mabibo hostel

MKINDE

Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
43
Reaction score
45
wana JF mimi ni new member ila ile nimeingia tu humu nimekutana na mada kuhusu mabibo hostel kwamba iwapo utapangiwa kuishi mabibo hostel basi ujiandae kuwa na tabia mbaya na chafu na hatimaye ujiandae na ku-disco, nilikaa kimya nikajua ni masihara tu kumbe dhana hii imewaathiri hadi wazazi yaani live bila chenga nimeshuhudia wazazi wakizun gumzia kuhusu mabibo hostel kwa ubaya ubaya hadi nikatamani niingilie kati kupinga hoja zao. Jamani wana JF wenzangu dhana hii ya kwamba mabibo hostel kuwa ni sehemu ya kuharibika kwa tabia za wengi pia ni sehemu ya ku-disco ni potofu na tena nailaani vikali na tena ilaaniwe na isipotoshwe tena. Kama wewe uliyepangiwa mabibo hostel ni limbukeni na zuzu na unayependa kuiga iga tabia za wengine bila kujua kilichokufikisha eneo lile basi hujapevuka akili rudi kwenu na uhairishe mwaka maana wewe ndiye wa kwanza kutuharibia sifa za hostel za mabibo. asanteni wana JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…