Mabasi yaliyokuwa yakisafirisha Wafuasi wa NASA yazuiwa na Askari wa Polisi

Mabasi yaliyokuwa yakisafirisha Wafuasi wa NASA yazuiwa na Askari wa Polisi

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Habari wanaJF,

Mabasi 3 ya Modern Coast yaliyokuwa yakisafirisha wafuasi 82 wa NASA hadi jijini Nairobi kwa kiapo cha Raila yazuiliwa mjini Voi. OCPD wa Voi Joseph Chesire asema mabasi hayo yamevunja sheria za trafiki.

> Wengi wa abiria ni vijana wasio na vitambulisho

=======

Nasa-buses+pic.jpg

Three buses that were transporting Nasa supporters from Mombasa to Nairobi have been intercepted in Voi, Taita Taveta County.

The buses were among six that left Mombasa for Nairobi ferrying the supporters to attend the swearing-in of Nasa leaders Raila Odinga and Kalonzo Musyoka.

TRAFFIC OFFENCES

Voi OCPD Joshua Chesire said the vehicles were seized for "traffic offences". They were stopped at Voi at around 3am, according to one of the supporters.

"In the buses there were 82 passengers who also had not adhere to traffic rules. Most of them are youth of whom 10 did not have ID cards. Among them are four women," said Mr Chesire.

He added that the passengers would be taken to court and charged with traffic offences.

BUSES

The Nasa supporters left Mombasa on Monday aboard six Modern Coast buses that awaited them at Treasury Square near Mombasa Governor Hassan Joho’s office.

Traffic police sources said the buses' number plates had earlier been circulated to them to ensure they do not proceed with the journey.

The buses were flagged off by Mombasa County Speaker Harub Khatri, who was accompanied by the county ODM Chairman Mohammed Hatimy.

Bus+pic+2.jpg

CANAAN

Speaking to journalists, Mr Khatri said the supporters were expected in Nairobi on Tuesday morning to witness Mr Odinga’s oath taking.

“We are determined in this struggle. We will have at least 50 buses transporting about 3,000 supporters. This is the beginning of the journey to Canaan. No one has been forced but we are doing [this] for the love our leader,” said Mr Khatri.

He said other buses would leave from Coast Bus offices.

Mr Khatri said Nasa supporters voted for Mr Odinga and Mr Musyoka in the August 8 General Election and the two leaders won but their victory was stolen by Jubilee.

“We know that we won that election and that is why we want to swear in our President – the people’s president. We voted for him and we must see him take the oath,” he added.

TRANSPORT

Mr Hatimy said no county funds was spent on transporting supporters.

“We want to put it clear that this is a party affair. Our speaker had promised to take our supporters to Nairobi and he has just fulfilled his promise. We will camp at Uhuru Park and see our leader taking the oath,” he said.

During Mr Odinga’s visit to Mombasa last week, Mr Khatri pledged to offer buses to transport the supporters to Nairobi for the Nasa event.

Police have warned people against going to Uhuru Park and its environs, saying they were not informed on the planned event.

Source: Daily Nation
 
Wakenya wakubali demokrasia ya Afrika ni tofauti na ya Magharibi, wamemaliza uchaguzi watulie wajenge familia zao.
Hizi habari ya kuapishana wakati rais tayari yupo ikulu, NASA supporter watakufa kwa sababu zisizo za msingi.


ILa nimependa ujasiri wao,kwa Tz haitokaa itokee.!!!
 
Wakenya wakubali demokrasia ya Afrika ni tofauti na ya Magharibi, wamemaliza uchaguzi watulie wajenge familia zao.
Hizi habari ya kuapishana wakati rais tayari yupo ikulu, NASA supporter watakufa kwa sababu zisizo za msingi.


ILa nimependa ujasiri wao,kwa Tz haitokaa itokee.!!!

Unatuombea balaa kama hilo na sisi litukute!!!!!!
Ati kisa wana democrasia!!!!!aseee tutakiane radhi mkuu tusiharibiane siku..
Nimetoka majuzi tu kifungoni(Bann)[emoji1321]
 
RAILA AMOLO ODINGA anaapishwa leo kuwa Rais wa Jamhuri ya watu wa Kenya, kama akifanikiwa na mpango wake huo anaweza kuiacha Kenya vipande, kama akiziuwa katika mpango wake huo, Kenya itabaki salama lakini Yenye kunukaa damu ya wafuasi wa NASA.., hii ngoma nzito kwa Rais Uhuru Kenyatta.

NASA wameshikilia msimamo wao kwamba RAO anaapishwa leo kuwa "RAIS wa Jamhuri ya Kenya" na sio "RAIS wa watu wa Kenya". Mshauri wa RAO anaitwa Salim Lone anasema RAI amefanikiwa kuliko kiongozi yoyote wa kitaifa katika siasa, anadai RAO "kashinda" chaguzi tatu na mabadiliko mara mbili ya katiba. Hivyo ni mwanasiasa anaependwa na wakenya.

Nguvu ya RAILA ipo wapi?

NASA wao wanasema RAO anashurutishwa na wananchi halali wa Kenya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Wanasema uchaguzi wa Oktoba ulikuwa ni "haramu" hivyo wanakwenda kutumia matokeo ya uchaguzi wa awali (August) kuapishwa kwa RAO ambae wanasema alishinda kwa kura milioni 8.7

RAO ana nguvu na ushawishi kwa wakenya. Ana wafuasi "loyal" sana kwake. RAO ndie alikuwa "instrumental in winning the presidency" kwa Mwai Kibaki mwaka 2002. Baadae wakatofautiana, RAO akiwa kiongozi wa ODM mwaka 2005 akaanza na vuguvugu la mabadiliko ya katiba.

Wafuasi wa RAILA wao wanaamini kwamba RAO ameshinda chaguzi za mwaka 2007, 2013 na 2017 na wanasema RAO anaporwa ushindi wake, wakati huu wamegoma na wanasema wanakwenda kufia UHURU PARK. wameuita "uwanja wa ukombozi"

Balaa linaanza katika uwanja wa kujiapisha (Uhuru Park)

Tatizo lipo katika Uwanja huo ambao NASA wamepanga kujiapisha leo (UHURU PARK). Serikali ya kaunti ya Nairobi wametangaza kuufunga uwanja huo kwa matengenezo. Na wamesema hakuna mkusanyiko wowote unatakiwa kuwepo hapo kwa siku hizo za matengenezo. NASA wamesisitiza hawana option nyingine ya uwanja zaidi ya UHURU PARK.

Wakati NASA wakiendelea na msimamo wao, serikali imetangaza kuufunga uwanja huo. Serikali pia imetangaza hali ya hatari kwa jiji la Nairobi. Ambayo itadumu kuanzia alfajiri hadi jioni. Kuna maeneo ambayo watu wamekatazwa kabisa kufika kwa siku ya leo.

Kauli ya mwanasheria mkuu wa serikali; attorney General (Githu Muigai) ameeleza kwamba, anachotaka kufanya RAO sio sahihi. Na kama akitenda hivyo tafsiri yake ni "UHAINI" adhabu yake ni kuhukumiwa kifo kwa kunyongwa. Kamanda wa police wa Nairobi (Japhet Koome) amesisitiza kwamba watamkamata yoyote ambae atahusika na uhaini katika jiji la Nairobi. NASA (CEO), Norman Magaya amejibu kauli hizo akisema "hawatishwi na vitisho hewa kamwe"

NASA wanasisitiza kwamba sherehe za kuapishwa kwa RAO ni agenda ya upinzani wao (Muungano wa upinzani). Wanasema wameshindwa kuvumilia kwa sababu RAO ameendelea kuporwa ushindi wake. Wanaelea kwamba uchaguzi huru na haki ni ule wa mwaka 2002 pekee. Na wanasema dirisha la mazungumzo sasa limefungwa wanakwenda kwenye vitendo.

Mbunge wa Rarieda, Otiende Amollo anasema wataendelea na mpango wao wa kumuapisha RAO kwa kutumia matokeo ya IEBC ambayo yanaonekana (kwa mujibu wao) RAO alishinda uchaguzi kwa kupata kura 8.1M wakati Uhuru alipata kura 7.9M.

Wakati huo, Gavana wa Siaya Cornel Rasanga, amesema anatoa mabasi yake bure kabisa kwenda kwenye eneo la tukio, wafuasi wa NASA Watafuatwa walipo popote (from all six sub-counties in Siaya) kwenda Uhuru Park. Wanasema lengo lao ni kuona RAO anaponya vidonda vyote vya maumivu ya uchaguzi. Mambo ni moto kweli-kweli.

Kwanini ni ngoma nzito kwa UHURU?

UHURU aliapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa marejeo. Ndie Rais, Je atakubali "sharubu" zake kushikwa na RAILA ambae anakwenda pia kujiapisha kwa jina hilo la "Rais wa Jamhuri ya Kenya?". Tusubiri kuona kiwango cha uvumilivu cha Uhuru Kenyatta katika hili.

Kuna kauli moja maarufu ya Malcom X inasema "BE PEACEFUL, BE COURTEOUS, OBEY THE LAW, RESPECT EVERYONE; BUT IF SOMEONE PUTS HIS HAND ON YOU, SEND HIM TO THE CEMETERY". Naona kabisa UHURU ameamua kufuata maagizo ya Malcom X katika hili. Hofu yangu ni kuona watu kadhaa wakimwaga damu baada ya sasa.

Ngumu sana kupambana na wafuasi wa RAO ambao wako "loyal indeed". Wafuasi hawa ndio walileta mabadiliko ya katiba, wakimwaga damu kila jumatatu ya mwanzo wa mwezi, Wafuasi wa RAO wapo tayari kufa wakiimba jina la RAO, wapo tayari kufuata lolote ambalo anasema RAO. Shughuli ni kubwa nchini Kenya. UHURU kichwa kinagonga.

Tusubiri na kuona.. Mambo yanakaribia, kuapishwa ni saa 4 asubuhi ya leo, wafuasi wa NASA wameanza kujongea kwa utaratibu kabisa UHURU PARK. Magari yaliyokuwa yamezuiwa barabarani yenye wafuasi wa NASA ndani yake yamepewa ruhusa kuingia mjini kutoka nje ya mji.. Kenya imepamba moto.

[emoji767] MMM, Martin Maranja Masese
 
Ninawaombea Amani Wamalize Salama. Kama Nawaona Hivi Polisi Wa Kibongo!!! Alafu NASA Ndiyo UKAWA,! Weeee! Wangejuta!!
 
Hakuna wanalojua wapinzani zaidi ya kufanya fujo halafu wasingizie wameonewa. Nazani nchi za kiafrika bado zinatakiwa kuongozwa na chama kimoja tu basi full stop
 
Back
Top Bottom