Mabango ya Waganga wa KIENYEJI, ni KERO au usanii mpya kwa Watanzania!!!

Mabango ya Waganga wa KIENYEJI, ni KERO au usanii mpya kwa Watanzania!!!

NKUU SINDE KWETU

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
830
Reaction score
91
Salaam JF!
Tanzania hivi sasa kuna staili mpya ya kupata Fedha! Huhitaji kutumia nguvu bali ni kucheza na akili ya mtu.

Kila unapopita utakuta tangazo la mganga wa kienyeji na wanaweka na namba zao za simu. Mpaka huku kwetu Nkuu siku hizi wapo..

Magonjwa wanayotibu sasa: Kumvuta mpenzi aliye mbali, kuongeza hips, makalio, kulipiza kisasi, kuongeza akili za darasani...etc kazi kweli kweli..

Kila mganga anaandika anatoka Sumbawanga, Tanga, Kigoma, Pemba....

Hivi serikali iko wapi wakuu,,??
Au sio kero kwa Jamii??

NKUU SINDE, Nduguyenu..
 
Wana JF,
Hivi kuna namna Mganga wa Kienyeji anaweza kuongeza akili za wanafunzi??

Nazikumbuka shule zetu za Kata...
 
hawa waganga wangekomboa nchi katika hii hali iliyopo sasa kuliko kuongeza makalio ambayo yanazidi kuongeza matatizo mitaani kwa baadhi ya watu,
 
Kama wanaongeza akili za darasani basi ningewashauri wale ndugu zangu wa rangi ya kijani waongezewe, labda itasaidia kidogo mambo kwenda sawa!
 
Nadhanikuna haja ya kuwaongezea uwezo kila mganga apate helikopta ya kupasua anga wapite kila shule ya msingi, secondary, vyuo vya ufundi, nk wawaongezee wanafunzi akili. sasa tatizo akili za za kuchanjwa chale sehemu za siri ni akili au matope? shenzi zao,,,,,,
 
Ongezeko la matangazo ya waganga wa jadi nchiniTZ hususan Dar wanaodai kuwapa watu utajir yanaleta picha gani kwa jamii?
 
watanzania wanaamini ushirikina sana hasa watu wa dar ni wavivu mno hata kupenda vya dezodezo
 
Ni kwamba Shetani muda wake umeisha sana hivyo anafanya kila njia ya kuwalaghai watu ili apate wa kwenda naye, time is really running out.
 
Back
Top Bottom