Mabondia wanne wa Tanzania wafungwa miaka 15 jela nchini Mauritius

mpenda pombe

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
1,406
Reaction score
711
Mabondia hao ni Case Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa na Petro Charles Mtagwa.

Wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, wote walikiri makosa ya kuingiza mihadarati hiyo nchini Mauritius wakati walipokwenda kushiriki mashindano ya ndondi barani Afrika mwaka 2008.

Wakiwa mbele ya Jaji, waliiambia mahakama kuwa walilazimika kuingia katika biashara hiyo haramu kutokana na hali zao za maisha kuwa maskini.

"Tunaomba radhi kwa taifa la Mauritius", waliiambia mahakama.
"Tu watu maskini na tunategemewa na familia, watoto na wazee wetu wanaotugemea."
"Kwa dawa hizi tungepata kiasi cha Pauni £4,000". walisema
Jaji Benjamin Marie Joseph alisema katika kutoa adhabu hiyo yote hayo ameyafikiria, kwani walitoa ushirikiano mzuri wakati wote wa uchunguzi wa kesi hiyo, kulikowezesha hata wafanyabiashara hiyo, raia wa Mauritius kukamatwa.

Wamekuwa mahabusu kwa siku 1,722, sawa na miaka miatano, hivyo watatumikia miaka kumi iliyobakia jela. Pia watatakiwa kulipa faini yapauni £1,600 na gharama nyingine za uendeshaji wa kesi hiyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa BBC nchini Mauritius Yasine Mohabuth in Mauritius, Jaji aliwashutumu kwa kuukosea umma wa Mauritius kwa kuingiza dawa hizo za kulevya aina ya heroin.

Mabondia hao waliwasili Mauritius tarehe 10 Juni 2008 na kuweza kupita uwanja wa ndege bila kunaswa hadi walipokamatwa katika hoteli waliyofikia ya Quatre Bornes.

Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.
 
Sembe ni tatizo Tanzania.. Mwitanga aliachiwa huru na mahakama ya Tanzania..
 
Adhabu ndogo saasna....Tsh 10m zawaozesha jeli for 15yrs, wangekubali kusukuma mkokoteni wangepungua nini.....tamaa mbaya
 
Sasa huyo alieachiwa hapa Tanzania kama kweli ni biashara yake si anaendelea..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…