Mabenki mengine mjihadhari, access bank itawanyang'anya wateja

koryo

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
639
Reaction score
278
Leoa asubuhi katika pitapita zangu nimeingia kama Beki mbili tofauti lakini cha kushangaza hakuna watu kabisa kama ilivyozoeleka kama zamani ambao mtu unaweza kukaa kwenye foleni hata masaa matatu. Nilipofika Accessbank kuuliza kulikoni kwa sababu watu walijaa sana wakanieleza kuwa gharama zao ni nafuu sana na hata ukiweka fedha zako kwa muda maalum wanatoa faida kwa kiwango kikubwa. Mfano:- ukiweka Tshs.50,000,000 kwa siku 30 unapewa faida ya 13.9%, miezi miwili 14.2%, miezi mitatu 14.5%, Miezi sita 14.8%, Miezi tisa 15.1%, Mwaka 15.4%. Hii ni tofauti kabisa na faida wanayotoa Benki zingine kama NMB au CRDB. Nilipouliza hii ni Benki ya wapi wakanieleza ni ya Kijerumani na ni Benki poa sana. Ninazishauri Benki zingine zibadilike vinginevyo watakuja kukimbiwa na wateja wao kama watakapokuja kufahamu AccessBank.
 
Anyway kuhusu interest katika deposit hao access siwajui vizuri. Ila ukitaka kufilisika kama wewe ni mjasiriamali nenda kakope access.
Mimi ni mteja wao wa mkopo sikuuliza vizuri rate ya interest wakati nakopa nilipelekwa tuu na jamaa yangu akaniambia wako vizuri na mkopo ni haraka. Nilikuwa nimetingwa kiasi fulani nikaenda wakanipa mkopo wa kama 35m kwa sababu ndio ilikuwa mara ya kwanza.
You can't imagine riba ya hiyo 35m ni zaidi ya 8m kwa Mwaka mmoja. Last wiki nimewapelekea hela yao yote yaani sina hamu bora hela za mtaani za moto.
 
Kwani interest yao asilimia ngapi?
 
Umetumwa ila hakikisha wanakulipa kwa tangazo hili
 
3.5% per month on straight line basis
asimia 42 kwa mwaka. ukienda bank nyingine ni asilimia 18 hadi 20 kwa mwaka. Ukiangalia balance sheet yao lazima utakuta wanakopa kwenye commercial banks kwa rate Kubwa. kwa hivyo ili watengeneze faida ni lazima wa charge hivyo
 
Hii benki noma sana mshahara laki nne kwa graduates. But wako very efficient kwenye operations lazima watakuwa na operations managers wazuri.

Mimi naiona kama bank ya kukimbilia watu wenye shida au waliopoteza imani kwenye mabenki mengine
 
Mkurugenzi wa Acess Bank kama hajabadilishwa anaitwa Mr. James. Mzungu mmoja hivi anaongea Kiswahili chote.

Alishawahi kufanya kazi Barclay's bank kwa zaidi ya miaka 30. Ana ujuzi na maarifa wa banking industry kwa muda mrefu. Labda ndiyo maana inafanya vizuri.
 
Hii benki noma sana mshahara laki nne kwa graduates. But wako very efficient kwenye operations lazima watakuwa na operations managers wazuri.

Mimi naiona kama bank ya kukimbilia watu wenye shida au waliopoteza imani kwenye mabenki mengine

hatudanganyiki ng'ooo.
 
Access Niliwahi kumdhamini mtangazaji fulani alikopa 5m hizo siku akichelewa rejesho mdhamini utatamani uzime sim siku nzima!
 
Hiyo asilimia 13.9% kwa siku 30 wewe utakuwa hujaielewa. interest ni kwa mwaka mmoja kwa hiyo hiyo 13.9% ya M 50 ambayo ni 6,950,000 unatakiwa tena uigawe kwa 12 ambayo utapata kitu kama 580,000.... ingawa sio mbaya ila pia kwa wafanya biashra sio nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…