Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mabaharia wote waliokuwa kwenye MV Tutor iliyopigwa na Houth hapo juzi na kusababisha tobo kubwa pamoja na moto wameondolewa kwenye meli hiyo ambayo imeanza kunywa maji.
Awali baharia mmoja alipotea baada ya shambulio hilo wakati ambapo meli za kivita za Marekani zilijaribu kuzima moto uliojitokeza.
Baada ya tukio la juzi kwa mara nyengine jeshi la Marekani lilitumia nguvu kubwa kupiga wanachosema ni radar zinazotumiwa na Houth kuzitambua na kuzipiga meli zinazopita kwenye mkondo huo wa bahari zenye mafungamano na Israel,Marekani na Uiengereza
Katika hali hiyo imeelezwa ya kuwa Marekani imezama kwenye tope la kupigana na Houth ambalo linaweza kuwazamisha kiuchumi na hawataweza kulishinda kundi hilo linalosema linawatetea raia wa Palestina.
Mara kwa mara meli zinazoshiriki kuzilinda meli zinazopita Red Sea au zinazowashambulia Houth zinalazimika kurudi Marekani kwenda kujaza mahitaji ya matumizi ya askari pamoja na silaha hasa kwa vile nchi kadhaa za Mashariki ya kati zimekataa kutoa msaada kwa Marekani katika vita vyake na Houth wakizingatia onyo lililotolewa awali na wanamgambo hao.
Sababu nyengine ya ugumu kwa Marekani katika vita hivyo ni gharama kubwa za makombora wanayotumia kupigana na Houth wanaotumia vifaa vya thamani ndogo sana kuzilenga meli wanazozikusudia.
Zaidi soma hapa,