Elections 2010 Mabango ya JK yaliyofichwa


Dada sio ulaya, piga hesabu ndogo tu, hizo pesa zilizoibwa kwenye EPA, RADAR, NDEGE YA RAIS, RICHMOND, MEREMETA, APTL, TWIN TOWERS na zingine nyingi tu zinazofujwa kwenye semina, safari za viongozi zisizokuwa na tija n.k unafikiri zingeshindwa kufanya kazi ya kujenga shule na kununua madawati? Angalia kiasi cha magogo yanayokwenda nje, kweli TZ ni nchi ambayo watoto wanatakiwa kukaa chini? Hebu angalia upotevu wa mabilioni kwenye halmashauri zetu (Pathetic!)

Issue kubwa inayoliangamiza taifa letu ni governance tu, tukiweza kwenye governance basi sidhani kama kuna nchi EAST AFRICA if not Africa inayoweza kutusogelea kwa maendeleo.
 
Wapendwa niwaambie kitu muhimu saana, Ng'ombe kufungwa kamba shingoni anafikiri ni haki yake kumbe kuna alternative ya kufungwa mguuni, watanzania waliowengi wanafikiria hayo maisha ya hao watoto na mwalimu ndio maisha yao na wanafikiri hakuna mabadiliko, wapendwa tunatakiwa kufika maeneo ya Vijijini kueneza huo ujumbe kwamba maisha hana yanasababishwa na CCM na tuweke chama mbadala CHADEMA kuyondo hayo matatizo, ama kweli ccm mtaji wao ni umaskini na ujinga wa watanzania.
 
Maisha bora kwa kila mtanzania yameyeyuka!
 

Mzee, nakubaliana nawe. Wazazi wa hawa watoto walio matumbo nje na wanaoishi kwenye mitaro ya maji machafu wanashindwa kabisa kuunganisha hali ya maisha yao na uongozi wa nchi. Itachukua muda na inahitaji nguvu ya ziada kuelimisha watu!
 

Mzee, nakubaliana nawe. Wazazi wa hawa watoto walio matumbo nje na wanaoishi kwenye mitaro ya maji machafu wanashindwa kabisa kuunganisha hali ya maisha yao na uongozi wa nchi. Itachukua muda na inahitaji nguvu ya ziada kuelimisha watu!
 

Kwa nini kila mwanafunzi akianza shule ya msingi au sekondari aende na dawati. na siku ukimaliza std 7 au Form 4 hauruhusiwi kuondoka na dawati lako. siku hizi walimu wameona ndio pakupatia dili unapewa form imeorodhesha dawati na malipo yake hapo pembeni. mtu unajiuliza shule imekuwepo miaka zaidi ya 10 madawati yamekwenda wapi na wanafunzi wamekuwa wakipeleka madawati kila mwaka????

Na ni familia ngapi huko majumbani wanaketi kwenye viti au meza na sio kwamba hawataki lakini wanaona ni bora chakula kuliko kununua meza na viti, mambo ya vipaumbele ambayo viongozi wetu wameshindwa kutumia akili zao walizopewa bure na Mungu pamoja na kujienjoy na elimu za bure mpaka Phd lakini ni sawa na bure tu hakuna mpangilio wa kipi kije kwanza na kipi kifuate na kipi hakina umuhimu. kwao wao wanaanza na the least important on the list. this is not the way to go hata nyumbani kwako mwenyewe lazima uwe na vipaumbele sembuse a whole Nation.
 

if you think education is expensive, then try ignorance!!!!!
 
Kweli Mungu timiza ahadi yako maana wewe Mungu umeikuza ahadi yako kuliko jina lako. Sikia maombi tuyaombayo wana na binti zako, ikiwa tumetenda dhambi tusamehe, kama hatuwezi tuwezeshe ila tunaomba mkono wako uende na kila mtanzania ktkt kituo cha kupiga kura tukachague yule ambaye umemweka wakati huu atutoe kwene tabu na dhiki hizi
 
Ni kweli tumetenda dhambi, Mungu tusamehe Tanzania na uondoe nguvu ya uchawi na giza lililotuloga sisi Watanzania na kutufanya kuwa tulivyo. AMEN
 



ELIMU BORA
CHAGUA CCM
CHAGUA KIKWETE

MIONGONI mwa hawa wapo ama kijijini kwako, au kijiji cha moja wa ndugu, jamaa na marafiki zako!!1 je, wewe kama Mtanzania mwenye uchungu na nchi yako umefanya nini hadi sasa ili kuwaondolea hadha hiyo? Sitaki kuamini kwamba solution pekee unayoiona ni kwa CCM kuondoka madarakani peke yake kwani u can do something hata wakati CCM ipo kwa power!
 
Hizi ndizo picha ambazo kama ingekuwa inawezekana kuwekwa kwenye billboards zingeipatia chadema plus. Ila ndio haiwezekani maana nasikia Cuf walimwendea Zadock wakitaka waweke matangazo kwenye mabango yake, akawajibu kuwa pesa nazipenda sana lakini sithubutu kukubali matangazo ya upinzani, maana watanidhibiti!
 
Ukiangalia vizuri kuna mtoto mmoja kavaa Tshirt ya CCM! Kifupi katika mazingia haya huwezi kujua kinachoendelea duniani, unafikiri huyu mwalimu anafahamu uozo wa CCM? Hapo ndipo CCM inapopiga bao, hebu imagine eneo kama hilo yet kuna tshirts za ccm!!!!!!!!!
 
Inashangaza sana kwamba sehemu za Tanzania ambazo watu wengi kama hawa wanapatikana ndiko ccm inashinda kwa wengi.

Sababu moja ni kwamba watu hawa ni rahisi sana kudanganywa kwa kanga, t-shirt, kofia, chumvi, sukari n.k.

Namuunga mkono sana yule jamaa aliyepewa tshirt ya kikwete na badala ya kuitumia yeye aliitinga kwa mbwa wake.

Hana kosa lolote kisheria ua lipo wanasheria.
 
Amina kubwa sana na mapenzi ya BWANA na yatimie.
 
Ni Kweli kabisa. Hii ni TZ. Jamani mpaka tumepata recognition UN. Kumbukeni!
 
Hawa hata zile peremende hawakupata

Peremende au wanasubili kupata MARELIA na Kipindupindu huoni hapo pembeni! Daaaa halafu eeeti wanapewa MBU NET za nini!? kuna watu ambao hawajui mahitaji ya watanzania! Ndiyo maana bagamoyo ipo kama ilivyo!
 
unajua jinsi hawa sisem wanavyojua kugeuza wajinga waliowengi watanzania kuwa mtaji wao wa kisiasa eti watu washasahau mara hii mwaka 2005 kauli mbiu ilikuwa MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ndani yake ndo kuna elimu bora<ndo kama hiyo picha hapo juu>, afya, maji, na kumwezesha mtanzani kuchumi ambapo leo inflation imepanda mara 4-5 tokea 2005 hadi leo.
lakini ccm baada ya kuona haijafanya lolote ikaamua kupiga kimya juu ya hiyo kauli mbiu yaMAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, haisemi chochote juu ya hiyo, ila tumegundua kuwa maisha bora ya yanawezekana kwa wachache yaani MAFISADI. Na ndo maana wameungana mafisadi kutetea maisha yao bora kwa kuendelea kuwadanganya watanzania.

Ila mara hii uelewa wa watanzania umekuwa mkubwa na ccm wakasahau hilo na ndicho kitakacho wamaliza.

ewe mtanzania shime tukapige kura 31 .10.10 kwa kishindo ili tufanye mabadiliko ya kweli

Mungu ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…