Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Jumla ya madaktari bingwa 49 waliotumwa na Rais Samia wamewasili mkoani Arusha, wakipokelewa na uongozi wa mkoa huo kwa lengo la kushiriki kambi ya matibabu ya siku sita itakayohusisha wilaya zote saba za mkoa huo. Madaktari hao wametakiwa kutoa huduma kwa moyo wa huruma na kujituma kwa wananchi wa Arusha.
Wito huo ulitolewa tarehe 21 Oktoba 2024 na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Charles Mkombachepa, wakati wa hafla ya kuwapokea madaktari hao iliyofanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Mount Meru.
“Mtakaa hapa kwa siku sita kuwahudumia wananchi wa Arusha. Ombi langu ni mtoe huduma kwa upendo ili kazi yenu ikumbukwe daima na wananchi wa mkoa huu,” alisema Dkt. Mkombachepa.
Aidha, Dkt. Mkombachepa aliongeza kuwa, hatua ya Rais Samia kupeleka huduma za kibingwa hadi katika ngazi za msingi imeonesha heshima kubwa kwa Watanzania, na kuwahimiza wananchi wa Arusha kutumia fursa hiyo kwa kujitokeza kwa wingi.
Soma pia
Kwa upande wa Wizara ya Afya, Katibu wa Afya, Rahim Ngaweje, alisema kuwa kambi hiyo ni mwendelezo wa awamu ya kwanza ambayo ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa.
“Baada ya awamu ya kwanza kuwafikia wananchi takribani 70,000, serikali imeona ni muhimu kuendeleza huduma hizi kwani wananchi wengi wenye mahitaji ya matibabu ya kibingwa hawakuwa na uwezo wa kuyapata kutokana na gharama,” alisema Ngaweje.
Aliongeza kuwa, katika awamu ya kwanza walibaini kuwa baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamepewa rufaa walirudi nyumbani kutokana na changamoto za kifedha, hali ambayo ilimfanya Rais Samia kuona umuhimu wa kufanyika awamu nyingine ili wananchi wengi zaidi wapate huduma.
Madaktari bingwa, Dkt. Patrick Kushoka na Muuguzi Mkunga, Fatma Sitta, wakiwakilisha wenzao, walisema wako tayari kutoa huduma bora kwa wananchi wa Arusha na kuhimiza wananchi kujitokeza kwa wingi.
“Pia tutashirikiana na wenzetu wa ngazi ya msingi kuwapa mbinu bora za kuwahudumia wagonjwa, kama vile namna ya kumhudumia mama mjamzito anapokuja kujifungua ili kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika,” alieleza Fatma Sitta.
Source: Michuzi TV