Mabenki yangeangalia namna ya kupunguza makali ya uchumi mwezi wa Januari hata kwa kutoa mkopo kidogo

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Tanzania imekuwa kama wimbo. Ikifika Januari kila mtu analia hali ngumu ya uchumi. Miaka na miaka tunalia hii hali bila kuwa na suluhisho la maana.

Nashauri benki zingeangalia uwezekano wa kupunguza hii hali hata kwa kutoa mikopo midogo. Mtu hata kama anamkopo benki basi Januari aweze kutop hata laki tano au saba hivi kulingana na mshahara wake. Makato yake yaongezwe ili hii hela aweze lipa kwa miezi 12.

Kwa wafanyabiashara nako iwe hivyo kulingana na mahitaji na uwezo.

Hiki kilio cha njaa January huchosha sana.
 
Kweli ndugu Januari huwa na rabsha zake si za mchezo. Kumbuka pia mikopo isiyozalisha, ni kuongeza maumivu mengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…