Mabati kuzunguka uwanja mpya wa taifa bado yanahitajika?

Kyachakiche

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2009
Posts
986
Reaction score
208
Kuna jambo linalonitatiza kidogo. Jambo lenyewe ni mabati yaliyozungushwa kwenye uwanja mpya wa Taifa tangu kipindi unajengwa hadi sasa wakati ukuta umekwishakujengwa na makabidhiano baina ya serikali ya China na ya Tanzania yameshafanyika karibu mwaka mmoja uliopita. Je, kinachosubiriwa ni nini? Bati zenyewe zimeshakuwa na kutu, zinaharibu mandhari nzuri ya uwanja, na pia si salama wakati wa mkusanyiko wa watu wengi kama jana kwenye mchezo wa Ivory Coast na Tz ambapo kusukumana kulikuwa jambo la kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…