BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile anawakaribisha Mabalozi wote wa mashina na wajumbe mkutano mkuu wa jimbo la Mufindi Kusini kwenye Mkutano Maalumu wa Jimbo utakaofanyika Jumamosi hii Oktoba 05, 2024 kwenye Viwanja vya Igowole Shule ya Msingi. Mgeni rasmi kwenye shughuli hii kubwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu John Mongella.