Mabaraza ya Kata

Mabaraza ya Kata

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887
TAMBUA MABARAZA YA KATA HAYANA MAMLAKA YA KUSIKILIZA NA KUAMUA MIGOGORO YA ARDHI TENA.

Na Comred Mbwana Allyamtu(CMCA)
Sunday-01/05/2022
Sumbwanga, Rukwa, Tanzania

Leo itupendeze tutajadili jambo mujadidi kuhusu mabaraza ya aridhi ya Kata.

Mjadala wetu leo utajikita katika kutazama mamlaka (jurisdiction) na nafasi (locus standi) ya mabaraza hayo katika kusikiliza mashauri ya migogoro ya aridhi.

Kwa mujibu wa Sheria ya mabadiliko ya Sheria namba 3 ya mwaka 2021, yani Written Laws (Miscellaneous Amendment No 3 ) Act, 2021, ambayo kimsingi imekuja kufanyia marekebisho Sheria ya The Land Dispute Courts Act Cap 216 RE 2019 kwenye kifungu cha (15).

Kwa mujibu wa sheria hii ambayo ilikifuta kifungu cha 15 cha sheria ya The Land Dispute Courts Act, Cap 216 R E 2019, ambacho kifungu hicho huko mwanzo kiliwapa mamlaka baraza la kata (Ward tribunal) Kusikiliza mashauri yanahusiana na masuala ya ardhi.

Kifungu hicho cha 15 ilikuwa ni lazima kisomwe pamoja na kifungu cha 10 cha Sheria Ya Mabaraza ya Kata Sura Ya 206 Marejeo ya mwaka 2002 yani The Ward Tribunal Act Cap 206 R.E 2002.

Ambapo vifungu vyote hivyo viliwapa mamlaka ya Kusikiliza na kuamua masuala yote yanahusiana na mambo ya ardhi yasiyozidi thamani ya shilingi million tatu (3,000,000/=)

Kwa maana hiyo sasa baraza la kata lilipewa nguvu za kimahakama ambapo tunaweza kusema ilikuwa ni kama "mahakama ya mwanzo".

Kwahiyo sehemu ambayo mtu alikuwa anaanzia kufungua Kesi inayohusu mambo ya ardhi ilikuwa ni baraza la kata mtu asiporidhika anakata rufaa kwenda baraza la nyumba na ardhi la wilaya, rufaa yake inaenda mahakama kuu kitengo cha Aridhi na Kisha mahakama ya rufani, Hivyo ndivyo ilikuwa utaratibu wa mashauri ya migogoro ya aridhi ilivyokuwa.

Sasa mwaka 2021 kuliwasilishwa mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria mbalimbali ambayo yalifanywa, moja ya mabadiliko hayo na pamoja na hili la mabaraza ya aridhi ya Kata.

Mabadiliko mengine ilikuwa ni pamoja na kuruhusu mawakili kwenye mahakama ya mwanzo, kutokuwahusisha wazee wa mahakama kwenye Mahakama ya mwanzo na mengine kadhaa ambayo tutajadili siku za usoni huko mbeleni kwa kudra za Mungu.

Sasa turudi kwenye mabadiliko ya Sheria ya mabaraza ya aridhi ya Kata.....

Mabadiliko hayo ni kwamba baraza la kata halina mamlaka tena ya Kusikiliza na kuamua masuala yoyote ya ardhi (kutoa hukumu) au nguvu za kimahakama na kiufupi tunaweza kusema wame nyang'anywa mamlaka ya kimahakama.

Kwasasa baraza la kata linafanya kazi kama baraza la usuluhishi tu.

Hapa narudia tena, kwa sasa mabaraza ya aridhi ya Kata yatakuwa na mamlaka ya kufanya kazi kama baraza la usuluhishi tu, yaani ikitokea Kuna watu wana mgogoro unahusiana na ardhi akienda baraza la kata watawasikiliza na wanatoa ushauri tu kuwa labda kwenye suala hili mtu B umeingilia kwa Mtu A na hivyo hilo shamba uliache basi.

Kwa namna nyingine tunaweza kusema baraza watawasikiliza na kutoa ushauri tu au kuwasuluhisha na kuhakikisha suala lenu linashughulikiwa bila kufikia kwenye vyombo vya kisheria.

Hii inamaana kwamba Baraza la kata watakuwa hawana mamlaka hata ya kuandaa hukumu/ Kwasasa baraza la kata haliwezi kutoa hukumu hivyo latageuka na kuwa baraza la usuluhishi.

Na baraza la kata wanatakiwa kusuluhisha suala hilo kwa muda wa siku 30 na watatakiwa kutoa cheti ikiwa watu wenye mgogoro wameshindwa kufika hitimisho au maamuzi.

Hii inamaanisha kuwa iwapo kama mgogoro haujasuluhishika basi mmoja wapo asiyeridhika basi atapewa na cheti ambacho kimetolewa na baraza la kata na Kisha ataenda nacho baraza la aridhi la wilaya kifungua shauri rasmi katika baraza la nyumba na ardhi la wilaya ambapo litasikilizwa rasmi ikiwa ni pamoja na kutolewa hukumu.

Mabadiliko ya Sheria hii imetaka mashauri yote ambayo yalikuwa yakiendelea kwenye baraza la kata hayo yataendelea kwa utaratibu wa zamani na yatatakiwa kumalizika hadi kufika hatua ya hukumu.

Lakini Kesi yoyote inayoenda baraza la kata kwasasa sheria mpya itatumika, ikiwa ni pamoja na ule utaratibu wa Kusuluhisha tu na kupewa cheti pale ambapo mmoja wao hajaridhika ili kumruhusu kuendelea mbele kufungua shauri na Kusikiliza.

Utaratibu huu ni kama vile inavyo fanyika kwenye migogoro ya wanandoa mbele ya mabaraza hayo ya Kata, ambapo baada ya usuluhishi kufanyika na mmoja kutoridhika basi hupatiwa hati ya usuluhishi (form No 3) na kwenda nayo mahakamani kwajili ya michakato mingine ya kisheria.

Hivyo Sasa........

Kuanzia sasa ikitokea baraza la kata wakasikiliza shauri lolote la migogoro ya aridhi na kuandaa hukumu hilo litakuwa ni kosa kisheria na utaratibu huo utakuwa ni batili na hautakuwa na nguvu yoyote kisheria, "the procedure and proceedings shall be nullified so becomes fatal".
 
Back
Top Bottom