Mabadiliko yenye utata

BEAKER

Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6
Reaction score
1
Kwa akili ya kawaida ni vigumu kuamini kama J. Ntatiro angehama chama cha upinzani lakini kutokana na viashiria vya chama tawala hilo halikwepeki cha kufanya sasa hivi ni kupokea tu taarifa maana alishapangiwa mipango tokea muda ambao ulikuwa ukisubiriwa kwenye makubaliano juu ya mapokezi.
Watu wengi wanapotafuta pesa ama utajiri kwa njia ya kawaida kwa muda mrefu na hatimae kukosa kwa wale wenye roho ndogo lazima watumie njia mbadala kuupata utajiri hivyo basi kwa wale wote waloguswa na changamoto hizi za kuhma hama vyama vya siasa na kujifunika na mwamvuli wa kuunga mkono sio vibaya kwao lakini ni fedheha kwa wapiga kura na dharau bila kusahau matumizi mabaya ya pesa za umma na muda.

Ikumbukwe kwamba mtu anaacha ubunge au udiwani anajiunga na chama kingine hallafu anapiga kampeni kugombea tena kwa kutumia pesa ya walipa kodi bila kujali upotezaji muda na kuingiza gharama zisizo za lazima. pia wananchi tusikubali huu ujinga akija aambiwe maliza muda wako kisha uje ugombee kipindi cha pili ukiwa chama kingine ili kuokoa pesa ambazo zinzweza kununua vitanda kuweka hospitali .
Ninachokiamini pesa ina nguvu sana na ni vigumu kuushinda moyo wenye tamaa na hakuna biashara isiyo na faida. Huwezi kufanya biashara miaka 9 usione faida bana hivyo tusiwalaumu wanaotuingiza gharama mara kwa mara bali tulaumu mfumo wa serekali unaokubali jambpo hili ingawa lipo mkikatiba lakini liwe na kipimo . Amini usiamini idadi ikitimia uchaguzi utafanywa kwa pamoja ili kupunguza gharama kwa hiyo bado breaking news zitakuwepo tu.
 
Nasikia anapewa ukuu wa mkoa..ila sisemi ni upi.. kuna anaebadilishwa
 
Kweli inahitajika elimu...... elimu , elimu , elimu. Stasahau huu usemi siku ya kwanza niliusikia pale jangwani sio yanga aka vyura bali ilikuwa ni siku ya ufunguzi wa campaign za uchaguzi kwa mgombea wa UKAWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…