Mabomu ya Arusha hayahitaji siri tena

Mabomu ya Arusha hayahitaji siri tena

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Usiri wa watuhumiwa wa mabomu ya Arusha unatisha sasa. Watu wamekufa Olasiti na Soweto. Watu wamejeruhiwa. Watu waliteseka na kulia mno juu ya jambo hili. Wapo walioachwa wakiwa juu ya kadhia hii.Na watoto yatima. Na kadhalika na kadhalika. Siri ya nini tena katika kadhia hii ya Arusha? Wananchi wote wa Tanzania wanaisubiri Serikali yao ifanye jambo la faraja na la kisheria juu ya milipuko ile ya Arusha. Si wakati wa sinema za mtu kutoka nje na kusema halafu ajibanze tena ndani.

Jeshi letu la Polisi liliunda Tume ya uchunguzi.Bado hatujaisikia imegunduaje. Yawezekana waliokamatwa sasa ni matokeo ya uchunguzi huo. Hatuna hakika. CHADEMA walidai kuwa na mkanda wa video wa kadhia ya Soweto.Wamegoma kuutoa hadi leo.Mkanda umekuwa siri. Polisi wamelazimisha kuupata mkanda huo wa CHADEMA bila mafanikio. Sehemu hiyo ya sinema ikaisha.

Sasa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo anasema kuwa 'walioingiza mabomu na kulipua Arusha' wamepatikana.Yaani wametiwa nguvuni. Mulongo anasema kuwa bado wanahojiwa na Polisi kupata taarifa zaidi zizungukazo suala hili kwa ujumla wake.Haiko wazi walikamatwa lini. Hata kama ni washukiwa wa uhalifu wa aina gani,bado wana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda unaotambuliwa na sheria za nchi. Ni saa 24 tangu kukamatwa kwao.Lakini tayari tumeshajua kuwa mabomu husika yalitoka katika nchi ya Balozi-wa-Chama yaani China. Hapa pia usiri umetanda.

Mkuu wa Mkoa analiongelea jambo hili kama nani hasa? Anahusikaje nalo kiutendaji? Kweli hakuna watendaji wahusika wa suala hili? Kuwatangaza waliokamatwa si nafasi ya kujipatia sifa. Ni jambo serious tukizingatia madhila waliyoyapata watu wa Arusha kule Olasiti na Soweto.

Wahusika wa Jeshi la Polisi wajitokeze sasa na waweke wazi nini hasa kinaendelea juu ya jambo hili.Usiri utatupa wasiwasi.Utatupunguza imani. Tutaichukulia kesi itakayofuata kama ni mchezo uliopangwa na kupangika. Halitakuwa jambo jema.Hatutaki iwe hivyo. Wahusika jitokezeni na mtueleze.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Episode mpya inatengenezwa maana zile za zamani zimechuja na hazikupata mashabiki
Na suala la wahaliifu au washukiwa analizungumzia mkuu wa mkoa badala ya polisi jua hapo ni siasa tupu na atatoka na maelezo ya kisiasa zaidi
Na ni ngumu gani kuwataja tuu majina
 
hata mimi ninashangaa sana huu usiri, wengine wanaushahidi wanauficha(Mh. mboye) watuwekee basi hata huku mitandaoni kama mnaogopa polisi watauchakachua????? mboye kweli uko serious na damu za watanzania??
 
Ni nadra kusikia Mkuu wa Mkoa akiongelea upelelezi wa jinai (criminal investigation)bila wahusika CID/polisi) kuwepo. Sijui hili la Arusha linakuwaje tofauti. Hii si Mara ya kwanza mkubwa Hutu kulitolea taarifa!
 
Hii ni Jinai dhidi ya Binadamu tuache ushabiki wa Siasa maana kuna watoto hivi sasa wanaitwa Yatima kwa sababu ya ushenzi huu, Tusubiri matokeo ndio tujadili! tusijadili tangazo la kuleta matokeo, tujadili matokeo
 
mkuu ni kwamba, vijana wetu wamefanikiwa kuingia kwenye kompyuta za serikali na kupata report nzima ya jaji Menento aliyofanya juu ya tuko la arusha.

ikulu imetoa amri kuwa report hiyo ipotezwe na isitoke hadharani milele kwasbabu finger prints za CCM zinaonekana wazi kabisa.
lakini tumeshaipata na soon tunaiachia.
 
mkuu ni kwamba, vijana wetu wamefanikiwa kuingia kwenye kompyuta za serikali na kupata report nzima ya jaji Menento aliyofanya juu ya tuko la arusha.

ikulu imetoa amri kuwa report hiyo ipotezwe na isitoke hadharani milele kwasbabu finger prints za CCM zinaonekana wazi kabisa.
lakini tumeshaipata na soon tunaiachia.
Lini hasa tujiandae Mkuu paradiso?
 
Last edited by a moderator:
hata mimi ninashangaa sana huu usiri, wengine wanaushahidi wanauficha(Mh. mboye) watuwekee basi hata huku mitandaoni kama mnaogopa polisi watauchakachua????? mboye kweli uko serious na damu za watanzania??
ile ni kesi ya jinai. serikali inatakiwa ipeleke watuhumiwa mahakamani then akina Mbowe waitwe kama washahidi na hapo ndipo atakapotoa ule ushahidi wake alio nao. tatizo hapa ni kwamba serikali inajua ilichokifanya Arusha kwa kupitia jeshi la polisi ndio maana hawawezi kupeleka watuhumiwa mahakamani then wakaumbuke wenyewe maana ile kazi serikali ndio ilifanya yenyewe
 
Ohoooooo! mimi naogopa kuchangia hoja hii kwa kuwa tu nami nina mtoto mdogo. Mambo mawili yananiogopesha kuchangia hoja hii, la kwanza ni kuwa kama kweli waliyosema CHADEMA ni kweli kuwa Polisi ni wahusika wakuu? Hivi kweli itakuwa rahisi kwa Jeshi hilo kujivua nguo na kuanika ukweli kuwa waliohusika ni waajiriwa wa Jeshi hilo? mimi naona kigugumizi katika hilo kwa Jeshi hilo kuwa tayari kujisafisha kwa jamii na kusema kweli. Hilo linaniogopesha kuwa usiri unaweza kuendelea kama chombo hicho kimehusika.
Jambo la pili linaloniogopesha ni kuwa kama kweli Jeshi la Polisi lilihusika katika saga hiyo, kwa vyovyote vile Chama chenye dola hakitaweza kusalimika katika kashfa hiyo. Hivi kweli kitakubali uchunguzi uwekwe hadharani? Ingekuwa hiyo issue hawagusi mbona Nape angeiweka hadharani kitambo na mwenzake Mwingulu angekua ameshaanza ziara za mikoani kuwaambia umma wa Watanzania kuwa wahusika wa Jambo hilo ni kina nani? Ukiona jambo linafanywa siri basi lina siri kubwa. Maskini hilo ndilo linaniogopesha kuchangia hoja yako.
Nakuonea huruma paradiso kwani sidhani kama hawatakutafuta na wewe uwaambie ulipataje taarifa. Mimi sijui chochote ila ninachoweza kujua kuwa Haki ya Damu ya Watanzania iliyomwagika ardhi haitanyamaza mpaka watendewe haki. Ukifunika kombe leo kesho wako watalifunua. Afadhali ufunuo kombe leo wakati unao wa kujitetea kuliko usubiri lije kufunuliwa wakati huna wa kukutetea.
 
Back
Top Bottom