshwe.
(iii) Kuruhusu na kuwezesha tafiti mbalimbali kwa wanafunzi na watafiti mbalimbali iwe wa kiafya au masuala ya anga na ugunduzi wowote ule.
Faida za maboresho niyopendekeza yakitekelezeka:-
(i) Maboresho katika mfumo wa utoaji wa elimu ukiboreshwa utawajenga vijana kuweza kujitegeme na kujiajiri kupitia ujuzi watakao upata.
(ii) Faida za maboresho katika uongozi demokrasia na haki za binadamu. Yatasaidia katika kuleta ukosiaji, uadilifu na kuhusisha maamuzi.ya wananchi.
(iii) Faida zitakazo patikana kilimo kikiboreshwa. Itatusaidia kupata mazao mengi kwa ajili ya biashara na viwanda kwa kuuza ndani na nje ya nchi.
(iv) Faida za maboresho miundo mbinu itasaidia usafirishaji na mawasiliano kuwa rahisi na haraka.
(v). Uchumi wa taifa utakua kutokana na maboresho yote.
(vi). Maisha ya mtanzania yataboreshwa pia na kuwa na unafuu zaidi ya sasa.
Mambo ya kufanyika ili tuweze kupata maboresho:-
1. Ngazi ya serikali.
Serikali lazima ihusike moja kwa moja katika kufanya maboresho yote niliyopendekeza katika andiko hili. Serikali itahusikaje...?
(i) Kuwezesha maboresha yote niliyopendekeza katika andiko hili.
(ii) Serikali kujali imani za kidini kwa raia wake bila kuwabagua wala kuwatenga maana ni msingi moja wapo na haki ya kila binadamu katika kuabudu na kiitikadi. Kila mtu kwa imani yake ana haki sawa kwa wote.
(iii) Kusimamia haki na sheria katika utekelezaji wa kazi za kiserikali bila kuonea wala kupendelea mtu yeyote nchini.
(iv) Kuajiri vijana na kuwaandaa kuwa viongozi wa taifa la kesho. Wananchi wote hawawez kujiajiri lazima tuwe na kundi litakaloongoza jamii.
(iv) Serikali kuwa na mahusiano mazuri kikanda kibara na duniani kwa ujumla. Hii itasaidia biashara na mataifa mengine
2. Ngazi ya jamii.
(i) Jamii kutunza rasilimali za nchi, miundo mbinu na kuwa sehemu ya kuinua pato la taifa kwa kulipa kodi kwa kila mtu kulingana na kipato chake na shughuli afanyayo na iwe shughuli halali kulingana na sheria za nchi yetu.
(ii) Jamii kufuata maadili mema na kujali na kuheshimu kila mtu na imani yake bila kulumbani au kuvunjiana heshima.
(iii) Kila mtu afuate na kutii sheria na kuwa mzalendo wa taifa letu.
(iv) Jamii ichangie na ishiriki katika maboresho ya kikatiba au kwenye chaguzi au sensa nchini hii itasiadia kujua hitaji la wanajamii.
Hitimisho.
Wote jamii na serikali kwa ujumla na mtu mmoja mmoja lazima kushikamana ili kuweza kufikia maboresho hayo lendekezwa kwenye andiko hili. Ni jukumu la serikali kuboresha mazingira ya utafutaji, elimu, afya na uongozi bora pamoja na miundo mbinu pia.
Mwisho wa andiko langu. Ahsanteni wote niwatakie tafakari njema kupitia andiko hili

Upvote
2