Piga ua, hao madada iwapo wameshiriki katika hili kwa malipo sidhani kama wamepata zaidi ya kilo tano tano. Ujumbe kwenye video hauna maana na zaidi unaonesha umbumbumbu wa wale waliopanga kutengeneza video hii.
Nawasikitikia akina dada hawa maana kwa chochote kile walicholipwa kushiriki katika video ni cha kupita, tena muda mfupi tu. Na baada ya hapo majuto ya kushiriki katika video yatafatia, maana video itabakia daima hadi uzeeni mwao. Kama ni watu wa kujirusha, Bills napo itabidi kuogopa kukanyaga, maana wabongo wengine hawana simile na wanaweza kuwafanyizia kwa hili. Siasa Za maji taka zina gharama yake, wawe tayari kuitoa...