Kwa hiyo kesho si ajabu ukasikia Marando mwanasheria wa CCM, eti kwa sababu ana familia. Obama ni mwanasheria na kampuni yake haitoi utetezi kwa shauri lolote lenye maslahi ya kuwajenga republicans na hata wao hawa-consult kampuni hiyo kwa sababu hizo hizo. Kwa maneno mengine unataka kusema hata katika Chadema Marando alifuata mshahara na si itikadi. Na alikuwa mgombea wa uspika. Sina chuki na Marando lakini hapa kuna suala uadilifu na kama ningeandika kichwa cha habari ningesema kiongozi wa CDM atetea fisadi wa CCM. Kama ni familia, hata Nyerere alikuwa nayo wakati anaacha ualimu na kufanya siasa. CHADEMA INAPAMBANA NA MAFISADI NA SIO KUWAPAMBA.