Nadhani ni ile ya kwamba tulikuwa tunatumia daftari moja kuandikia darasani na hilo hilo kufanyia kazi za nyumbani. Pia ilikuwa vitabu hatununuliwi tunategemea vya shule yaani kama kuna maswali basi mwalimu agawe vitabu kwa makundi tukae duara tusome maswali kisha tuandike. Au aandike maswali ubaoni tucopy.Khaaa,, kwa kweli huu ni mwisho wa mfumo, mbona kipindi chetu huko nyuma hatukua na haya mambo na madaftari na wengine tulibeba na chakula?
Kuna kadogoo kamoja huwa kanakujaga kusubiri school bus hapa stend, ukimuona akiwa na begi lake unaweza ukacheka. Ana kamwili kadogo halafu ni kafupi,begi ni kubwa kiasi kwamba linamgotea mapajani na akitembea lazima apinde mgongo kwa mbele ili akabiliane na uzito wa begi unaomvuta nyuma. Mungu awanusuru na balaa hili kwa kweliDuuh! Ila kwa sasa hasa hawa wa International School haizuiliki mtoto kutokuwa na begi kubwa sababu humo ndani wanabeba daftari za Class work labda tuseme sita na za Home Work nazo sita na hapo daftari zote ni zile za page 200 bila kusahau vitabu navyo hapo, maji ya kunywa sijui juice haijawekwa hapo yaani ni lazima mzigo uwe mkubwa.
Na ni ngumu kusema labda baadhi ya daftari ziachwe nyumbani au vitabu sababu vyote vinatumika.
Hiyo iliwezekana zamani tena kwa wale tuliosoma Kayumba.