Wazee wa chama waliposema Mkapa aendelee 2000 kwani kulitokea mtu wa kumpinga? Au hamna hata kumbukumbu nini kilitokea kabla ya uchaguzi wa 2000 ndani ya CCM?
Naamini haya maneno yanaenezwa na watu ambao hawajui CCM inavyofanya mambo yake au magazeti ambayo yanataka kuuza habari.
habari haijataja ni kina nani lakini nadhani list tunayo na kila m2 anaijua, kuna mchangiaji mmoja ameongelea kuhusu kuona kama Malecela na wenzie watafanya nini kumsaidia JK, lakini mimi simwamini kabisa bwana Malecela aka jumanne, huyo mzee ni dakika 1 tu anakugeuka yaani hilo kundi la mafisadi likiamua kumsimamisha hata kesho anamkana kikwete hadharani, tuwe makini sana na huyo mzee nina wasiwasi mkubwa sana wa yeye kutumiwa na wapinzani wa JK
"Hizi si fedha kidogo. Lazima CCM ijipange kutumia mara tatu zaidi (Sh. 7.5 bilioni) kama inataka Kikwete apite," ameeleza mpasha habari
Hiki si kichekesho kingine! kwani akuitokea mtu mwingine akamshinda Kikwete kwenye kinyang'anyiro cha kuwania ugombea, CCM itashindwa? Ina maana kuwa nguvu za CCM ni Kikwete?Wiki iliyopita, aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Dar es Salaam, Hemed Mkali, aliliambia gazeti la NIPASHE kuwa lazima kila juhudi ifanywe "kuzima mahangaiko ya wanaotaka kugombea urais" mwaka 2010 vinginevyo CCM itaangamia.
Mkali alikuwa akisisitiza hoja ya wastaafu wa CCM ambao siku moja kabla ya kauli yake walitahadharisha mgawanyiko ndani ya chama chao, wakisema utatokana na kugombea urais mwaka kesho.
Hiki si kichekesho kingine! kwani akuitokea mtu mwingine akamshinda Kikwete kwenye kinyang'anyiro cha kuwania ugombea, CCM itashindwa? Ina maana kuwa nguvu za CCM ni Kikwete?
Kama ugombea urais unaweza kuleta ugomvi wa kiwango hiki, nini maana ya demokrasia ndani ya cahama hiki kikongwe?