MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Mabingwa wa kihistoria wa Ligi kuu bara club ya Young Africans, wamepata mwaliko maalum kutoka kwa Waziri wa Utamaduni sanaa na michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Bungeni Jijini Dodoma tarehe 23, 2024 ambapo aliwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa fedha 2024/25. Timu ya Young Africans ikiongozwa na Rais wao Eng. Hersi Said, Benchi la ufundi pamoja na kocha mkuu Miguel Gamondi wamepokelewa kwa makofi mengi pamoja na bashasha kubwa kutoka kwa Wabunge wakiongozwa na Naibu Spika Mh. Mussa Azan Zungu.
Club hiyo inatarajia kukabidhiwa kombe lake la 30 la LigiKuu Bara siku ya tarehe 25/05/2024 katika dimba la Benjamin Mkapa, ambapo itafikisha rekodi ya kutwaa vikombe 30 vya Ligi Kuu Bara, Rekodi ambayo haijafikiwa na club yoyote nchini na kwa sasa ndiyo timu bora zaidi hapa nchini, Afrika ya Mashariki na kati kiujumla.
Wakati huo mchezaji Aziz Stephane Ki akiongoza kwa idadi ya magoli na kutarajiwa kutwaa kiatu cha mfungaji bora wa Ligi kuu bara.