Mabango ya kampeni za uchaguzi 2020 yenye picha ya Hayati Magufuli yaondolewe mara moja

Mabango ya kampeni za uchaguzi 2020 yenye picha ya Hayati Magufuli yaondolewe mara moja

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Uchaguzi ulikwisha.

Na kwa bahati mbaya sana Mungu alimpenda zaidi tuliyempenda, hivyo sio vema kuendelea kuona sura yake ikipiga kampeni kwa picha zile za unyenyekevu.

Kwa Dar es Salaam hili lilifanyika punde tu parapanda ilipolia, sijui ni kwamba hawakumhitaji tena au zile nguzo zilipangiwa kazi nyingine.

Nimetembea mikoa kadhaa na kushuhudia bado mabango yapo, hii haileti picha nzuri. Anastahili kupumzika kwa heshima.

Kuendelea kuanika sura yake ikiwa katika unyenyekevu ule wa kuomba kura ni utani mkubwa kwake.

Apumzike kwa amani, Dr. JPM.
 
Dah na yalivyokuwa mengi...sijui na Bajeti yake ilikuwa bilions ngapi? Na ilitoka mfuko upi.
 
Unyenyekevu wa kuomba kura??

Kumbe kuzimia watu mtandao ambao kwa dunia ya sasa ni duka la kila kitu kwa siku 5 ndio ulikua unyenyekevu?

Angalia hapo bango linavyotolewa kwa unyenyekevu pia

 
Back
Top Bottom