Haya Mabilioni ya kikwete yananisikitishaga sana wakuu, waliopata ni wale wasio stahili na walio stahili kupata hawakupata, Mpaka leo na kesho sijajua dhumuni lake lilikuwa ni nini hasa,
wapo walio kopa wakaenda kuezekea nyumba zao, wapo waliokopa wakaenda kufanyia harusi, na hapo hapo viongozi wanajitapa wana mpango wa kuzifikia nchi kama thailand na zinginezo za asia,
Nchi hii imejaa siasa za kufa mtu na hatuwezi piga hatua za kuzalisha wajasiriamali ambao baadae watakuja kuwa ndo wanashikilia uchumi wa nchi kwa mwendo huu, hayo mabilioni bora hata wangetafutwa wajasirimali kumi pekee hapa nchini wenye muelekeao mzuri wakapewa kuliko kugawa mikopo kama pipi na bila kuangalia wanao pewa na wafanya biashara au la