Mabibi harusi acheni kuwachoresha mabwana harusi kwa kuwalazimisha kucheza "stepu"!!

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
5,771
Reaction score
17,849
Kuna hii tabia imezuka siku za hivi karibuni japo ilikuepo pia zamani. Tabia yenyewe ni hii ya maharusi kuingia ukumbini huku wakicheza muziki kwa step ili "kuchangamsha" shughuli.

Kichekesho ni pale unapokuta mmoja wapo wa maharusi hasa mwanaume sio mtu wa muziki na hajui kabisa kucheza! Unakuta jamaa hana "moves" kabisa yaani mziki unaenda kushoto yeye anaenda kulia ila kakazana tuu kitendo kinachomfanya achoreke na kutia huruma huku watu wakianza kucheka.

Jamani, mimi naona kama mtu hujui kucheza we kubali yaishe tuu mnaweza kuingia mmeshikana mikono bila mbwembwe nyingi na mambo yakanoga.
 
kuna yule baharia akaamuaga kuutwika kabla,ndio akaharibu kabisaaa mpaka bibi harusi akawa analia[emoji28][emoji28]
 
Mambo ya kuiga tu
Kuna hii tabia imezuka siku za hivi karibuni japo ilikuepo pia zamani. Tabia yenyewe ni hii ya maharusi kuingia ukumbini huku wakicheza muziki kwa step ili "kuchangamsha" shughuli.

Kichekesho ni pale unapokuta mmoja wapo wa maharusi hasa mwanaume sio mtu wa muziki na hajui kabisa kucheza! Unakuta jamaa hana "moves" kabisa yaani mziki unaenda kushoto yeye anaenda kulia ila kakazana tuu kitendo kinachomfanya achoreke na kutia huruma huku watu wakianza kucheka.

Jamani, mimi naona kama mtu hujui kucheza we kubali yaishe tuu mnaweza kuingia mmeshikana mikono bila mbwembwe nyingi na mambo yakanoga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikuoe mimi na bado unilazimishe kucheza kwaito! Bora atafute X wake waingie naye ukumbini mimi nitabaki kuwatazama.
 
Bibi harusi wakat wa kuingia ukumbini nitamwacha aletwe na wazazi wangu mimi nitatangulia na wazazi wake mbele maana naweza pata aibu bure ukumbini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nashangaa kwanini mabibi harusi wa zamani walikuwa wakilia kuanzia siku ya send off hadi siku ya harusi yenyewe?

Lakini mabibi harusi wa siku hizi wamejaa over confidence yaani maconfo kwmw yote?!

Mabibi harusi makauzu utasema kitu gani?! [emoji848][emoji848]

Kwenye kucheza ndiyo usiseme wanacheza kama hawana akili nzuri jamani chaaah [emoji108]

Inashangaza sana!

Kuna send off moja nilihudhuria sasa wimbo aliochagua bi harusi kuingilia ukagoma ku play aisee ilikua ni shida bi harusi mtarajiwa kagoma katakata kuingia na wimbo mwingine zaidi ya saa nzima watu wamekaa wanasubiri..
 
Nikuoe mimi na bado unilazimishe kucheza kwaito! Bora atafute X wake waingie naye ukumbini mimi nitabaki kuwatazama.

Mkuu utacheza tuu mabibi harusi wa karne hii ni shida kwanza kwenye harusi kila kitu wanapanga wao kuanzia aina ya gari anayotaka kupanda, rangi ya suti yako, ukumbi nk.
 
Back
Top Bottom