Nafahamu kwamba leo ndo mwisho wa kampeni na kesho hakuna hata anayeruhusiwa kuvaa au kupeperusha bendera ya chama chochote ktk kituo cha kupigia kura. Ktk kampeni hizi CCM imetundika mabango mengi nchi nzima ikiwa ni sehemu ya kampeni.
Tegemeo langu ni kuona kwamba leo ni mwisho wa kampeni mabango yote ya CCM yataondolewa. Kinyume cha hili watakuwa bado wanaendelea kupiga kampeni siku ya uchaguzi.