Katika pita pita zangu mitandaoni nimeona wenzetu wazungu wameadvance sana. Especially wanaokaa kwenye maeneo makubwa, wanawekeza katika kujenga mabanda ya kuku yanayotembea (mobile chicken coop).
Wengine wanayawekea magurudumu. Banda laweza kuwa round kama ilivyo greenhouse farming, au laweza kuwa na shape tofauti.
Kinachofanyika banda linajengwa katika mfumo ambao kuku wanasimamia kwenye wavu, vinyesi vinadondoka chini baada ya muda fulani mfugaji anaenda anasogeza tu banda hatua kadhaa mbele either kwa kusukuma kwa mkono au kulivuta kwa kutumia guta au gari (inategemea na ukubwa wa hilo banda).
Nimefikiria, hivi kuna watanzania walioanza kuwekeza katika mbinu hii? Faida yake,kuku au vifaranga wanakuwa salama dhidi ya wanyama kama mbwa na ndege waharibifu kama mwewe au tai.
Pili hauhitaji kufagia mbolea maana inadondokea moja kwa moja shambani.
Tatu, hawapigwi na jua kali maana banda linakuwa na kivuli ambacho mara nyingi ni turubai au bati.
Unaweza kuwa mbunifu kipande kidogo kinaweza kisiezekwe ili ikitokea kuna kuku wanaohitaji jua wanaweza kuota jua wakiwa kwenye banda.
Nikipata designer mzuri nataka kuwekeza katika hii kitu maana naishi shambani nina eneo kubwa. Kama kuna mtu anamfahamu designer mzuri naomba tushee uzoefu na kupeana connections.
Kwa haraka haraka designer anatakiwa awe mtu anayeshughulika na kuchomelea, pamoja na fundi wa vyombo vya moto kama bajaj (nafikiria kuweka matairi ya bajaj. Naomba kuwasilisha