GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 309
CRDB: Kwa sasa hatuwezi kuizungumzia Uda
Na Jimmy Mfuru, 23rd March 2012
Wakati Shirika la Usafiri Dar es salaam (Uda), linasema mradi wa mabasi ya wanafunzi yaliyotolewa na Benki ya CRDB, unajiendesha kwa hasara na kufanya mabasi kusimama kutoa huduma kwa wanafunzi Jijini Dar es salaam, benki hiyo imesema kwa sasa hawawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa wanalifanyia kazi.Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kampuni ya Simon Group, Robert Kisena, ambae ni mbia katika Uda, alinukuliwa na NIPASHE kuwa mabasi hayo yanajiendesha kwa hasara na kuishauri benki hiyo ili mabasi hayo yaweze kujiendesha nyakati za mchana yabebe abiria wa kawaida.
Akizungumza na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano wa CRDB, Nasibu Kalamba, alisema kwa sasa benki hiyo haiwezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa linafanyiwa kazi.
"Kwa sasa Benki haiwezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa bado linafanyiwa kazi," alisema Kalamba.Benki ya CRDB ilitoa mabasi matano mwaka 2010 ambayo yalizinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa ajili kusaidia kubeba wanafunzi jijini Dar es Salaam ili kupunguza kero, lakini mabasi hayo kwa sasa yamesimama kwa zaidi ya miezi miwili bila kutoa huduma.CHANZO: NIPASHE