Godlisten9
Member
- Jul 14, 2021
- 7
- 5
Kilimo cha Bangi,kuweka tozo na kupunguza posho za watumishi wa Serikali katika kuongeza pato la Taifa mbadala wa tozo za simu, mafuta ya petroli, dizeli, mafuta ya taa, mafuta ya chakula na sukari.
Habari nawasalimu wadau na wana JF wote, nina imani mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku.
Nimewaleteeni story of change fupi na ambayo inaleta tija kwa wanajamii wa namna zote na wa hali zote, kwa kukusanya maoni mbalimbali kwa wadau mbalimbali ninaomba pia mchango wenu.
Huduma za simu katika nchi yetu kwa kipindi hiki kifupi zimeonekana kuingia katika mvutano mzito kati ya serikali, wamiliki wa makampuni ya simu za mkononi na wananchi kwani hali ya maisha imekuwa ngumu na isiyotabirika huku karibu kila kitu kikipanda bei iikiwemo
Serikali imesababisha mitandao ya simu:
Kwa kuingiza sheria mpya.
Picha na mtandao.
Hii ni bei ya zamani na ya sasa katika kutoa na kuweka hela
MIBADALA YA KODI ZA UZALENDO
KILIMO CHA BANGI
Bangi ni majani ya mmea wa kike wa mbangi (Cannabis). Ndani yake mna dawa inayosababisha namna ya ulevi unaotegemea kiasi cha dawa kinachoingia mwilini
Katika ripoti moja ya mwaka 2019 ya Taasisi ya masuala ya bangi Afrika (Africa Regional Hemp and Cannabis), inasema afrika ina mchango wa millioni $37.3 katika soko la dunia la bangi ikiwa ni sawa na 11% ya pato duniani.
Nchi mbalimbali hivi karibuni zimearifiwa kuhalalisha kilimo cha bangi, ikaririwe vyema sio kuhalalisha matumizi ya bangi bali kubalalisha kilimo hicho kwa maslahi mapana ya pato la taifa kwa mfano Nchi ya Jamaica,mexico, uhispania, ureno na brazil ambapo nchi hizi sio rahisi kuzifukuzia kiuchumi katika Korea Kaskazini
Bangi hukua kwa wingi sana Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni
Nchi na mabara yaliyoendelea yanaichukulia bangi katika nafasi kubwa ya kuendeleza uchumi wa nchi zao.
JAMBO LA KUSHANGAZA
Serikali ya Tanzania ikiruhusu kilimo cha Bangi itaanza kwa upande wa serikali peke yake kulima na kuanza kuuza nje ikifuatia sekta binafsi kuanza kulima na kuuza nje halafu kukata kodi katika mauzo hayo, bangi isiruhusiwe kwa matumizi ya nyumbani bali kwa matumizi ya dawa na kuuza nje ya nchi kupata fedha za kigeni
Faida za bangi
Umewahi kujiuliza kwanini Tanzania kuna kesi za bangi? Je jumla za faini zinazotozwa kwa waliokutwa na makosa ya bangi na jumla ya kodi zitakazotozwa pale mauzo ya bangi yatakapofanyika ni kipi kiasi kikubwa cha fedha kwa serikali?
👉Ni kutokuwa na akili ya mali kuteketeza hekari za bangi kama Tanzania ifanyavyo ikiwapata wakulima wa zao hilo.
Picha na mtandao.
KUPUNGUZA AU KUWEKA MAKATO KATIKA POSHO NA MISHAHARA YA WATUMISHI WA UMMA
Watumishi wa umma haswa wabunge hapa nchini wanalipwa hela kubwa ambazo hizo ni kodi za wananchi ambapo katika hela zao za mishahara kuna uwezekano wa kuweka kodi na katika posho zao za kila kikao na za kila mwezi pia.
Mfano Mbunge anapokea Tsh milioni 12 kama mshahara wa mwezi katika kila kikao wanachofanya sio chini ya millioni tatu mpaka sita wanazopewa viongozi bila tozo ya asilimia yoyote lakini leo hii hivi vihela vidogo vya wananchi ndivyo wanavyolilia.
Asilimia 15% kwa 20% walitakiwa wakate katika mishahara na posho za wabunge na mawaziri kama ni kodi ya uzalendo kwanini tusiwe wazalendo wote tunakuwa wananchi pekee yetu?
Mawaziri na wakurugenzi wanalipwa mamilioni ya fedha za wananchi masikini wanaotozwa kodi katika mishahara pamoja na kodi za hao hao wanamchi lakini wao wanapolipwa posho na mishahara yao haina tozo.
Ili kucompasate na kodi ya uzalendo kuliko kuwaumiza watanzania wa hali ya chini ni bora nchi ifanye
1.Kilimo cha bangi kwa sekta binafsi na Za umma
2.kuwakata wabunge na watumishi wengine wa serikali kiasi katika posho zao wanazopokea katika vikao vyao vingi na mikutano ya siasa zikiwa zote ni kodi za wananchi.
Maoni ya wadau👉pale Twitter
MUHIMU
IKUMBUKWE KWAMBA MAWASILIANO NA MIAMALA YA SIMU NI HUDUMA KAMA HUDUMA NYINGINE HIVYO HUDUMA SIKU ZOTE TIJA YAKE KUBWA NI KUIBORESHA NA SIO KUIKANDAMIZA NA KUWAUMIZA WATU PASI NA HAPO ISIMAMISHWE.
Katika nchi mbalimbali inaonekana kuboresha zaidi huduma za mawasiliano kwa mfano Marekani na uingereza.
Rwanda imeboresha huduma za mawasiliano karibu nchi nzima,kenya na uganda wameonyesha unafuu kuizidi tanzania katika mawasiliano na teknolojia
Katika nchi ya Tanzania huduma za simu zipo chini hazina ubora wala hazijafikia kiwango cha kusema watutoze kodi kubwa hivyo kuna sehemu haya makampuni hayajaweka hata minara yao, ukituma au kutoa pesa meseji itakuja kesho, ukinunua data bei ni kubwa Network unatafuta mwenyewe, wanatudanganya ni 4G, ukikosea kutuma pesa inarudi ndani ya siku tatu hadi nne, ukituma meseji haiendi, mtu akikupigia haupatikani na laini ipo hewani wanapata wapi ujasiri wa kuweka vifurushi na tozo au makato juu kiasi hicho wanatukosea heshima sana.
BAADHI YA MAONI YA KUJENGA KUHUSU MIAMALA YA SIMU
Kwa upande wa vocha na vifurushi
Kwa upande wa miamala kutoa na kuweka hela
Hitimisho
Tuiangalie katiba mpya ni nyenzo kuu katika kubadili haya maamuzi yanayopitishwa bila kuchukua maoni ya wananchi.
Toa maoni yako.
Imeandikwa na Godlisten mwasha

- Makato ya miamala kutoa na kuweka pesa katika mitandao yote ya simu
- Kupanda kwa bei za vifurushi na mabadiliko ya vifurushi kwa mitandao yote.
- Bei ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa shilingi 100 kwa kila lita.
- Pombe kupanda bei
- Mafuta ya kupikia na sukari vipo juu
- Kodi za kila aina zinapanda na zinazidi kupanda
Serikali imesababisha mitandao ya simu:
- Kubadili bei za vifurushi
- Kubadili vifurushi
- Kupandisha bei za miamala/transactions
Kwa kuingiza sheria mpya.
Picha na mtandao.
Hii ni bei ya zamani na ya sasa katika kutoa na kuweka hela
MIBADALA YA KODI ZA UZALENDO
KILIMO CHA BANGI
Bangi ni majani ya mmea wa kike wa mbangi (Cannabis). Ndani yake mna dawa inayosababisha namna ya ulevi unaotegemea kiasi cha dawa kinachoingia mwilini
Katika ripoti moja ya mwaka 2019 ya Taasisi ya masuala ya bangi Afrika (Africa Regional Hemp and Cannabis), inasema afrika ina mchango wa millioni $37.3 katika soko la dunia la bangi ikiwa ni sawa na 11% ya pato duniani.
Nchi mbalimbali hivi karibuni zimearifiwa kuhalalisha kilimo cha bangi, ikaririwe vyema sio kuhalalisha matumizi ya bangi bali kubalalisha kilimo hicho kwa maslahi mapana ya pato la taifa kwa mfano Nchi ya Jamaica,mexico, uhispania, ureno na brazil ambapo nchi hizi sio rahisi kuzifukuzia kiuchumi katika Korea Kaskazini
Bangi hukua kwa wingi sana Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni
- Nchi kadhaa za kiafrika ikiwamo Lesotho iliidhinisha kilimo cha bangi kwa ajili ya tiba, na matumizi ya nyumbani.
- Zimbabwe ni nchi ya pili barani afrika kuruhusu kilimo cha bangi.
Kati ya tarehe za 14.10.2020 Rwanda iliruhusu bangi itumike kimatibabu na kiuchumi
Nchi na mabara yaliyoendelea yanaichukulia bangi katika nafasi kubwa ya kuendeleza uchumi wa nchi zao.
JAMBO LA KUSHANGAZA
Serikali ya Tanzania ikiruhusu kilimo cha Bangi itaanza kwa upande wa serikali peke yake kulima na kuanza kuuza nje ikifuatia sekta binafsi kuanza kulima na kuuza nje halafu kukata kodi katika mauzo hayo, bangi isiruhusiwe kwa matumizi ya nyumbani bali kwa matumizi ya dawa na kuuza nje ya nchi kupata fedha za kigeni
Faida za bangi
- Hutumika kukinga na kutibu presha ya jicho(glaucoma) na presha ya kawaida
- Kuboresha mapafu na kuondoa madhara ya tumbaku katika mapafu
- Ina tetrahydrocannabinol au THC kemikali inayosaidia kuzuia kifafa.
- Ina cannabidol au CBD kemikali inayoweza kupunguza na kuzuia kansa.
- Kupunguza maumivu ya mwili na kutibu utumbo pia huongeza kinga ya mwili
- Katika chuo kikuu cha Nottingham mwaka 2010 tafiti zilionyesha kuwa kemikali zilizopo kwenye bangi hushirikiana na seli za mwili kuongeza kinga ya mwili na maumivu ya tumbo.
Umewahi kujiuliza kwanini Tanzania kuna kesi za bangi? Je jumla za faini zinazotozwa kwa waliokutwa na makosa ya bangi na jumla ya kodi zitakazotozwa pale mauzo ya bangi yatakapofanyika ni kipi kiasi kikubwa cha fedha kwa serikali?
👉Ni kutokuwa na akili ya mali kuteketeza hekari za bangi kama Tanzania ifanyavyo ikiwapata wakulima wa zao hilo.
Picha na mtandao.
KUPUNGUZA AU KUWEKA MAKATO KATIKA POSHO NA MISHAHARA YA WATUMISHI WA UMMA
Watumishi wa umma haswa wabunge hapa nchini wanalipwa hela kubwa ambazo hizo ni kodi za wananchi ambapo katika hela zao za mishahara kuna uwezekano wa kuweka kodi na katika posho zao za kila kikao na za kila mwezi pia.
Mfano Mbunge anapokea Tsh milioni 12 kama mshahara wa mwezi katika kila kikao wanachofanya sio chini ya millioni tatu mpaka sita wanazopewa viongozi bila tozo ya asilimia yoyote lakini leo hii hivi vihela vidogo vya wananchi ndivyo wanavyolilia.
Asilimia 15% kwa 20% walitakiwa wakate katika mishahara na posho za wabunge na mawaziri kama ni kodi ya uzalendo kwanini tusiwe wazalendo wote tunakuwa wananchi pekee yetu?
Mawaziri na wakurugenzi wanalipwa mamilioni ya fedha za wananchi masikini wanaotozwa kodi katika mishahara pamoja na kodi za hao hao wanamchi lakini wao wanapolipwa posho na mishahara yao haina tozo.
Ili kucompasate na kodi ya uzalendo kuliko kuwaumiza watanzania wa hali ya chini ni bora nchi ifanye
1.Kilimo cha bangi kwa sekta binafsi na Za umma
2.kuwakata wabunge na watumishi wengine wa serikali kiasi katika posho zao wanazopokea katika vikao vyao vingi na mikutano ya siasa zikiwa zote ni kodi za wananchi.
Maoni ya wadau👉pale Twitter
MUHIMU
IKUMBUKWE KWAMBA MAWASILIANO NA MIAMALA YA SIMU NI HUDUMA KAMA HUDUMA NYINGINE HIVYO HUDUMA SIKU ZOTE TIJA YAKE KUBWA NI KUIBORESHA NA SIO KUIKANDAMIZA NA KUWAUMIZA WATU PASI NA HAPO ISIMAMISHWE.
Katika nchi mbalimbali inaonekana kuboresha zaidi huduma za mawasiliano kwa mfano Marekani na uingereza.
Rwanda imeboresha huduma za mawasiliano karibu nchi nzima,kenya na uganda wameonyesha unafuu kuizidi tanzania katika mawasiliano na teknolojia
Katika nchi ya Tanzania huduma za simu zipo chini hazina ubora wala hazijafikia kiwango cha kusema watutoze kodi kubwa hivyo kuna sehemu haya makampuni hayajaweka hata minara yao, ukituma au kutoa pesa meseji itakuja kesho, ukinunua data bei ni kubwa Network unatafuta mwenyewe, wanatudanganya ni 4G, ukikosea kutuma pesa inarudi ndani ya siku tatu hadi nne, ukituma meseji haiendi, mtu akikupigia haupatikani na laini ipo hewani wanapata wapi ujasiri wa kuweka vifurushi na tozo au makato juu kiasi hicho wanatukosea heshima sana.
BAADHI YA MAONI YA KUJENGA KUHUSU MIAMALA YA SIMU
Kwa upande wa vocha na vifurushi
- Kama sitaweka salio wiki nzima watakata wapi hiyo hela?
- Nitakuwa na tumia simu siku za week end tu.
- Serikali imeanza kuwasumbua makampuni ya simu kwanini pamoja na wananchi kulalamika serikali imewapangia makampuni bei elekezi bila kuwashirikisha watu wenye busara na maarifa ama wananchi.
- Ni afadhali watunyime kutumia simu kabisa
Kwa upande wa miamala kutoa na kuweka hela
- Serikali yetu ni kandamizi haimpi mwananchi nafasi ya kutoa maoni na kuchangia mabadiliko inatumia nguvu na mawazo ya watu wachache wenye madaraka ambapo pengine sio waliopewa dhamana na wananchi bali wamepachikwa.
- Ni bora kama hawatushirikishi katika maamuzi muhimu kama hayo basi na sisi pesa zetu tutahifadhi katika masanduku au mikebe huko nyumbani.
- Kuliko nitume pesa kwa kutumia simu bora nipeleke mwenyewe nauli ni mdogo kuliko gharama za kutuma na kutolea
- Sasa ni muda wa kuhamia zaidi kwenye mabenk yana bei nafuu kidogo.
- Posho za wabunge zikatwe VAT uchumi ukuzwe sasa jini maana ya huduma??
- Si bora hizo hela nipeleke kwa bodaboda niwasalimie na kuwasalimia ndugu zangu?

Upvote
3