Asante kwa kuanzisha mjadala huu.
Mimi nashindwa kuelewa pia, watu wa NBC ukienda kuchukua pesa yako wanakulazimisha uende ATM yao kuchukua balance na wanakukata 75/- halafu ukichukua pesa wanaongeza makato ya 500/- Hivi wanashindwa kuona balance ya mtu anayechukua pesa kwenye akaunti yake? Wanataka lazima uchukue ATM, uchomolewe 75/- Nadhani hiyo sio sawa. Unajua hata ukiuliza tu kuna pesa ngapi wanakuonyesha na kukata 75/-?
NMB wanajizungusha tuuuu, ukienda dirishani mjazano nadhani wao ni tija, kama sikosei wanafanya kazi kama benki ya Posta, ambako ukienda unapoteza siku nzima na wao wako bize hata hawajali wateja wana haraka zao pia.
DECI iliokoa watu wengi na mabenki wakajikuta hawana wateja tena, wakachoka utambi na benki kuu wakasingizia mambo kibao wakati hakuna mwanadeci hata mmoja aliyewahi kulalamika, badala yake wamehodhi pesa za walalahoi walioanza kuinukia DECI. Hao wanaoshikiliwa viongozi wa DECI wanasumbuliwa tu, nadhani mabenki wangebadilika, DECI ingeua mabenki yote maana hata kama inakuja leo tena watu kibao wataiunga mkono, hata mimi pia.
Leka