Mbalamwezi1
JF-Expert Member
- Dec 20, 2013
- 2,073
- 2,026
Kwenu wenye mamlaka, naandika ujumbe huu nikiwa ndani ya Basi la Saibaba kutoka Arusha kwenda Dar, basi hili ni la safari ndefu lakini linasimamisha abiria kama Daladala.
Hili ni Moja nililoshuhudia Mimi ila mabasi mengi yale yanayopaki stendi kuu ya Arusha yanafanya hivi, cha kushangaza hili basi limesimamishwa trafiki mwanamke hapa Makao Makuu ya Polisi (W) Arumeru na ameona kabisa basi Lina abiria wamesimama lakini hakuchukua hatua yoyote zaidi ya konda kushuka na kutia tu stori mbili tatu Kisha hao tukaondoka huku nikiweweseka kiwendawaImu.
Hii ni hatari kwa kwa kuwa ikitokea ajali hawa waliosimama kwenye korido ndio watakuwa wa kwanza kudhurika kwa kuwa hawana sehemu maalum za kishikililia.
Tusisubiri mpaka ajali itokee Kisha tuseme basi lilikuwa limebeba abiria zaidi ya uwezo wake!
Tafadhali askari wa barabarani tekelezeni wajibu wenu.
Pia soma KERO - Mabasi ya Abood (Dar - Moro -Dar) yanajaza abiria kupitiliza kama Daladala za Mbagala, hii si sawa