Mabaya na mazuri ya toyota RAV4 old model

Duh kumbe noah ni mobile guest house? Ah ah ahh msituogopeshe jmn
 
RAV 4 matairi yake yanataga, baada ya muda matairi yanapinda pembeni.
 
hiyo gari ni nzuri sana hakikisha mara mbili mbili kua engine ni 3S kweli usije kua umeambiwa tu ukanunua yenye engine ya 4D....
RAV4 mayai (new model) inauzwa, engine ni D4
 
Sasa nimefikia maamuzi ya kununua toyota RAV4 old model milango 5,cc2000,3S,kama kuna mtu anaifahamu anijuze mabaya yake na mazuri yake plz

Ni pm, ninayo rav 4 old model naiuza, kama vipi nicheki
 
TIQO kumbe noah inateta heshima kitaa eeh! mh bora niikose tu hiyo heshima.
Huku kanda ya ziwa ukionekana na Noah tu, mtu hahitaji tena kukuuliza kabila lako, Kwani Noah inafahamika kwamba ni magari ya wasukuma!
 
Gari yoyote ina mabaya na mazuri depending on matumizi and so forth. Rav 4 ni nzuri especially hiyo ya 3s ila mafuta inakula kutokana na ukweli wa kwamba ni full time 4WD. Gear box hazisumbui kama service is on time pamoja nankwamba gari nyingi zenye full time 4WD zinasumbuaga gearbox
 
TIQO kumbe noah inateta heshima kitaa eeh! mh bora niikose tu hiyo heshima.

Unataka anunue Noah asbh na jion apakie abiria wapunguze makali ya mafuta?
 
Last edited by a moderator:
Nunua hutajutia hata kidogo maana hiyo ni gari ya starehe (haishuki heshima) halafu ni gari ya kazi kwa long way na roughs roads
 
Tatizo kubwa la RAV4 old model ni gear box, jana tu nimetaka kununua nilipoenda kwa fundi kuicheki kabla sijamlipa jamaa ikabainika ina tatizo la gearbox na kununua mpya ni kama ml1.2. Ila ni gari imara kama haima shida ya gearbox
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…