Mabasi ya mwendokasi yawe suluhisho kwa wanafunzi mikoani

Mabasi ya mwendokasi yawe suluhisho kwa wanafunzi mikoani

Gulugujatza

Member
Joined
Sep 1, 2024
Posts
61
Reaction score
143
Habari za Asubuhi mlio hai na kupata uzima wenye Nuru na baraka kutoka kwa Mungu Mwenye mamlaka ya dunia hii.

Leo Asubuhi Wakati naelekea kwenye mazoezi ya kuweka mwili fiti kidogo nilibahatika kupitia kwenye Barabara kubwa yenye mengi magari hapa mkoani kwangu,kubwa zaidi lilonifanya nifike hapa na kuliandika hili ni changamoto nilizoziona kwa wanafunzi ambao ni watoto wadogo ni kati ya darasa la 3 Hadi la 5 wakiwa wanahaha kupata usafiri kwa ajili ya kufika shuleni.

Changamoto kubwa kwao ilikuwa ni makonda wa daladala zile kwani waliweza kuwazuia wasiingie ndani ya gari na kushindwa kufanikiwa kwenda shuleni kwa wakati sahihi..,Sikupenda ikanibidi nikasimame nao kwanza kama mzazi na kuwaombea kwenye daladala hizo,kwa mbinde sana nilifanikwa na wakaondoka.

Nilipoiona ile changamoto nikapatwa na maswali na kujiuliza.

Hivi yale mabasi ya mwendo kasi ambayo yapo geleji hayawezi kurekebishwa na kugawiwa mikoani huku ili yakamsaidia mtoto huyu ambaye anapata hadha ya kunyanyasika huku kwenye hizi daladala?

Kutokana labda na uchache magari basi yangeanza kupita high way asubuhi na jioni kwa ajili ya wanafunzi tu hata wakisema 200 sawa tu ila mtoto awe na uhakika wa gari ya serikali linapita pale alipokuwa.

Soma Pia:

NIOMBE KWA SERIKALI YANGU
Hawa watoto wanaopata shida kwenye hizi stendi za daladala ni watoto walipa Kodi pia vile vile ni kizazi tegemezi kwa taifa la baadae.

Niombe kama basi za mwendo kasi zipo na zipo gereji embu zilekebisheni zisaidie Hawa viumbe,najua ni ngumu labda kuleta mapya ila hata hayo yaliyopo GELEJI yanaweza anza kusaidia kwenye hili jambo.

ASANTENI NAOMBA KUWASILISHA 🙏


mwendokasi.jpg
 
Back
Top Bottom