Mabeyo: Jeshi libuni miradi kuisaidia Serikali

Mabeyo: Jeshi libuni miradi kuisaidia Serikali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
MKUU wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo amevitaka vikosi vya jeshi kutumia wataalamu wa ndani kubuni miradi ya kimkakati na kuhimiza uadilifu kwenye miradi iliyokamilika.

Mabeyo alisema hayo wakati wa kuzindua kituo cha mafuta cha R971 kilichojengwa na jeshi eneo la Ihumwa.

Alisema jeshi kama taasisi linaweza kufanya mambo makubwa na kinachotakiwa ni kujiamini, kuwa na mitazamo chanya, wakati wote kuwa wabunifu na waadilifu katika miradi hiyo.

“Hakuna kisichowezekana na wenzetu wameweza kwani sisi tusiweze, kuna taaluma chungu nzima ndani ya jeshi lakini tumezilaza, tuziibue taaluma tulizonazo kwa manufaa ya jeshi na taifa kwa ujumla, mimi bado naamini inawezekana,” alisema.

Mabeyo alisema pamoja na kuwa serikali ina wajibu wa kuhudumia jeshi kwa asilimia 100, bado kuna haja ya jeshi kuwa na mchango kwa nchi kama ilivyo kwa majeshi makubwa kwa kuanzisha miradi mbalimbali.

“Nilipata fursa za kutembelea maeneo ya ndani na nje ya nchi yakiwemo majeshi makubwa, wenzetu huko wanafanya mambo makubwa na wanachangia uchumi na pato la Taifa, lakini sisi tulikuwa tunategemea serikali kwa asilimia 100. Wajibu wa serikali kulihudumia jeshi ni kweli ndio dhana, je, sisi hatuna mchango wowote? Mchango wetu ni kuhakikisha tunachochea ukuaji uchumi na jukumu letu la msingi la ulinzi wa nchi na haya yanawezekana,” alisema.

Aidha, Mabeyo alisisitiza vikosi kuendelea kuimarisha miradi iliyokwisha kamilika na kufikiria miradi mikubwa zaidi na ya kimkakati.

“Fikra hizo ni lazima tuelekeze kwenye ubunifu, tubuni miradi mikubwa na ya kimkakati kama huu (kituo cha mafuta). Watu hawaelewi kama mafuta ni mradi wa kimkakati, mafuta yakikosekana katika nchi ina paralyzed nchi na iki paralyze nchi hakuna usalama katika nchi na ndio maana nilifikiria hili lazima tulibebe maana ni suala la kimkakati na la kiusalama,” alisema.

Mabeyo alisema hivi sasa jeshi linaangalia uwezekano wa kuagiza mafuta moja kwa moja ili kuwa na akiba ya nchi na kuwa na mitambo ya kusafisha mafuta nchini. Alisema kikosi cha R 971 ni miongoni mwa vikozi vitatu vilivyoanzisha miradi ya kimkakati. Vingine ni 12 KJ na 27 KJ. Mabeyo aliahidi kukipatia kituo hicho Sh milioni 100 kwa ajili ya kukipa uwezo zaidi ikiwa ni mbali na Sh milioni 100 zilizotolewa awali.

Pia alitoa wito kwa maofisa, askari na wakazi wa Ihumwa wenye vyombo vya usafiri kuwa wateja wa kwanza kwenye mradi huu wa kituo cha mafuta. Vile vile alipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kuwa mfano wa kutekeleza miradi ya kimkakati ukiwemo wa skimu ya umwagiliaji ambao umelenga kujilisha na kuweka akiba chakula.

Awali Kamanda wa kikosi R971, Kanali Justus Kitta alisema kituo hicho kimejengwa kwa gharama ya Sh milioni 280 kikiwa na matangi yenye uwezo wa kuhifadhia zaidi ya lita 60,000 za mafuta.

Alisema mkakati uliopo ni kuongeza visima zaidi na kujenga kituo kingine jijini Dodoma kabla ya kuwa na vituo vya mafuta kila mkoa.
 
Jeshi la biashara. Limepora fursa za wafanyabiashara. Shughuli zote za clearing and forwarding zinafanywa na jeshi, ulinzi kwenye ofisi mbalimbali za umma zinafanywa na jeshi kupitia kampuni yake ya Suma.

Ujenzi wa majengo mbalimbali unafanywa na jeshi.

Iko wapi nafasi ya wafanyabiashara/ wazabuni? Je tunakuza uchumi wa wa watu wetu au tunaudhoofisha?

Jeshi lijikite kwenye kulinda mipaka ya nchi yetu, biashara tuachieni wanyonge tuifanye
 
Pale lugalo tumeona fremu nyingi zinajengwa kwa mfumo wa uzio... nadhani ndo mojawapo ya uwekezaji wa jeshi kujipatia mapatoo

Wekeze kwenye viwanda vya nguo na viatuu ili tuwe tunavaa magwanda/combatii
 
Majeshi yalikua yameanza kubuni miradi mingi awamu iliyopita iliingia na kukwamisha machache katika jeshi.

Jeshi sasa linaamua kurudi taratibu liliko toka. Hizi sio wakati wa kujificha misituni tuu. Uzuri sasa kambi nyingi zimekutwa na mazingira ya mwananchi wa kawaida.

Kongole kwa jeshi
 
Jeshi la biashara. Limepora fursa za wafanyabiashara. Shughuli zote za clearing and forwarding zinafanywa na jeshi, ulinzi kwenye ofisi mbalimbali za umma zinafanywa na jeshi kupitia kampuni yake ya Suma.

Ujenzi wa majengo mbalimbali unafanywa na jeshi.

Iko wapi nafasi ya wafanyabiashara/ wazabuni? Je tunakuza uchumi wa wa watu wetu au tunaudhoofisha?

Jeshi lijikite kwenye kulinda mipaka ya nchi yetu, biashara tuachieni wanyonge tuifanye
Mnyonge ni wewe peke yako, unyonge sio sifa nzuri.
 
TPDF kwanza litekeleze wajibu wake kwenye kiapo chake ,kulinda mipaka yetu na SIO vinginevyo kwa sasa,nchi imegeuka kuwa ni hub ya syndicates za ajabu,from drugs lords to humans trafficking.
 
Kazi ya jeshi kubwa ni kulinda mipaka ya nchi pia inaweza kuchangia uchumi na ujenzi wa taifa kwa kutoa huduma katika sekta ya afya na elimu ila hilo la kufanya biashara litaleta ukakasi na itakua ni kichaka cha wapigaji kujificha.
 
Hujui jeshi wewe Jeshi dunia nzima nchi zenye utulivu na amani jeshi ni serikali yenye kila wizara na wataalamu

Mfano Afya wana hospitali za rufaa hadi madaktari bingwa kuliko popote hata Donald Trump alilazwa military hospital

Elimiu wana shule hadi vyuo vikuu na maprofesa wanajeshi

Engineering wana mainjinia wanajeshi wa kila fani tena registered kabisa kuanzia ujenzi,umeme,computa ,uinjinia wa magari,ndege,maji,nk

Siasa wako political scientsist s kibao na minyota ya kijeshi nk nk

Lengo moja nchi isihujumiwe wanasiasa wahujumu wakitaka kuhujumu jeshi linatoa watu wake linawaingiza uraiani kuendesha nchi bila shida

Pili wakipigana na kuteka nchi ya adui waweza shika nchi na kuiendesha bila shida

Tatu ni sehemu ya ulinzi wataalamu wao waweza jipenyeza kila sekta na kupewa nafasi kulinda hilo eneo au kuchunguza waweza JWTZ wakaingia hata chadema kama walinzi wawe wa mheshimiwa Mbowe nk hawashindwi kupenya hata ujitie mjanja vipi nk

Jeshi in multi sectoral sio tu kushika mibunduki hizo in theory za kizamani

Tii sheria bila shuruti
 
Jeshi la biashara. Limepora fursa za wafanyabiashara. Shughuli zote za clearing and forwarding zinafanywa na jeshi, ulinzi kwenye ofisi mbalimbali za umma zinafanywa na jeshi kupitia kampuni yake ya Suma.

Ujenzi wa majengo mbalimbali unafanywa na jeshi.

Iko wapi nafasi ya wafanyabiashara/ wazabuni? Je tunakuza uchumi wa wa watu wetu au tunaudhoofisha?

Jeshi lijikite kwenye kulinda mipaka ya nchi yetu, biashara tuachieni wanyonge tuifanye
Labda kwenye ulinzi pekee,sekta zingine mbona fursa bado tele
 
Labda kwenye ulinzi pekee,sekta zingine mbona fursa bado tele
Sekta kibao ziko wazi mfano gesi ya kupikia nilikuwa Ghana vijijini watu kusiko na barabara wanapeleka mitungi kwa punda sababu magari ya kampuni za gesi hayafiki kule !!! Wamejiongeza .Hapa kwetu gesi biashara mwisho miji mikubwa .Jeshi laweza ishika miji midogo karibu na kambi zao wakaweka maduka ya bei jumla ya majiko ya gesi ya kupikia wakawapa biashara bodaboda wakachukua maduka hayo jirani na kambi na kwenda kuuza rejareja huko ndani ndani vijijini kwa walimu,wakulima,nk kwa kuwapelekea majumbani au kujifungulia viduka vidogo vijijini vya maduka ya Gesi

Kampuni za gesi bado hazijawafikia watu wote kampuni za gesi zaweza pia mikataba ya kibiashara na JWTZ wao wana nagari yawezayo fika popote porini kwenye wateja

Kampuni za gesi ya kupikia zichukue hii kama opportunity ya kufikisha bidhaa zao remote areas kusikofikika na magari yao
 
Jeshi la biashara. Limepora fursa za wafanyabiashara. Shughuli zote za clearing and forwarding zinafanywa na jeshi, ulinzi kwenye ofisi mbalimbali za umma zinafanywa na jeshi kupitia kampuni yake ya Suma.

Ujenzi wa majengo mbalimbali unafanywa na jeshi.

Iko wapi nafasi ya wafanyabiashara/ wazabuni? Je tunakuza uchumi wa wa watu wetu au tunaudhoofisha?

Jeshi lijikite kwenye kulinda mipaka ya nchi yetu, biashara tuachieni wanyonge tuifanye
usisahau juzi kati wamezindua kituo chao cha kujaza mafuta. kama sikosei kipo barabarani ukikaribia kuingia dodoma kutokea morogoro.

mtu yoyote anaruhusiwa kwenda kujaza mafuta, ni pesa yako.
 
Back
Top Bottom